Nabubujikwa na machozi hapa mbele ya luninga yangu ninapoangalia Citizen TV ya kenya wakishangilia na kuzindua katiba yao mpya. Kama una uwezo sasa fungulia uone wenzetu wanavyo rebrand nchi yao na kuingia enzi mpya ya maendeleo. Hivi sisi hasa watawala wetu hatuwezi kujifunza kutoka kwa wenzetu?
Wenyewe wametangaza kuwa ni sherehe za kuzindua Jamhuri ya pili na sherehe kubwa za pili tengu wamepata uhuru
Karume ameish fika ila Kikwete hajaingia viwanja vya Uhuru, mseveni na moi wamzomewa.
Viongozi wetu hawaoni umuhimu pia wetu wa kuwa na katba mpya, tuaingia kwenye jamhuri ya pili na kupata nafasi ya kuandika katiba yetu wenyewe kuliko hiyo iliyopo na viraka kibao
jamani tujifunze kwa hawa watu.
wakenya leo wanaanza mwanzo mpya naona rais kibaki ndo anaingia uwanjani akiwa katika landrover special ya kijeshi kumtambulisha kamaamiri jeshi mkuu