Kenyan, Tanzanian ivory seized in China!

Yaaani jamani hivi watanzania hasa viongozi wa umma wanasikilizia wapi?
Hapa kinachotakiwa kwenye katiba mpya ijayo tuweke kipengele cha kuwa :Rais akifanya jinai basi ashitakiwe na kuchukuliwa hatua kisheria.maana tukifanya hivyo moja kwa moja tutakuwa tumeweka wazi kuwa kiongozi anawajibishwa,kuliko katiba ya sasa ambayo ibara ya 45 na 46 zina mpa kinga mtawala kitu ambacho huwafanya kufanya makosa kwa makusudi.
Mfumo wetu wa kiutawala sio mzuri unawapendelea sana viongozi na wana siasa.kwa maana hiyo Rais amelundikiwa madaraka mno kiasi ambacho yanamshinda na badala yake mam:hungry:bo yanakwenda hovyo hovyo na kuonekana kama vile serikali imekwenda likizo kumbe ipo.
 
kweli hii nchi imetapakaa rushwa,lakini mwakyembe si alimsimamisha kazi mkurugenzi wa TPA kwa tuhuma za rushwa?naskia kuna mkurugenzi mpya pale.
 
Baada ya Tanzania kuomba tena kibali cha kuuza stock yake ya pembe za ndovu zaidi ya kilo 101,005 wiki iliyopita na kujiwa juu na vyombo vya mazingira, Hong Kong imekamata makontena mawili kutoka Tanzania na Kenya yakiwa yamesheheni pembe za ndovu zaidi ya kilo 3,628 zenye thamani ya dola za Kimarekani million 3.4 (sawa na Sh. Bilioni 4.4).

Mamlaka husika upande wa Tanzania walipoulizwa walikataa kusema lolote. Waziri husika Mh. Khamis Kagasheki alikataa kusema lolote akidai atatoa statement baada ya kupata details zaidi. Lakini amekubali anazo taarifa za kukamatwa kwa makontena hayo yakiwa yamesheheni pembe za ndovu.

Maafisa wa Hong Kong walitonywa na Wachina kuwa kuna mzigo ulikuwa unaingia Hong Kong kutoka East Africa hivyo waukague. Baada ya kutonywa wakakaa mkao wa kula wakisubiri mzigo uingie. Ulipoingia tuu wakakagua kontena la kwanza kutoka Tanzania ambalo wahusika walisema lilikuwa limebeba mabaki ya plastiki na maharage na kukuta pembe za ndovu zenye dhamani ya dola za Kimarekani milioni 1.7.

Siku iliyofuata kontena la pili kutoka Kenya liliwasili na kukutwa na pembe za ndovu zenye dhamani ya dola milioni 1.7. Watu saba akiwemo raia mmoja wa Hong Kong wamekamatwa na China.

Mamlaka husika Hong Kong wanasema kuna uwezekano makotenta mengine yamepelekwa nchi nyingine kama Japan, Taiwan na kwingineko.

Hii habari imesambaa sana kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Ila hapa bongo nimeona gazeti moja tuu ambalo limeandika hii story (The Citizen). Unaweza kujichagulia links mbalimbali kuhusu hii habari hapa: Country Disowns Tusks Seized in Hong...

Sehemu ya mzigo uliokamatwa kama unavyoonekana kwenye picha. Kwa nchi za wenzetu, lazima watu waachie ngazi. Kwetu huu ni upepo utapita tuu.

