Keki ya mayai, vanilla na maziwa

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Mahitaji
Kikombe 1½ cha unga wa ngano (kama gramu 200)
½ kikombe cha siagi (margarine, kama gramu 133)
Mayai 2
Vijiko 2 vikubwa vya vanilla
Kikombe 1 cha sukari nyeupe (Ni kama gramu 200. Mie nimetumia mchanganyiko wa sukari nyeupe na brown)
Vijiko 1¾ vya hamira
½ kikombe cha maziwa (maziwa ya maji)

Maelekezo

Hii ni keki rahisi sana kuandaa lakini ni tamu kupita maelezo. Mapishi haya ya keki ni rahisi sana kupika na hayahitaji ufundi mkubwa sana. Unachotakiwa kufanya ni kuandaa vitu vizuri na kuacha mambo mengine yaendelee. Unaweza kuandaa keki hii kwa oven, jiko la mkaa au kwa rice cooker. Jaribu kuandaa na uonje utamu wake.

Washa oven na weka kwenye nyuzi 350°F (180°C)
Paka chombo utakachotumia kuoka keki siagi (au mafuta) kwenye pande zote. (Mie huwa natumia foil paper, lakini ni vizuri utumie mafuta ili upate umbo zuri la keki yako)

Kwenye bakuli ya wastani, weka siagi na weka sukari. Changanya pamoja. Hakikisha vimekuwa laini na vimechanganyika vizuri. (Unaweza kutumia mashine ya umeme ya kuchanganyia, lakini hata kwa mkono inawezekana. Mie nimetumia whisk ya mkono tu kuchanganyia)

Gonga mayai, changanya kwenye mchanganyiko wako. Koroga hadi yachanganyike vizuri. Weka vanilla, koroga zaidi.

Kwenye bakuli tofauti, changanya unga na hamira. Koroga vizuri ili zipate kuchanganyika kwa ufasaha.

Changanya mchanganyiko wa unga na hamira kwenye mchanganyiko wa mayai pamoja na sukari. Koroga vizuri ili vipate kuchanganyika sawia.

Weka maziwa kwenye mchanganyiko na koroga vizuri hadi iwe laini na ichanganyike vizuri.

Mwaga mchanganyiko kwenye bakuli la kuokea. Kisha weka kwenye oven. Tega muda wa dakika 40 na usubirie.

Baada ya dakika 40, toa keki, weka pembeni ipoe na kisha kata vipande ujirambe.
 
Back
Top Bottom