VUVUZELA
JF-Expert Member
- Jun 19, 2010
- 3,103
- 785
Mkuu Vuvuzela
Sina mashaka kuwa unaelewa CHINA anamkopesha US au US anadaiwa mapesa mengi na CHINA. US ana deni kubwa la China. Lakini US hapendelei kuiona Afrika inafanya ukaribu au urafiki na China.
Hapa sio hili la mkopo wa mradi huu tu. Ukweli utabaki China ametoa misaada na mikopo kwa nchi za Afrika bila ya masharti kama ya IMF na World Bank, wala China huwa haingilii mambo ya ndani ya nchi husika. Ni wazi kuwa China wana-wanachokitaka kutoka kwetu lakini ni business oriented na sio kui-control nchi husika kama wafanyavyo hawa "wazungu" wetu.
Si umesoma kuwa UK wanasema tusiwabuguzi mashoga au atatunyima misaada. Masharti juu ya masharti.
Ni wazi sisi tumewafata wachina na kuwambia tunataka mkopo, sio kuwa mchina kaja kutulazimisha tuchukue mkopo. Kama "viongozi" wetu wameamua kututia mkenge basi lawama haziendi kwa China. Lawama tuwabebeshe "viongozi" wetu.
Out of the debt of 14 trillion USD, China anaidai US only 1.5 trillion. Sasa iweje wenye kuidai US sehemu kubwa ya deni wasipige kelele sana kuliko China?
Russia alipoivamia Georgia baada ya South Osertia kuvamiwa hatukuona hizo theory zisizo na kichwa wala miguu na watu mlikaa kimya hapa. Nahisi watu mna gundu na US kuwa kila anachokifanya basi mtaanza kuja na theories zenu za ajabu ajabu.
Al shababu ni mzigo na matatizo kwa Africa na dunia. Big up Kenya na Kibaki, mkiweza twanga risasi yeyote atakaekaa mbele yenu huko Somalia awe raia ama hao majangili wa kisomali na Kenya wakiweza waitwae Somalia yootee iwe part of Republic of Kenya on a permanent basis