nipo hap ubungo mataa zaidi ya dk 30, kisa ni askari kaamua kuongoza magari. kuna haja gani ya kuongoza magari asby yote hii askari
Siku kuu inakuja, lazima wazuge ili ukiwa na haraka, akuchomoe10,000. Lakini nawasihi acheni kutoa rushwa kwa ma-trafic, tuwe wepesi wa kulipa faini ili tuache kuwanenepesha polisi, ili watambue serikali yao haiwajali
Mimi ni mmoja kati ya wachukia rushwa na niko tayari kuchelewa safari zangu ili tu nifate taratibu na nisilipe rushwa...(On a very serious note, SINA UHAKIKA KAMA VILE VITABU VYAO VYA BARABARANI NI HALALI, na RISITI TUNAZOPEWA NI ZA KWELI NA HELA INAINGIZIA PATO TAIFA, Ndio maana nimeopt kutake a long route) Mara Nyingi Traffic akikuona una msimamo wa kukubali kosa na kuwa tayari kutoa ushirikiano wa kwenda kituoni, Huwa wanakuachia....Ni wiki iliyopita tu nilikamatwa Kingolwira kosa ni kwenda 57 sehemu ya 50, nikakubali kosa na kuwaomba waniachie niendelee na safari, wakataka fine nikatoa jibu rahisi kabisa, SINA PESA HAPA... wakataka twende kituoni nikalale hadi Jumatatu nikajibu shitaka mahakamani nikakubali (nikijua kabisa nikifikishwa kituoni sitalala kwasababu ntawaomba waniachie na Police wa kituoni huwa wanaachia tu watu kwa mambo kama hayo)... Nikakaa pale kama dakika 40 baadae wakanipa leseni yangu nikaondoka, Sasa Ningekuwa na moyo wa rushwa pale ningejifanya nataka kuwahi nikawaachia nusu ya fine (15,000) Nikaondoka... Patience saved my doe...
Tusiwe wepesi wa kujifanya tuna haraka utadhani tunawahi wagonjwa tuwafanyie operation wasife, Utasikia mtu ooh watanichelewesha. kumbe anawahi bar au nyumbani kwake... Kwani unakoenda kunahama??
Traffic ni Binadamu kama sisi, wana aibu, huzuni na huruma kama watu wengine... Ukiwa na Kauli nzuri hata siku moja hawatakusumbua.