Kenyans On Street Again

KUNANI PALE TGA

Senior Member
Feb 6, 2009
138
7
Wakenya wameingia barabarani kupinga bei za bidhaa zikpanda holela kama mafuta na chakula.
Source: Aljazeera.
 
wenzetu wakiingia mitaani wanapata wanachotaka serikalini, hivi watanzania tuweze kubadilisha tactics za ku-protest na cdm jifunzeni nchi zingine anything is possible
 
Inabidi Kwanza serikali Itu-Ngeleje mwaka mzima ndio tutatia akili. La sivyo inabidi kuzoe mood ya Ngeleja kwa kwenda mbele. Kelele kwa sana, wao wanamalizia stock ya generator zao na kuuza umeme wa mafungu. Wasanii wameingia na biashara za solar panel fake, na miradi kibao ya umeme ya mifukoni. Njaa ndio hiyo imetengamaa huku mkuu wa kaya akisema yeye sio wingu. Kazi kweli kweli
 
Polisi nchini Kenya imetumia gesi ya kutoza machozi kutawanya mamiya ya waandamanaji mjini Nairobi wakipinga kupanda kwa bei ya chakula na mafuta.

100118144901_kenya-somaliarrests386.jpg


Polisi wazima maandamano


Mwandishi wetu, Robert Kiptoo akiwa mjini Nairobi anasema kuwa ummati huo wa watu ulipita katikati ya jiji ukiimba nyimbo za kukashifu wakati wakizuia mtiririko wa magari na kusababisha wenye maduka kuyafunga.

Kuna uhaba wa mahindi kote Afrika mashariki kutokana na ukame.

Serikali ya Kenya hivi karibuni ilipunguza kodi juu ya mahindi yanayoagizwa kutoka nje ili kuepusha kupanda kwa bei.

080104kenyapolice187.jpg


Maandamano kupinga gharama kubwa


Wanafunzi kadhaa wa Chuo kikuu na wanaharakati za haki za utu walikamatwa wakati wa maandamano ambayo Polisi waliyataja kama yaliyofanywa bila kufuata utaratibu wa sheria sababu hawakuomba ruhusa kuandaa maandama

Baadhi ya waandamanaji walisoma vipengee katika Katiba mpya , vilivyoongezewa mwaka jana, wakielezea haki yao ya uhuru wa kuandamana, anasema mwandishi wetu.

Hata hivyo juhudi zao za kufika kwenye afisi ya Rais na Waziri mkuu kuwasilisha malalamiko yao zilikwama pale Polisi wa kuzia fujo walipotumia gesi ya kutoza machjozi na mbwa kuwatawanya.

Mwandishi wetu anasema kuwa kupanda kwa gharama za maisha kumewaudhi raia wengi wa Kenya.

Bei ya hii leo ya mfuko wa kilo mbili ya unga wa mahindi ni sawa na dola mbili za Marekani au pauni 1.25 za Uingereza.
Bei hiyo ni kubwa kwa raia milioni 40 wa Kenya.

Waandamanaji hao pia wamewatuhumu wenye viwanda vya kusaga mahindi kwa kuhodhi mahindi ili kuona kuwa bei inapanda.

Watu takriban milioni 12 katika pembe ya Afrika wamekumbwa na ukame - ambao haujatokea katika eneo hili katika kipindi cha miaka 60.
Halikadhalika Kenya inakabiliana na mfumko wa bei huku sarafu yake ikiwa imeshuka kiasi ikilinganishwa na dola ya Marekani.
 
Wakenya wameingia barabarani kupinga bei za bidhaa zikpanda holela kama mafuta na chakula.
Source: Aljazeera.

sisi tutabaki kupiga domo tu, kawaida yetu ushabiki.. Simba na yanga, Chadema vs ccm, zitto vs makinda, mara babu wa loliondo akili zetu zote zinahamia huko and life goes on
 
Jamani polisi chonde chonde mtawaliza raia bure. Hamjui kuwa chakula ni muhimu hata kwenu nyie na familia zenu?
 
Hao ndiyo Polisi wa kwetu! Wenyewe wanajinadi professional! naona mwalimu wao mmoja tena kesha kufa Kama Tanzania; Kama Kenya.
 
ndo mana mwanakijiji amepata njozi ya kuanza kugawa chakula maeneo ya mijini kwanza.
Na hali kama hii ikitokea bongo ujue ndo mwisho wetu wa kisiwa uhuru hewa na amani miyeyusho. .
 
Kila nchi inatamaduni zake za kuishi tusipende kuiga kila wanachofanya majirani zetu naamini tunaenda vizuri na tutafanikiwa kulikomboa taifa kwa njia hizi hizi pasipo kuiga kenya wala tunisia kwani sisi tulivyo ingia mtaani kupinga kupanda bei ya sukari haikushuka jamani tusibeze jitiada kubwa anazofanya slaa na chadema kwa ujumla naamini tunaenda vyema na tutashinda soon
 
Jamani me nipo Nairobi sasa ila sipo eneo la tukio lakini huku maisha ni gharama mno,hata Tanzania hatuoni ndani......
 
wenzetu wakiingia mitaani wanapata wanachotaka serikalini, hivi watanzania tuweze kubadilisha tactics za ku-protest na cdm jifunzeni nchi zingine anything is possible

Niliyaona yale maandamano ya jana na waandamanaji wale walichokipata ni kipigo na kukamatwa na hakuna kilichobadilika kwenye yale yaliyowasukuma kuandamana. Sasa sijui kama hicho ndicho walichokitaka!
 
Jamani me nipo Nairobi sasa ila sipo eneo la tukio lakini huku maisha ni gharama mno,hata Tanzania hatuoni ndani......[/QUOT

They the grass is greener on the other side, till you get there to see for yourself!
 
DNFOODDEMO0707CF.jpg


Members of civil society protest in Nairobi on July 7, 2011. Ten people were arrested and police forced to lob several teargas canisters to disperse the group of Unga Revolution campaigners who were pressing for a reduction in the cost of flour and the sacking of Education minister Prof Sam Ongeri



DNFOODDEMO0707HJ.jpg



DNFOODDEMO0707C.jpg



DNFOODDEMO0707hj.jpg



 
Back
Top Bottom