Kenya yachoma moto pembe za ndovu zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 200

JAMII-ASM

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
1,305
524
CZt4XujWcAEJvaS.jpg

Haitakuwa mara ya kwanza kwa Kenya kuchoma moto pembe za ndovu. Hii ni katika sifa au ''legacy'' za kupigiwa mfano alizoacha Mzee Arap Moi,kwani yeye ndio muasisi wa uchomaji pembe za ndovu Afrika.

Rais Kenyatta kaamua kuivunja rekodi ya Mzee Moi. Kenyatta kaamua kuchoma pembe za ndovu zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 120 ,sawa na shilingi za kitanzania bilioni mia mbili. Pembe hizi zina uzito wa tani 120 na inasadikiwa zilitokana na mauaji ya tembo elfu nne.(4,000) .Huu ni mzigo mkubwa kuliko yote duniani kupigwa moto.

Tukio hili ,litakalo fanyika mwezi Aprili ,litahudhuriwa na watu maarufu duniani , akiwemo Leonardo Di Caprio (wa muvi ya Titanic), Nicole Kidman,mchezaji maarufu wa basketball mchina Yao Ming.
Matajiri wakubwa duniani Paul Allen (muasisi wa Microsoft),mtoto wa Warren Buffet aitwae Howard Buffet (huyu aliwahi kuwafadhili helikopta TANAPA lakini bahati mbaya helikopta ilipata ajali na kuua rubani),George Soros,mwanamuziki shoga Elton John..na tajiri Michael Bloomberg.

Inaaminika Tanzania tuna mzigo mkubwa sana..kuliko huu.Lakini tumegoma katakata kuuteketeza. Huko unakotunzwa una usalama kiasi gani ... labda wadau mnipashe.
Leonardo DiCaprio and Nicole Kidman to Attend Torching of Largest Ever Ivory Stockpile to Help Put an End to Poaching
Video ya Kenyata akichoma tani 15
 
Yaan kenyata ni mshenzi anachoma mabilioni bora angeifadhi ziwe ni asset
Hivi unamfahamu vizuri huyu dogo..Ni katika watu matajiri wakubwa mabilionea duniani..familia yake inamiliki mbuga za wanyama na fukwe za bahari. Ni tajiri usipime.
 
Duh,,wanachoma asset, pesa iyo,bora wangeziifadhi,,maana baadae tembo duniani wataisha,wengeziuza kwa Hela ndefu kuimarisha kikosi cha kupambana na ujangili wa wanyama wengineo
 
Tanzania inaendelea kuzihifadhi ingawa wakati mwingine "watu" hupata dili humo. Ndiyo maana kuna mashirika yalijitolea kuzihifadhi nje ya nchi. Wazo la kuziweka nalikubali, tatizo ni hao mchwa.
 
Safi sana!! Kuziweka / Kuzitunza ni kuzidisha balaa za Bure tu maana hiyo ni "mali" iliyotokana na mauaji ya mnyama ambae ana roho!!
 
Nini lengo la hao waalikwa kushiriki ktk uchomaji wa Pembe za ndovu??
 
Tanzania sijui tutachoma lini, au wanampango wa kuziuza?
Tanzania imepigia kampeni marufuku au zuio la uuzwaji wa pembe...Mwaka 1990 ''ban'' ikawekwa..lakini Hongkong na Japan ikiungana na South Africa,Zimbabwe,Namibia na Botswana walipinga sana.
''Tanzania, attempting to break down the ivory syndicates that it recognised were corrupting its society, proposed an Appendix One listing for the African Elephant (effectively a ban on international trade). Some southern African countries including South Africa and Zimbabwe were vehemently opposed. ''
Ivory trade - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Nini lengo la hao waalikwa kushiriki ktk uchomaji wa Pembe za ndovu??
Hawa ndio wafadhili wakuu wa shughuli za uhifadhi Afrika,Asia na Amerika.Na huwa wanafadhili miradi ya mabilioni (in us dollars).Kama huyo Howard Buffet ana miradi mingi ya uhifadhi nchini.
 
Na wewe unaamini zilikuwa tani 120 tu?
Huu mzigo wa tani 120 unaandaliwa kuchomwa. Utachomwa mwezi wa nne. Huo kwenye video tani 15 ulichomwa mwaka jana.Uhuru atazichoma kweli.Si utani.Kapania.
 
Naomba kufaham.Huwa kuna tatzo gan kama nchi inaamuwa kuuza mzigo kama huo na pesa zikaingia kueleza nchi badala ya kuzichoma?
 
Back
Top Bottom