PatPending
JF-Expert Member
- Aug 17, 2007
- 491
- 101
Kumekuwa na tabia chafu ya magari ya wizara, idara na mawakala mbalimbali wa serikali, mawaziri, spika, naibu spika, majaji na hata wanajeshi kujiona ya kwamba wao wapo juu ya sheria za usalama barabarani na hivyo kwa dharau na kejeli kubwa kuamua kutokukaa foleni na kuamua kulazimisha kupita pembeni aidha katika hifadhi ya barabara au upande mkabala wa barabara ama "kutanua" kama inavyojulikana siku hizi.
Mifano hai ipo mingi tu na ni karibia kila siku inatokea, mfano gari la Waziri wa Ulinzi halikai foleni, leo hii gari la Naibu Spika halikukaa foleni, yote licha ya kutokuwa na mwongozo wa askari polisi au ving'ora.
Hakuna sheria au kifungu chake kinachowapa haki hii na hii ni dharau na kejeli kubwa dhidi ya walipa kodi na watumiaji wengine wa barabara. Sheria ya Usalama Barabarani No.30 ya mwaka 1973 na marekebisho yake mbalimbali kuanzia yale ya mwaka 1980, 1996, n.k hayawapi ruhusa hii. Wengine wanadiriki kusema au kufikiri kwamba wao ni msafara wa kiofisi jambo ambalo si sahihi kwa mujibu wa ufafanuzi wa sehemu ya 4 kifungu namba 43(2) cha sheria hii kinachosema
"For the purposes of this section ''an official motorcade'' means
a motorcade of two or more motor vehicles escorted by or carrying a
police officer to ensure that such motorcade has a safe and unimpeded
journey to its destination"
Vile vile pia tambueni ya kwamba nyinyi si magari ya huduma za dharura kama vile sehemu ya 4 vifungu vya 54 (1), 54(2) na 54(5) vinavyoainisha.
Nawaombeni askari wa usalama barabarani mfanye kazi yenu na kuwabana hawa watu maana sisi sote tuna haraka na sio wao pekee tu. Sheria iko wazi maana watu wote wenye kutanua wanafanya makosa chini ya kifungu namba 50 kinachohusiana na "Careless or inconsiderate use of motorvehicles"
Tabia hii chafu inakera na kuhatarisha usalama wa watu, mali na vyombo vingine vinavyotumia na kuzunguka barabara.
Tabia hii chafu hutendekea zaidi majira ya asubuhi na jioni pale wakati kunapokuwa na msongamano mkubwa wa magari barabarani.
Tafadhalini jamani, kama mna haraka sana basi wahini kuamka asubuhi au kutoka kabla ya barabara kufurika.
Mnatukwaza sana sisi walipa kodi wenye kufuata sheria. Sheria za nchi ni lazima ziheshimiwe na kufuatwa na wote.