Kenya kuruhusu mfumo wa kifedha wa Kiislamu

Pepombili

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
439
58
Kenya hao wanaanza kuujuwa uisilamu sasa wabongo nyie kaaeni tu na makanisa yenu hayo ya kinyonyaji na mifumo yenu ya kikatoliki
 
Kenya kuruhusu mfumo wa kifedha wa Kiislamu
Serikali ya Kenya imetangaza kuwa itapitisha sheria ya kuondoa vivingiti vya kodi katika kuchapishwa Hati ya Dhamana ya Kiislamu kabla ya kumalizika mwaka 2011.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Kenya inatazamia kuzindua Hati za Dhamana za Kiislamu maarufu kama Sukuk ifikapo mwishoni mwa mwaka.

Kenya ambayo ina uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki bado haijaweza kupenya katika soko la kimataifa la hati za dhamana za kawaida na kwa hivyo inajaribu kutumia hati za dhamana za Kiislamu kupata fedha kutoka wawekezaji wanaozingatia sheria za Kiislamu, amesema Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Profesa Njuguna Ndung'u kupitia barua pepe.

"Tumepokea maombi ya mradi ambao tutautaja na unaweza kugharamiwa kupitia fedha zitakazopatikana kwa kuchapisha hati za sukuk", amesema Ndung'u.

Benki Kuu ya Kenya iliwahi kupata fedha za miradi ya miundo mbinu kupitia fedha za sukuk mwaka 2009. Hata hivyo ukosefu wa sheria za kodi ni kizingiti kikubwa katika ustawi wa soko la sukuk nchini Kenya.

Bara la Afrika limekuwa eneo la ustawi mkubwa wa mfumo wa kifedha wa Kiislamu huku nchi kama vile Senegal na Afrika Kusini zikijitahidi kuanzisha mfumo wa benki za Kiislamu na hati za dhamana za Kiislamu, sukuk.

Kenya sasa inataka kuwa kituo kikuu cha mfumo wa kifedha wa Kiislamu barani Afrika na inapanga kutoa huduma zaidi za kifedha za Kiislamu.

Weledi wanasema huku eneo la kaskazini mwa Afrika lilikumbwa na misukosuko ya kisiasa, Kenya inatazamia kutumia fursa hiyo kuwavutia wawekezaji kutoka nchi zenye utajiri wa mafuta za Ghuba ya Uajemi.

Kenya ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika Mashariki na Kati kuanzisha benki za Kiislamu mwaka 2007.
 
Kenya hao wanaanza kuujuwa uisilamu sasa wabongo nyie kaaeni tu na makanisa yenu hayo ya kinyonyaji na mifumo yenu ya kikatoliki

本书为斯瓦西里语版, 共分为二十课, 旨在培养学习者汉语听说读写基本技能和一定的汉语
交际能力, 也可用于针对某一特定言语交际技能的汉语教学。
 
Kenya hao wanaanza kuujuwa uisilamu sasa wabongo nyie kaaeni tu na makanisa yenu hayo ya kinyonyaji na mifumo yenu ya kikatoliki

Mkuu.
Umeanza mada yako kwa kutangaza vita.Tutafika kweli.
Haikuwa lazima kwa mada ya kiuchumi kutaka malumbano ya kidini.
 
Kenya hao wanaanza kuujuwa uisilamu sasa wabongo nyie kaaeni tu na makanisa yenu hayo ya kinyonyaji na mifumo yenu ya kikatoliki

waigeni waarabu tu,hamjui kuwa waarabu wana mafuta hawahitaji riba kumake profit,..we mndengereko wa mwananyamala anzisha benki yako isiyotoza riba kama haijafa
 
A step in the right direction. Our society should be sensitized to follow suit as one of the ways of avoiding surging interest rates which scare off potential lenders in conventional commercial banks. This is not about religion, it is about economy and welbeing of the citizenry.
 
Kenya hao wanaanza kuujuwa uisilamu sasa wabongo nyie kaaeni tu na makanisa yenu hayo ya kinyonyaji na mifumo yenu ya kikatoliki
JF sio kijiwe cha mihadhara kidini kama manzese. kama huna hoja kukaa kimya nako ni njia nzuri ya kuwasilisha ujumbe wako!
 
Kenya wako kimaslahi zaidi, kufanya hivyo haina maana kwamba ndio wanakubali sana imani yenyewe. Kama umesoma vizuri habari hiyo, lengo kuu la wakenya ni kuvutia wawekezaji toka nchi zenye utajiri wa mafuta, na sio waeneza uislam kutoka nchi hizo. Iko kiuchumi zaidi.
 
This book is a Kiswahili version, is divided into twenty lessons, speaking and writing of Chinese learners to develop basic skills and some Chinese
Interpersonal skills, can also be used for a particular Chinese teaching verbal communication skills.(hicho ndicho ulichoandika kwa kichina)
 
waigeni waarabu tu,hamjui kuwa waarabu wana mafuta hawahitaji riba kumake profit,..we mndengereko wa mwananyamala anzisha benki yako isiyotoza riba kama haijafa

Maandamo jina lako zuri mkuu unaonekana tena mpambanaji.
Hivi Malaysia, indonesia. mfano mdogo nimetaja hizo mbili uchumi wao mzuri kuna bank nyingi tu za kiislam sio waraabu na sio wachimbaji wa mafuta kama unavyosema wewe. uwezi kuamini mpaka VATICAN CITY wamechukuwa idea hii ya mfumo wa fedha wa kiislam, ukipata muda mkuu pitia.
Islamic banking-
Wikipedia,the free
encyclopedia
 
Kenya hao wanaanza kuujuwa uisilamu sasa wabongo nyie kaaeni tu na makanisa yenu hayo ya kinyonyaji na mifumo yenu ya kikatoliki

hatuhitaji kuiga wakenya ambao ni wabinafsi mno. gap kati ya tajiri na maskini ni kubwa kupindukia kuliko hali ambayo tunailalamikia hapa TZ. waliowengi kenya ni hoi kweli kweli-inatisha na viongozi na wafanya biashara wachache wamebeba uchumi na miradi yote -hata ARDHI yote ya kenya ni mali ya viongozi na wafanya biashara.
 
Kenya hao wanaanza kuujuwa uisilamu sasa wabongo nyie kaaeni tu na makanisa yenu hayo ya kinyonyaji na mifumo yenu ya kikatoliki

Chanzo cha habari yako ni kipi mkuu? Hata hivyo mbona hapa tz walishaanza kutumia huo mfumo toka siku nyingi? au Kenya Wanadesa kwetu?
 
We si ubaki na madras zenu mnabali kulalama tu na kushindwa kudeal na mambo ya maana na mnabaki na umwinyi tu!
 
本书为斯瓦西里语版, 共分为二十课, 旨在培养学习者汉语听说读写基本技能和一定的汉语
交际能力, 也可用于针对某一特定言语交际技能的汉语教学。
Hebu tutilie irabu kwa maandishi ya "Kikristo"
 
Back
Top Bottom