Kero ya wananchi

MKWELIMAN

Senior Member
Nov 24, 2008
126
21
Kuna siku za miezi kadhaa nilipita katika barabara hiyo nikakuta BANGO limetoa ILANI kuwa hakuna ruhusa kupita eneo hili kuanzia muda wa saa 12 jioni hadi saa 12 asubuhi
kutoka eneo la ocean road hospital mpaka karibu na Tanganyika swimming club ya waogeleaji.

Hivi majuzi nikipita nilikuta BANGO lile halipo nikapita ghafla askari wa FFU. Akatokea na kunisimamisha mimi na magari ya wangine kama kumi na kuni hoji kwa nini nimepita barabara ile.

Hii ilikuwa saa nne asubuhi, nilimwambia askari yule kuwa mimi sijui kama barabara hii imekatazwa kwani BANGO sikuliona kama limebadilishwa na kuwekwa lingine kuwa tusipite,yule askari akasema nakupeleka ukachangiye serikali au ulipe faini ya shs 30000/=

Nikamwambia nipeleke maana hunielewi kuwa sikujuwa, baada yakubadilshana maneno mahali akaniruhusu kuondoka,hawo waliokuwa nyuma yangusijui kama walichangia hizo shs 30000/=.Je hapa sio mwanya wa rushwa.

Sasa nauliza mimi na wadau wengine tunauliza barabara hii inafungwa kwa mamlaka ya nani? na kwa sababu gani?kwa sababu barabara hii tumekuwa tukiutumia tangu enzi za EDWARD TWINNING wa ukoloni mpaka tumepata uhuru mpaka uongozi wa waziri kmuu wa kwanza na rais wa kwanza ,barabara hii haikufungwa,beach hizo tulikuwa tukizitumia usiku kucha wakati wa BANDA BEACH. na kuogelea hapo usiku na mchana.

Leo iweje tufungiwe kupita tena mchana,hata kwa nisababu za usalamawa viongoziau jengo la ikulu,
basi na soko la samaki pia lifungwe maana hapo maadui ndio rahisi kufanya uhalifu, kuliko sisi tunapitakupata upepo au kuwahi kazinitukiepa foleni katika barabara zetu tuendapo kigamboni.

Naomba askari hawa wa FFU watumiwe vizuri kwa kuwakamata wauza UNGA NA WAVUTA BANGI, ambawo ndiyo wanafanyia biashara haramu kuliko kutubughudhi wapita njia.

Tunakuomba mheshimiwa rais ingilia kilio chetu hiki,usalama wa taifa ni wawote sio la FFU na mitutu ya bunduki.

Wadau wa barabarani

salaam.
 
..nami nlipita kama miezi miwili nyuma kutokea cvu...nlipofika kona ya kuingigia ocean road nkaliona hilo tangazo lao...lakin lilikataza mda wa jion si asubhi. Nkajua hao askar huwa hawana taratib za kufuata sheria wao hufuata amr wanazopewa...nkakunja kulia sikunyoosha!
Pole member!.
 
Kumbuka kuwa kuna tofauti kubwa sana kwa viongozi wa zamani na sasa. Kutokana na maovu wanayoyafanya, kila wakati wanahofu kuwa unaweza ukajipenyeza na ukawadhuru.

Pole viongozi wa leo si rafiki tena bali wako mbali sana na watu wa kawaida hata maisha ni tofauti sana! pole, ya Mungu mengi, kuna siku
 
Back
Top Bottom