Kenya kutumia vivutio vya utalii vya Tanzania katika ndege zao ni sahihi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Wakati tukiendelea na kampeni ya kuutarifu ulimwengu kuwa "Olduvai Gorge" ipo Tanzania na si Kenya kama ambavyo Mwanadada wa Kikenya alivyouambia ulimwengu,katika mitandao ya kijamii kumezidi kusambaa kwa picha za ndege ya KQ aina ya B777 inayoonyesha "Fuselage Name" ya "Mt.Kilimanjaro".Hali hii imezua malalamiko mengi kwa watu mitandaoni na kusababisha watu kuona Kenya wanatumia vivutio vyetu kuitangazia dunia kuwa vinapatikana nchini kwao Kenya.Hii inatokana na malalamiko ya muda mrefu ya Tanzania kuituhumu Kenya kupata watalii kwa mgongo wa vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.

Ukweli ni kuwa hakuna "makosa" yoyote ambayo Kenya kupitia ndege za shirika lake la Taifa(National Carrier) la Kenya Airways linafanya,kwenye ulimwengu wa usafiri wa anga,shirika la ndege la Taifa huwa ni kama "Flying Ambassador".Kuiwakilisha nchi na yote yanayoihusu kule inapokwenda na kutua,zaidi ya yote mashirika haya yamekuwa yanatumia "fuselage name" za vivutio vya utalii kuelezea ulimwengu kuwa ukipanda shirika hili la ndege basi unaweza kufika mahali fulani palipo na kivutio fulani.Kwa upande wa Afrika Mashariki,shirika la ndege la KQ limekuwa likitumia "fuselage name" kama "Mt Kilimajaro","Victoria Falls","Maasai Mara" nk kuulezea ulimwengu kuwa popote unapokuwa duniani ukipanda Kenya Aireays utafika katika vivutia hivyo.

"Fuselage Name" haifanywi na KQ(Kenya Airways) tu,bali hata shirika la ndege la KLM limekuwa likitumia "fuselage Name" ya "Mt Kilimajaro" kwa ndege yake moja aina ya B777 PH-BQP inayofanya safari zake toka Ulaya kwenda nchi za Asia.Hii inawasaidia KLM kupata abairia wengi wanaotoka nchi za Asia na kutaka kuja Mlima Kilimanjaro,kuonekana kwa fuselage name hii itafanya abiria wengi kukata tiketi za KLM wakijua kuwa watafikishwa moja kwa moja kuuona Mlima Kilimajaro,itakumbukwa kuwa shirika la KLM hufanya safari zake kila siku kutoka Amsterdam-Kilimajaro(KIA)-Dsm na baadae kurudi Amsterdam.

Hii haifanywi na KLM na KQ tu,hata shirika la ndege la Ujerumani baada ya kuzindua ndege yake mpya aina ya Airbus 380(A380) imeipa ndege hiyo jina la "Johanesburg" sababu limeanzisha safari za kwenda Afrika ya kusini.Ndege nyingi za Swiss Air zina majina ya vivutio vinavyopatikana nchi nyingine za Ulaya,na hivyo kuwahakikishia abiria kuwa wakipanda Swiss Air wana uhakika wa kufika katika vivutio hivyo vya utalii.

