Kelele za dar live mbagala

Pepombili

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
439
58
Toka kumenzishwa huu ukumbi pale mbagala zakhiem kumekuwa na kelele nyingi sana za muziki ambazo hutusumbua sana sisi wakaazi wa mbagala usiku wakati wa kulala kwa kweli naomba serikali ya mtaa ijitahidi kudhibiti hizi kelele au la sivyo ule ukumbi uondkoshwe au waweke sound proof kuzuia kelele.
 
Hapa labda muandamane maana na hii rushwa ilivyokithiri.
 
Mbona hulalamikii guest houses ambazo zipo kibao karibu na maeneo yako
 
na wakati kuna mtu hapo kafanya tathmini na kuibuka na ripoti ndeefu inayoonesha kuwa hakutakuwa na madhara yoyote kwa wakazi wa maeneo ya jirani....

hii ipo tanzania tu.
 
Mbona hulalamikii guest houses ambazo zipo kibao karibu na maeneo yako

Yeye analalamikia kelele za huo ukumbi sasa kama gesti za huko kwenu zina kelele toa dukuduku lako na wewe
 
Mwenye hii post pamoja na kuiweka hapa ni vyema ukamfuata mwenyekiti wa serikali za mtaa na kumweleza ana kwa ana maana sidhani kama ni mpitaji wa humu, pia iweje ukumbi wa kifahari na wa kisasa kama huu iweje washindwe kuweka soundproof?
 
yeye ana lalamikia kelele ! Guest house watu hulala, hivyo hawapigi kelele. Acha kujitoa fahamu !

umejuaje kuwa hawapigi kelele kiongozi?
Isitoshe dar live haipo karibu na makazi ya watu. We mwandishi tuambie vizuri unakaa wapi?. Au we teja unalala standi ya hapo zakhem
 
ni kweli kiongozi dar live makelele kibao mtu huwezi kulala sasa sijui hawa watu walioanzisha wazo la kuweka ukumbi pale hawakufikiria ama hawajui maana ya sound polution.
 
Yeye ana lalamikia kelele ! Guest House watu hulala, hivyo hawapigi kelele. Acha kujitoa fahamu !

naona wewe hujui makelele ya guest ni zaidi ya club..bora hata ya club unaweza ukaamka ukacheza kuliko ya guest maana yanakufanya akili iruke na ipoteze concentration ya usingizi.
 
Dar Live ina mkono mrefu wa Riz 1. Haiwezi kufungwa hata watu wakifa kwa kelele labda M4C wachukue nchi.
TAFAKARI, CHUKUA HATUA
 
Labda kwa vile hamkuzowea, wenzenu wa kinondoni ni balaa, kuanzia matangazo ya barabarani hadi hayo maukumbi
 
Toka kumenzishwa huu ukumbi pale mbagala zakhiem kumekuwa na kelele nyingi sana za muziki ambazo hutusumbua sana sisi wakaazi wa mbagala usiku wakati wa kulala kwa kweli naomba serikali ya mtaa ijitahidi kudhibiti hizi kelele au la sivyo ule ukumbi uondkoshwe au waweke sound proof kuzuia kelele.

kabla hamjalalama, kwanza mjiulize watu wa mbagala mnachangia sh ngapi ktk pato la taifa. Hamjui kuwa pato kubwa linatokana na uuzaji wa pombe?!, mnataka ukumbi ufungwe ili serikali ikose mapato?!. Poleni.
 
huwa nikipozi pale kwetu mtoni mtongani nasikiaga mizik zaidi ya 5 kila siku usiku tokea huko huko mbagala.
 
Jamani wana jamvi wenzangun naomba tushrikiane. Kwa hili ule ukumbi sawa na ngoma za zamani fujo tuokoe jamii yetu inaharibikiwa
Labda kwa vile hamkuzowea, wenzenu wa kinondoni ni balaa, kuanzia matangazo ya barabarani hadi hayo maukumbi
 
Back
Top Bottom