Kenya na Tanzania zashuka orodha ya Fifa

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Kenya kwa sasa wamo nambari 115 nao Tanzania nambari 130.

Harambee Stars wameshuka baada ya kushindwa mechi mbili za kufuzu kwa Kombe la Mataifa Bingwa Afrika na Guinea Bissau.

Taifa hilo la Afrika Magharibi limepanda hatua 45 hadi nambari 102.

Guinea Bissau waliichapa Kenya 1-0 mechi ya kwanza tarehe 23 Machi na kwenye mechi ya marudiano wakashinda tena 1-0 jijini Nairobi.

Tanzania hawajahesabiwa mechi yoyote ya karibuni. Walishinda 1-0 dhidi ya Chad mechi ya kwanza ugenini lakini Chad wakajiondoa na hawakushiriki mechi ya marudiano jijini Dar es Salaam. CAF ilifuta matokeo hayo dhidi ya Chad katika kundi G.

CAF: Chad yajiondoa, Tanzania mashakani
Miongoni mwa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uganda inaongoza ikiwa nambari 72, Rwanda inafuata nambari 87, Kenya nambari 115, Burundi nambari 122, Tanzania nambari 130 na Sudan Kusini nambari 155.

Orodha ya mataifa kumi bora Afrika ni kama ifuatavyo:

  1. Algeria
  2. Ivory Coast
  3. Ghana
  4. Senegal
  5. Misri
  6. Cape Verde
  7. Tunisia
  8. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
  9. Guinea
  10. Congo
Duniani, orodha ya kumi bora ni kama ifuatavyo:

  1. Argentina
  2. Ubelgiji
  3. Chile
  4. Colombia
  5. Ujerumani
  6. Uhispania
  7. Brazil
  8. Ureno
  9. Uruguay
  10. England
Habari kutoka BBC
 
huwa najiuliza hao ubeligiji kigezo gani kimewafanya wawe wa pili na kuna kipindi waliongoza mechi yao ya mwisho tuu friend mechi na ureno walikaa iyo ipo kwa ajili ya magwiji nini..Amerika ya kusini timu ni kali Argentina na Brazil wanatafuta sare mbona muda wote haziwi juu ...
 
Kama Argentina ipo namba 1 na Spain top 10 kwangu inatosha hao Tz hata wakipitwa na Tahiti kwangu hainipunguzii lolote
 
huwa najiuliza hao ubeligiji kigezo gani kimewafanya wawe wa pili na kuna kipindi waliongoza mechi yao ya mwisho tuu friend mechi na ureno walikaa iyo ipo kwa ajili ya magwiji nini..Amerika ya kusini timu ni kali Argentina na Brazil wanatafuta sare mbona muda wote haziwi juu ...

Vigezo ni vilevile ambavyo vinaifanya Tz iwe karibu na mwisho. Ubelgiji kwa miaka 3-4 iliyopita imekuwa kwenye kiwango cha juu sana hadi kiasi cha kupewa nafasi ya kutwaa kombe la dunia huko Brazil 2014. Usiichukulie poa.
 
...Rwanda 87, then Tanzania 130, hebu tuanze kuuliza kama kuna aliyetulaani tukamuombe msamaha!
 
Vigezo ni vilevile ambavyo vinaifanya Tz iwe karibu na mwisho. Ubelgiji kwa miaka 3-4 iliyopita imekuwa kwenye kiwango cha juu sana hadi kiasi cha kupewa nafasi ya kutwaa kombe la dunia huko Brazil 2014. Usiichukulie poa.
sina kumbukumbu vizuri,lakini sioni kikubwa kilichofanywa na belgium kushika namba 2
 
baba kiki nina kumbukumbu ya mpira wa miguu tokea 1990 mashindano ya kombe la dunia au mechi za kawaida hakuna walichokifanya hao ubeligiji mkuu huwezi pata nafasi ya juu kwa msimu mmoja hata kombe ls ulaya hana wala kombe la dunia hata moja hana hao uholanzi kila msimu wanatoka nusu fainali inakuaje kama ni kufuata kombe la dunia pekee..
 
ubeligiji hawawezi kuwafunga colombia,uruguay hata chile mechi saba zile ndio awe nafasi ya kwanza duniani? blatter mcheza dili sana aisee
 
Back
Top Bottom