Kuna mambo ya kulalamikia lkn si haya,sisi tunapaswa kuirudisha ATCL yenye nembo ya Twiga wetu anagani.Pembeni ya ndege zetu za ATCL kulikuwa na maandishi yameandikwa "WINGS OF THE KILIMANJARO",lakini pia ndege nyingi za ATCL zilikuwa na "fuselage Name" kama "Serengeti","Manyara","Ngorongoro","Zanzibar" nk.Leo tunao Precisiona Air wanafika Nairobi tu...baadhi ya "Fuselege Name" zake ni "Rombo","Kilimajaro","Iringa","Musoma" na "Mwanza".Tuache kulalamika kwa baadhi ya mambo,tusideke kwa kuombaomba "huruma" ya kuonyesha tunadhulumiwa,dunia ya leo ni "ubabe" na "ukatili" wa kutetea cha kwako na kulinda vyako.Nilipofuatilia mzungumzaji baada ya Miss Odinga kwenye lile Kongamano la IYLA aliposema "Olduvai Gorge" ipo Kenya,mzungumzaji aliyefuatia alikujai kuzungumzia "Maendeleo ya Technolojia na Vijana",kabla ya kuanza mada yake akasema "Ninamshukuru leo Rosemary,nilikuwa najua Olduvai Gorge ipo East Africa,lakini leo nimejua mahususi kumbe ipo Kenya,ndio uzuri wa kukutuianisha vijana toka nchi mabalimbali ulimwenguni".Bado naendelea kufuatilia majina ya vijana wa Kitanzania walioshriki mkutano huo wa IYLA na kwanini hawakujibu hapo hapo,lakini toka August 215 leo baada ya mitandao ya kijamii kama JamiiForums kuibua dhihaka hii ndio Tanzania Tourism Board wanaibuka na tamko.Aibuuu!!!
Fly Emirates ilitumia fursa ya Kombe la Dunia 2014 na kujibandika "machata" ya kombe la Dunia na kunadika "Fuselage name" za miji yote kombe la dunia lilipokuwa linachezwa nchini Brazil..Kwao ilikuwa fursa na kwa Brazil ilikuwa ni kutangaza miji yao bila ghalama yoyote.Tuitumie fursa ya Wakenya kututangazia Vivutio vyetu bila ghalama kupitia shirika lao la KQ.

image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
 
ok.. waendelee kubeba hao abiria mi ntaendelea kujitahid kuuambia ulimwengu kua..

[HASHTAG]#foundinTanzanianotKenya[/HASHTAG]
 
Attachments

  • 1456844481325.jpg
    1456844481325.jpg
    42.5 KB · Views: 56
Hata waseme Nyerere alikuwa kiongozi wa Kenya saws maana viongozi wa kwetu hawana wanachofiikiri zaidi ya kuhakikisha Zanzibar inakuwa chini ya ccm na Meya wa Dar naye anatoka ccm.
Kwamba wako tayari kusema kwenye kura za Umeya hata Rais na PM nao wapige kura kwa vile wako Dar
 
Wakenya wangekuwa wanatumia maeneo ya Tanzania bila kudai kuwa yako Kenya haingekuwa tatizo, lakini manyang'au yanadai kuwa Mt Kilimanjaro na Olduvai Gorge viko Kenya. That's a big problem! Magu naye ameconcentrate tu na the so called majipu hajui yanayoendelea huko nje!
 
Buchanan cha muhimu ni sisi kutangaza kwa nguvu zaidi yao
 
Wakenya wangekuwa wanatumia maeneo ya Tanzania bila kudai kuwa yako Kenya haingekuwa tatizo, lakini manyang'au yanadai kuwa Mt Kilimanjaro na Olduvai Gorge viko Kenya. That's a big problem! Magu naye ameconcentrate tu na the so called majipu hajui yanayoendelea huko nje!

Lakini usichokijua ni kwamba sehemu kubwa ya mabaki ya Olduvai Gorge na ambayo ndiyo Olduvai yenyewe yako makumbusho London na siyo Arusha au Dar, sasa mbona hilo hamlitolei povu? Mbona TTB hawaandiki kuwataka Wazungu Waingereza warudishe mabaki ya Olduvai?
Ila Mkenya kusema kuongea tu mnaifanya inakuwa ishu?

Ndiyo maana nasema tatizo ni akili ndogo na chuki binafsi dhidi ya Waafrika wenzetu na wala siyo Uzalendo kwa maana kama kweli tungekuwa wazalendo tungetaka mabaki ya Olduvai yarudishwe TZ kutoka London kwa maana ndiyo Olduvai yenyewe!

1280px-Olduvai_stone_chopping_tool.jpg
 
Sisi ni vichaa tuliogeka kwa tunguli zetu wenyewe. Ndugu yangu Barafu umesema ukweli mtupu.Ila Air tanzania haitofufuka milele kwa sababu tumekuwa mapimbi mpaka najichukia.

Nilishasema Air Tanzania haiwezi fufuka kwasababu tumeruhusu mdudu Fastjet kuweka base yake hapa ambapo Duniani hakuna anayefanya hivi kwa uhai wa National Carrier.

