Kenya: Madaktari kugoma kisa malipo hewa ya Bima ya afya kwa hospitali hewa

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Katika nchi jirani hapo KENYA chama cha madaktari Kenya KOSATU ( samahani kama nimekosea) kinaandaa mgomo wa nchi nzima Baada ya Katibu mkuu wa wizara wakishirikiana na bodi ya Bima ya Afya nchini humo ( NHIF) kulipa malipo hewa kwa hospitali ambazo hazipo zaidi ya shilingi za Kenya Mil 3.

Hivyo chama hicho cha madaktari wanawataka Waziri, katibu wake wa wizara na mkurugenzi wa NHIF kujiuzuru na kufikishwa mahakamani kwa ubadhirifu na ufisadi wa mali ya umma.

My take:

Hapa kwetu mchezo huu haufanywi kweli maana sie wafanyakazi wanatulazimisha kujiunga na bima ya afya na wanatukata kweli na huduma ni mbovu. Kila siku sie watu wa bima hakuna dawa na vipimo vya muhimu tunalipa wenyewe.

Nadhani Brandina Nyoni na Kina Nkya watakuwa wanaijua hii biashara vizuri
 
Ufisadi kwa kweli ni jadi katika Afrika. Hapo kuna wajanja wanajipanga kwa ajili ya uchaguzi wa urais unaofuata. Wizi wizi wizi wizi kila mahali kwa lengo la kujitumiki. Ni lini viongozi wetu wataacha kujitumikia na kuwatumikia wananchi??? Mungu shusha kiberiti kama kile cha sodoma na gomora! Khhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Back
Top Bottom