Kenya yamhamishia al-Faisal Gambia

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,822
NAIROBI,Kenya

SERIKALI ya hapa imemuhamishia nchini Gambia muhubiri wa Kiislamu raia wa Jamaica anayelaumiwa kwa kuhubiri chuki baada ya kuingia nchini kinyemela.

Abdulllah al-Faisal alikamatwa wiki iliyopita na kumekuwa na taarifa za kutatanisha kuhusu mahali alipo.

Waziri wa Wizara ya Uhamiaji nchini, Otieno Kajwang amesema muhubiri huyo alichagua mwenyewe apelekwe Gambia.

Amesema kulikuwa na matatizo kuhusu apelekwe wapi muhubiri huyo, kwa kuwa nchi nyingi zilimkataa, hata kupitishiwa ndani ya mipaka yao.

Kajwang amesema al-Faisal amehamishwa kutokana na historia yake ya kuhusika katika vitendo vya kigaidi.

Muhubiri huyo ameshawahi kufungwa jela nchini Uingereza kwa kipindi cha miaka minne baada ya kupatikana na kosa la kuchochea kuuawa kwa Wayahudi na Wahindu.

Kumekuwa na malalamiko kutoka makundi ya kiislamu ya kutetea haki za binadamu kuhusu namna al-Faisal alivyochukuliwa.

Faisal alizaliwa mjini St James, Jamaica na kupewa jina Trevor William Forrest , na akaondoka huko kwenda Uingereza miaka 26 iliyopita.

Wazazi wake walikuwa maofisa wa kanisa la Jeshi la Wokovu , na alilelewa kama Mkristo.

Hta hivyo alipofikisha umri wa miaka 16 alikwenda nchini Saudi Arabia ambako inaaminika alikaa kwa kipindi cha miaka nane na bubadiri dini na Muislamu.

Ianelezwa kuwa baada ya kubadili dini aliingia chuoni mjini Riyadh na kupata shahada ya masomo ya Kiislamu kabla ya kurejea nchini Uingereza.

Baada ya kufukuzwa kutoka Uingereza mwaka 2007 alikwenda kuhubiri nchini Afrika Kusini.

Serikali ya hapa inasema kuwa al Faisal aliwasili nchini humu Desemba 24 mwaka jana baada ya kupita katika nchi za Nigeria, Angola, Msumbiji , Swaziland , Malawi na Tanzania.
 
anahubiri dini au ugaidi? tatizo la dini ya wenzetu hii, kila mtu anaiogopa, kwasababumwanzilishi wake aliipokea mojakwa moja toka katika kiti cha ibilisi shetan.
 
Back
Top Bottom