Ndio maana wakenya wanatudharau kwa kuwa sisi ni mapimbi narudia mapimbi.
 
Sasa sisi tusilalamike twende tukaandike kwenye bajaji, tren ya mwakyembe na maguta.....hamna namna tena......ndege hatuna
 
Sisi ni vichaa tuliogeka kwa tunguli zetu wenyewe. Ndugu yangu Barafu umesema ukweli mtupu.Ila Air tanzania haitofufuka milele kwa sababu tumekuwa mapimbi mpaka najichukia.

Nilishasema Air Tanzania haiwezi fufuka kwasababu tumeruhusu mdudu Fastjet kuweka base yake hapa ambapo Duniani hakuna anayefanya hivi kwa uhai wa National Carrier.

Ndio maana wakenya wanatudharau kwa kuwa sisi ni mapimbi narudia mapimbi.

:(:(:(:(:(;);););)
 
Kama wewe ni PIMBI shauri yako. Usituchanganye WaTz wote!! Issue hapa ni kujua tatizo (eneo dhaifu) na kulifanyia kazi, Sio kuitana majina yasiokuwa na maana na kuacha tatizo likiwa palepale.
 
Kila kitu kinawezekana katika mageuzi ya kiuchumi kwani hao Fast jet ni bicon haiwezi kutoka? tayari kuna mikakati ya kulifufua Shirika la ndege Tanzania, wewe unaotuita mapimbi utakua umetumwa kutukatisha tamaa.
 
Kama wewe ni PIMBI shauri yako. Usituchanganye WaTz wote!! Issue hapa ni kujua tatizo (eneo dhaifu) na kulifanyia kazi, Sio kuitana majina yasiokuwa na maana na kuacha tatizo likiwa palepale.

Niwie radhi kwa kuku kwaza lakini inatia fedheha sana tumejiharibu akili na saikolojia zetu.Taifa limekosa dira kila,sehemu ni uozo tumeshindwa kujisimamia wenyewe mpaka kila kitu kizuri,kifanywe na wageni. Na sisi sifa yetu kubwa ni siasa za kuharibu na sio kujenga siasa imetawala weledi.
 
Wakenya wangekuwa wanatumia maeneo ya Tanzania bila kudai kuwa yako Kenya haingekuwa tatizo, lakini manyang'au yanadai kuwa Mt Kilimanjaro na Olduvai Gorge viko Kenya. That's a big problem! Magu naye ameconcentrate tu na the so called majipu hajui yanayoendelea huko nje!
Kwa hyo wakisema haupo kwao ndo utafaidika au mtanzania atafaidika?
Wakati tukiendelea na kampeni ya kuutarifu ulimwengu kuwa "Olduvai Gorge" ipo Tanzania na si Kenya kama ambavyo Mwanadada wa Kikenya alivyouambia ulimwengu,katika mitandao ya kijamii kumezidi kusambaa kwa picha za ndege ya KQ aina ya B777 inayoonyesha "Fuselage Name" ya "Mt.Kilimanjaro".Hali hii imezua malalamiko mengi kwa watu mitandaoni na kusababisha watu kuona Kenya wanatumia vivutio vyetu kuitangazia dunia kuwa vinapatikana nchini kwao Kenya.Hii inatokana na malalamiko ya muda mrefu ya Tanzania kuituhumu Kenya kupata watalii kwa mgongo wa vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.

Ukweli ni kuwa hakuna "makosa" yoyote ambayo Kenya kupitia ndege za shirika lake la Taifa(National Carrier) la Kenya Airways linafanya,kwenye ulimwengu wa usafiri wa anga,shirika la ndege la Taifa huwa ni kama "Flying Ambassador".Kuiwakilisha nchi na yote yanayoihusu kule inapokwenda na kutua,zaidi ya yote mashirika haya yamekuwa yanatumia "fuselage name" za vivutio vya utalii kuelezea ulimwengu kuwa ukipanda shirika hili la ndege basi unaweza kufika mahali fulani palipo na kivutio fulani.Kwa upande wa Afrika Mashariki,shirika la ndege la KQ limekuwa likitumia "fuselage name" kama "Mt Kilimajaro","Victoria Falls","Maasai Mara" nk kuulezea ulimwengu kuwa popote unapokuwa duniani ukipanda Kenya Aireays utafika katika vivutia hivyo.