ivory_2375009b.jpg
 
Nji hii ina wenyewe,wengine wasindikisaji tu,lakini bora salama,kama Twiga mmoja tena live alisababisha watu kufukuzwa kazi,sijui Bro Kaga atasemaje kuhusu hawa Tembo 604 waliouwawa na kutolewa meno yao,tena meno yao yakapitia bandarini yakakaguliwa na usalama wa Taifa ,POLISI, TRA wakaweka seal zao kisha TICKS wapakia katika meli mpaka Hong Kong,huo mlolongo wote nao atawashughulikia?mbona hakuwashughulikia wale wa KIA ili ujue kuwa ulichofanya ni uonevu shughulikia na hili sasa,uone jinsi mtandao unavyofanya kazi waweza mkuta mkeo nae yumo.Hivi sasa umezidisha ukali kwa watumishi wanyonge kwa kuwafukuza fukuza kazi badala ya kuwapa motisha wafanye kazi kwa bidii haya ndiyo matokeo yake.Majangili yamepandisha bendera yana furahia utumishi wako na watumishi nao wanakuangalia ukicheza ngoma yako ya mtu mmoja.kuna usemi unasema kunguru mwoga hukimbiza bawa lake hivyo ujue watumishi wote unaowaongoza kwa mabavu wamekimbiza mbawa zao kuangalia jinsi unavyokatika kwa ngoma yako ya mtu mmoja.
 
Inawezekana kweli huu mzigo ulipita kimya kimya bila a go head ya mkubwa fulani?
 
Hivi tuliowapa dhamana ya kuongoza nchi hii wako wapi?Mbona kila kukicha kuna sinema zinaendelea na hakuna wa kusimama na kukemea?Kweli mpo likizo.
 
Inawezekana kweli huu mzigo ulipita kimya kimya bila a go head ya mkubwa fulani?

Kwa hili hakuna go ahead ya mkubwa ni uchafu wa watu wachache wasiokuwa na huruma ya wanyama wa nchi hii,wakishirikiana na watu wa nje haswa hawa wachina tunaowaabudu kujenga barabara zetu kumbe wana lao jambo.
 
Pembe za mwanzo zilizokamatwa kulikuwepo na maneno mazuri kuwa serikali yetu itafuatilia lakini kimya hadi leo.ukiangalia sana inawezekana ni sababu tosha zilizonyima serikali kibali cha kuuza pembe.kwa sasa zimekamatwa nyingine zimetoka Tz na kenya kampuni zinazosafirisha mali nje lazimaziwe na fiziko address na inawezia kuwa sio mara ya kwanza kupeleka mzigo kama huo ila arobaini yao imefika.je aliyeizinisha kwa kukagua kontena hilo lazima afahamike.na ukimchunguza atakuwa kwa shift yake anakuwa ndiye mpitisha makotena ya kampuni hiyo ya kupeleka MABAKI YA PLASTIC CHINA.Mkiendelea kumchunguza mtamkuta na mahekalu na si ajabu kumkuta anatembea na magari ya bei mbaya na akaunti ambayo mbwa haruki.kazi kwa Mwema na intelijensia yake.wakishindwa hii ambayo wana sehemu ya kuanzia wajue wazi MAMILIONI ya USWIZI na kwingineko hawataweza.IFIKE MAHALI WATU WENGINE WALIOKO JUU YA SHERIA WATURUDISHWE KATIKA USAWA.tuache kusikia wanaohusika ni vigogo bali tusikie KIGOGO kakamatwa akitaka kiliibia taifa.
 
Kwa hili hakuna go ahead ya mkubwa ni uchafu wa watu wachache wasiokuwa na huruma ya wanyama wa nchi hii,wakishirikiana na watu wa nje haswa hawa wachina tunaowaabudu kujenga barabara zetu kumbe wana lao jambo.

Haya....
 
Wanabodi,

Maofisa Forodha wa Hong Kong wamekatama kontena mbili za pembe za ndovu zenye thamani ya Dola za Marekani 3.4 milioni (wastani wa Sh5.4 bilioni), zilizotokea Tanzania na Kenya.

Pembe hizo, vipande 1,209 vyenye uzito wa tani nne, zilikamatwa juzi nchini humo zikiwa kwenye kontena mbili ambazo ziliwekwa alama kuwa zimebeba plastiki chakavu na maharagwe aina ya roscoco.

