Kelele za Gesti Zawachanganya Wanafunzi,

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Kigogo ya jijini Dar es Salaam, wameadhimia kuandamana hadi Ikulu kumuona Rais Jakaya Kikwete kwa kupinga uwepo wa nyumba ya kulala wageni iliyokuwa ndani ya eneo la shule hiyo
Wanafunzi hao ambao mwishoni mwa juma walionekana kufanya fujo shuleni hapo kupinga uwepo wa nyumba hiyo bubu iliyopo katika maeneo ya shule hiyo iondolewe kwa kudai inawachanganya katika masomo yao ya kila siku.

Nyumba hiyo ya kulala wageni ipo pembezoni mwa madarasa ya shule hiyo ya kata ambapo wanafunzi hao wamedai kuchanganywa kutokana na miziki na pilikapilika za watu za kila siku zinazofanywa katika nyumba hiyo jambo ambalo linaenda kinyume na na sheria za haki elimu na kudai kuwapotezea usikivu wawapo darasani ikiwemo na kuwafunza maadili mabovu wawapo shuleni

Hata hivyo wanafunzi hao walishafika ngazi za chini kuripoti tukio hilo lakini imeonekana taratibu za kisheria zinakwenda taratibu na kuonekana watendaji kushindwa kuifungia nyumba hiyo.

Hivyo wanafunzi hao wameadhimia kufanya maandamano ya amani kwenda kwa Rais Kikwete kumweleza kero hiyo ili aweze kuwasaidia.

Wakilalama wanafunzi wamedai “makelele ya wateja wa gesti yanatusumbua wakati wa masomo, mana ni vurugu badala tumsikilize mwalimu wakati mwingine wateja wanagombana vyumbani na kutupigia makelele, mara nyingine mavazi yanayovaliwa na baadhi ya wateja si stahili yanatuletea maadili mabovu.

Kwa kuwa madirisha ya gesti yanatizamana na madirisha ya shule mara nyingine ni rahisi kuona yanayotendeka ndani ya vyumba kwa kuwa madirisha hayana pazia, walilalama wanafunzi hao kwa jazba

Vilevile walilalamikia tabia ya kuona wasichana wenye umri mdogo wakiwa wanaingia na watu wenye rika kubwa mithili ya baba zao ni hali ambayo wanadai kuwaumiza kisaikolojia.

Hata hivyo wanafunzi hao wameadhimia kufika kwenye kituo wanachoshughulikia haki za watoto ili kupata msaada zaidi wa suala hilo

Nyumba hiyo ya kulala wageni ’Gesti bubu’ iliyopo ndani ya eneo la shule hiyo imedaiwa na mmoja wa wahusika kuwa hulipiwa kodi kihalali na imesajiliwa kwa mujibu wa sheria zote za Serikali ya Tanzania kwa jina la The Queen Guest House.
 
Mi kuna vitu vingine vinanishangaza jinsi ambavyo serikali ye2 inafikiri,waende 2 2one,halafu watu wanadhubutu kujiuliza kwa nn wanafunzi wanafeli,
 
Lazima kutakuwa na kosja la kiutendaji hapo. Je kati ya shule na hiyo huduma ya gest hapo nani alitangulia kuwa hapo? Baada ya hapo ndo tujadili zaidi
 
Simuungi mkono: baba enock, mamzalendo wala Eng mayeye, wanafunzi wanapaswa kusoma bila visingizio.
 
hata hili jambo nalo linahitaji kupelekwa Ikulu?!!...........
 
Simuungi mkono: baba enock, mamzalendo wala Eng mayeye, wanafunzi wanapaswa kusoma bila visingizio.

Unajua unalolisema mkuu? Watosomaje wakati wanashambuliwa kutoka kila kona na mambo ya mahaba?

Hili ni tatizo kubwa sana kwani mfumo wa mwili wa kimahaba na ule wa ku-concentrati haichangamani!
 
Jamani hivi hao watoa leseni hawakaguagi sehemu biashara zilipo? Kwanini watoe lesene ya guest eneo la shule?au kwanini walojenga shule hawakujali mazingira?
 
madogo hawa bana..sasa vilio vya mihemuko gesti si ndo vingekuwa vinawapa stimu za kukokotoa magazijuto na kusolve simultaneous equations??? hawa vipi hawa
 
hata hili jambo nalo linahitaji kupelekwa Ikulu?!!...........
Hili swala lilitakiwa kumalizwa haraka na ofisi ya mtendaji kwa kushirikia na uongozi wa shule na sio kwenda IKULU. Ukiona hawamfanyi kitu mwenye hiyo gesti ujue tayari mlungula umepenyeshwa kwa uongozi wa shule
 
Watume wawakilishi kwa DEO akishindwa waende kwa DC, akishindwa waende kwa RC, akishindwa waende kwa Waziri Mkuu, akishindwa wana haki ya kupambana na FFU kuelekea Ikulu.
 
Hatujawahi kuwa serious na issues TZ,ikiwemo elimu.Hata kama gesti likuwepo,uanzishwaji wa shule ungezingatia mazingira yaliyopo kwa kuihamisha/kuifunga au kufungua shule kwingineko..
 
Je kati ya shule na Guest ni ipi ilitangulia kujengwa?..huenda guest ilikuwepo hapo muda mrefu hivyo shule ikajengwa baadae. kama mwenye kumiliki hiyo guest bubu aliijenga shule ikiwa tayari imejengwa basi sheria iangalie kama kanuni za ujenzi wa nyumba za starehe na bar kwenye makazi ya watu zilizingatiwa.
 
Yaani mwnyekiti serikali za mtaa,mtendaji wa kata,tarafa,mkuu wa wilaya ,mkurugenzi mkuu wa mkoa,waziri wote wameshindwa kuwatatulia watoto shida yao mpaka habari iende kwa Raisi hii nchi basi ni upupu mtupu,watoto lazima wapewe mazingira mazuri ya kusoma
 
hii gesti ipo kitaani kwetu kabisa hii.wakiitia ni pigo kubwa kwetu lakini ina haki ya kutolewa
 
madogo hawa bana..sasa vilio vya mihemuko gesti si ndo vingekuwa vinawapa stimu za kukokotoa magazijuto na kusolve simultaneous equations??? hawa vipi hawa

Kweli kigogo umedata. Ngono na taaluma wapi na wapi? unachanganya mchele na kokoto kupika pilau? unashangaza jinga kubwaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom