Kenya: Viongozi fisadi sasa walanguzi wa silaha?

Huduma

Member
Jan 26, 2008
68
1
YAPO madai kubwa kuwa japo serikali ya Kenya inadai shehena ya silaha toka Ukraine ni zake lakini ukweli ni kwamba silaha hizo ni mali ya viongozi na wakuu wa jeshi wa nchi hiyo ambazo wamezinunua kwa ajili ya kuilangua Sudan ya Kusini.

Hivi sasa viongozi hao wanajaribu kuwazima mdomo wale wote wanaokanusha kuwa silaha hizo si mali ya majeshi ya Kenya.

Kenya ambayo inapakana na Sudan kwa hivi sasa inanufaika sana na biashara na Sudan ya kusini.

Ipo ajenda ya kidini pia na viongozi wa Kenya kutumiwa na Marekani katika vita vya ugaidi kwa kuhakikisha Sudan inagawanywa katika mapande mawili-ile ya Wakristo na jengine la Waislamu.

Polisi wa Kenya wametajirika haraka sana katika miaka ya hivi karibuni kwa kutumia kofia ya vita dhidi ya Ugaidi kuwadhulumu au kuwafutia uraia na hata kuwaua Waislamu matajiri mkoa wa Pwani wasiokuwa na hatia.

Hata hivyo Waislamu wengi katika nchi hiyo ni waoga na walioshindwa kuungana ili kupambana na adui yao na badala yake wanapigana wenyewe kwa wenyewe ikiwemo na kuchongeana kwamba huyu au yule ni gaidi kwa sababu tu ni adui ya mwingine.

Biashara ya ulanguzi wa silaha sio kitu kigeni. Viongozi na matajiri wa nchi hiyo wamenufaika sio haba na kulangua siasa Burundi, Rwanda, Congo, Somalia, Chad na Uganda wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko.

Bandari inayotumika zaidi kwa biashara hii ni Mombasa na husimamiwa na jeshi la nchi hiyo kwa amri toka juu.

TANZANIA ina kila sababu ya kuwa makini sana katika kuingia kwenye ushirikiano au muungano na nchi ambazo zinaongozwa na watu ambao wako tayari kusababisha watu kuuana ili wao watajirike na kuishi kifahari!
 
Hicho sio kitu kigeni hata kidogo ,niliwahi kwenda sudan ya kusini mwaka huu kwenda kufanya haya na yale niligundua kwamba wanajeshi wengi wanaopogana upande wa waasi sio wasudani wenyewe ni kutoka nje haswa kenya , urusi na baadhi ya nchi za ulaya na ndio hawa wanaotoa hizo silaha kwa ahadi ya kupatiwa mikataba minono ya mafuta hapo watakapojitenga mbeleni
 
kenya wenzetu wanajua kufaidika na fadhila zao..sisi tungetaka kufaidika tungetakiwa kuwa mbali...fikiria..uganda,zimbabwe,msumbiji,angola,namibia,south africa...congo...serikali yetu haifaidiki wala wafanyabiashara hawajaitumia influence ya misaada yetu kuleta utajiri nyumbani...sasa kama kenya wameamua kunufaika na sudan kusini kwa sababu ya misaada waliyowapa...wacha wafaidike ..maana siisi tumelala!!!
 
Back
Top Bottom