SOURCE: MWANANCHI OKTOBA 22, 2012.
 
itakuwa ni michongo ya wafadhili wa chama wanakusanya pesa za kuwanusuru 2015 bila shaka
 
Baada ya Tanzania kuomba tena kibali cha kuuza stock yake ya pembe za ndovu zaidi ya kilo 101,005 wiki iliyopita na kujiwa juu na vyombo vya mazingira, Hong Kong imekamata makontena mawili kutoka Tanzania na Kenya yakiwa yamesheheni pembe za ndovu zaidi ya kilo 3,628 zenye thamani ya dola za Kimarekani million 3.4 (sawa na Sh. Bilioni 4.4).

Mamlaka husika upande wa Tanzania walipoulizwa walikataa kusema lolote. Waziri husika Mh. Khamis Kagasheki alikataa kusema lolote akidai atatoa statement baada ya kupata details zaidi. Lakini amekubali anazo taarifa za kukamatwa kwa makontena hayo yakiwa yamesheheni pembe za ndovu.

Maafisa wa Hong Kong walitonywa na Wachina kuwa kuna mzigo ulikuwa unaingia Hong Kong kutoka East Africa hivyo waukague. Baada ya kutonywa wakakaa mkao wa kula wakisubiri mzigo uingie. Ulipoingia tuu wakakagua kontena la kwanza kutoka Tanzania ambalo wahusika walisema lilikuwa limebeba mabaki ya plastiki na maharage na kukuta pembe za ndovu zenye dhamani ya dola za Kimarekani milioni 1.7.

Siku iliyofuata kontena la pili kutoka Kenya liliwasili na kukutwa na pembe za ndovu zenye dhamani ya dola milioni 1.7. Watu saba akiwemo raia mmoja wa Hong Kong wamekamatwa na China.

Mamlaka husika Hong Kong wanasema kuna uwezekano makotenta mengine yamepelekwa nchi nyingine kama Japan, Taiwan na kwingineko.

Hii habari imesambaa sana kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Ila hapa bongo nimeona gazeti moja tuu ambalo limeandika hii story (The Citizen). Unaweza kujichagulia links mbalimbali kuhusu hii habari hapa: Country Disowns Tusks Seized in Hong...

Sehemu ya mzigo uliokamatwa kama unavyoonekana kwenye picha. Kwa nchi za wenzetu, lazima watu waachie ngazi. Kwetu huu ni upepo utapita tuu.

ivory_2375009b.jpg
Watanzania ni deadly bana eh!......kuna uwezekano mkubwa kuwa kukamatwa kwa wizi huu kumesababishwa na watanzania kufanyiana fitna kwenye deal....very possible....maana hata 'tip off' yenyewe imetoka Guang dong (China)wakati mzigo umekamatiwa Hong Kong.....Kuna uwezekano mkubwa pia kuwa hii tip off iliyopelekea mzigo huu(container)kukamatwa ni mpango mzima wa kuvuruga mpango wa serikali ya Tz kuuza nyara zake kwenye masoko ya kimataifa baada ya kuruhusiwa na CITES....hizi zinaweza kuwa endelezo la watanzania kuharibiana deal.....haswa baada ya kuona kuwa wapo watakaokosa ulaji......Nimeona sana watanzania kufanyiana ubaya...kwa sababu za wivu tu....haswa wanapokuwa nje ya nchi.....nimeshuhudiaga jamaa (wabongo)wanamlipua(kumripoti kwa immigration authorities) mwenzao(mbongo aliyeoza/kuishi bila kibali nchi fulani)..kisa eti jamaa amepata hela kuwazidi(wao wakiwa wanaishi kama raia wa nchi hiyo).......haya mambo yapo mzee.........
 
Kagasheki aliahidi kujiudhuru kama yatatokea makosa ya kizembe kwenye wizara yake, ngoja tuone.
 
wale wafanyakaz wanaousika na ukaguz na vibali bandalin wako wap? walikuwa wanafanya nini,watimuliwe mara moja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom