Kenyatta- Watanzania iombeeni Afrika Mashariki

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
NAIBU Waziri Mkuu wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewataka Watanzania kuiombea Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kukabiliana na matatizo yaliyo mbele yake.

Alisema bila msaada wa nguvu za Mungu ni vigumu kupata utatuzi wa matatizo yaliyo mbele ya jumuia hiyo kwani ni kikwazo cha maendeleo.

Akizungumza jana wakati wa ibada ya Mavuno katika Kanisa La Mtakatifu Joseph, Kenyatta ambaye pia ni Waziri wa Fedha, alisema msaada wa Mungu na juhudi za kila mmoja zitasaidia kutatua matatizo yaliyo mbele na kuinua uchumi wa wananchi wa jumuia hiyo.

Alisema kila mmoja kwa wakati wake anatakiwa kutenga muda wa kuombea jumuiya hiyo aliyosema inayokabiliwa na matatizo mbalimbali, ili Mungu awape busara viongozi wake katika kuyatatua.

Uhuru alisema yuko nchini kuhudhuria kikao cha masuala ya jumuia hiyo na katika ibada hiyo, aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Mambe na Balozi wa Kenya nchini, Mutindo Mutiso.

Kenyatta pia alichangia Kwaya Kuu ya Mtakatifu Joseph Dola 200 kwa ajili ya safari ya kuhubiri Injili watakayofanya Mombasa nchini Kenya kuanzia Novemba 18 mwaka huu.

Ibada hiyo iliongozwa na Padre Camilius Sawio aliyetaka waumini kutoa mavuno yao na kuomba hekima na busara kwa Mwenyezi Mungu ili kuweza kutatua masuala mbalimbali ya kimwili na kiroho.

Paroko Msaidizi wa Kanisa hilo, Edwin Igomba alisema kanisa hilo lina wajibu na nafasi kubwa kuomba kwa ajili ya nchi hususani kwa waliopotoka katika masuala mbalimbali.
 
Back
Top Bottom