"Fuselage Name" haifanywi na KQ(Kenya Airways) tu,bali hata shirika la ndege la KLM limekuwa likitumia "fuselage Name" ya "Mt Kilimajaro" kwa ndege yake moja aina ya B777 PH-BQP inayofanya safari zake toka Ulaya kwenda nchi za Asia.Hii inawasaidia KLM kupata abairia wengi wanaotoka nchi za Asia na kutaka kuja Mlima Kilimanjaro,kuonekana kwa fuselage name hii itafanya abiria wengi kukata tiketi za KLM wakijua kuwa watafikishwa moja kwa moja kuuona Mlima Kilimajaro,itakumbukwa kuwa shirika la KLM hufanya safari zake kila siku kutoka Amsterdam-Kilimajaro(KIA)-Dsm na baadae kurudi Amsterdam.

Hii haifanywi na KLM na KQ tu,hata shirika la ndege la Ujerumani baada ya kuzindua ndege yake mpya aina ya Airbus 380(A380) imeipa ndege hiyo jina la "Johanesburg" sababu limeanzisha safari za kwenda Afrika ya kusini.Ndege nyingi za Swiss Air zina majina ya vivutio vinavyopatikana nchi nyingine za Ulaya,na hivyo kuwahakikishia abiria kuwa wakipanda Swiss Air wana uhakika wa kufika katika vivutio hivyo vya utalii.

Kuna mambo ya kulalamikia lkn si haya,sisi tunapaswa kuirudisha ATCL yenye nembo ya Twiga wetu anagani.Pembeni ya ndege zetu za ATCL kulikuwa na maandishi yameandikwa "WINGS OF THE KILIMANJARO",lakini pia ndege nyingi za ATCL zilikuwa na "fuselage Name" kama "Serengeti","Manyara","Ngorongoro","Zanzibar" nk.Leo tunao Precisiona Air wanafika Nairobi tu...baadhi ya "Fuselege Name" zake ni "Rombo","Kilimajaro","Iringa","Musoma" na "Mwanza".Tuache kulalamika kwa baadhi ya mambo,tusideke kwa kuombaomba "huruma" ya kuonyesha tunadhulumiwa,dunia ya leo ni "ubabe" na "ukatili" wa kutetea cha kwako na kulinda vyako.Nilipofuatilia mzungumzaji baada ya Miss Odinga kwenye lile Kongamano la IYLA aliposema "Olduvai Gorge" ipo Kenya,mzungumzaji aliyefuatia alikujai kuzungumzia "Maendeleo ya Technolojia na Vijana",kabla ya kuanza mada yake akasema "Ninamshukuru leo Rosemary,nilikuwa najua Olduvai Gorge ipo East Africa,lakini leo nimejua mahususi kumbe ipo Kenya,ndio uzuri wa kukutuianisha vijana toka nchi mabalimbali ulimwenguni".Bado naendelea kufuatilia majina ya vijana wa Kitanzania walioshriki mkutano huo wa IYLA na kwanini hawakujibu hapo hapo,lakini toka August 215 leo baada ya mitandao ya kijamii kama JamiiForums kuibua dhihaka hii ndio Tanzania Tourism Board wanaibuka na tamko.Aibuuu!!!
Fly Emirates ilitumia fursa ya Kombe la Dunia 2014 na kujibandika "machata" ya kombe la Dunia na kunadika "Fuselage name" za miji yote kombe la dunia lilipokuwa linachezwa nchini Brazil..Kwao ilikuwa fursa na kwa Brazil ilikuwa ni kutangaza miji yao bila ghalama yoyote.Tuitumie fursa ya Wakenya kututangazia Vivutio vyetu bila ghalama kupitia shirika lao la KQ.

View attachment 326728 View attachment 326729 View attachment 326730
 
kuna tatizo gani wakati sisi hata ndege hatuna? hiyo moja utaandika vivutio vyoye hivyo? aliyelala usimwamshe. sanasana mshushie na net ili alale vizuri bila bughudha ya mbu na nzi
 
Back
Top Bottom