Kenya&Olimpiki 2012-Medali&Kutangaza Vivutio Vs TZ&Olimpiki2012-Visingizio

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
6,983
6,237
Wanajamvi!
Wakati jirani zetu wa Kenya wameandaa kwa muda mrefu timu/wachezaji zao za Olimpiki hususani RIADHA,NDONDI kwa ajili ya Riadha, tena walikabidhiwa Rasmi Bendera ya Taifa na Rais Kibaki IKULU Nairobi, na kufuatiwa na hotuba nzito toka kwa Waziri wa Michezo then Mhe. Rais Kibaki zote ni katika kuwapa moyo ili wafanye vizuri huko LONDON kwenye olimpiki.

ZAIDI, KENYA wamefungua sehemu ya Maonyesho inaitwa KENYA HOUSE hapo LONDON ambapo wanaonyesha vivutio(utalii&uwekezaji vinavopatikana Kenya), wiki ya kwanza ya Michezo hiyo Rais Kibaki atakwenda London while wk ya 2 Waziri Mkuu Odinga atakwenda huko pia. Sasa Tujilinganshe na sisi wa Tanzania tumejiandaaje? timu zetu zimeandaliwaje?tutegemee medali? tumetumia vipi nafasi hii ya olimipki kutangaza vivutio vya utalii na uwekezaji? au ndio watendaji wa serikali/wizara ya michezo na TOC wamekalia kugombea kuwepo kwenye list ya kwenda LONDON ili wapate Per Diem Allowance? Filbert Bayi,Dkt. Mukangara&Makala mna jipya?kwa style hii ya kuwa na uongozi uozo namna hii kwa nini wakenya wasitudharau? tuna kila kitu TZ kuanzia Vivutio vya utalii, Vijana wenye vipaji ila tumekosa VIONGOZI WABUNIFU.
 
Tumepeleka Wanamichezo 6 hatujui wamejifunza kambi gani; Wameagwa na Leonard Thadeo pale Airport Viongozi

Walioambatana na hao Wanamichezo 6 ni 20 karibia wote wa kamati ya Olympic, Riadha, Ndondi wakati Bondia ni Mmoja;

Swimming wakati Muogeleaji ni Mmoja. na viongozi wa wizara
 
Wanamichezo 6 wanaongozwa na Viongozi 20?! Hii kali, ratio ya 1:3, Inatisha!!!!
 
Back
Top Bottom