Keki ya kuku ndani

Kasuku Mdogo

Member
Jun 2, 2016
14
23
Mahitaji
Unga wa ngano 250g
Butter 250g
Mayai 9
Baking powder kijiko cha chai 1
Kuku wa kusaga 2 cups
Chumvi kijiko cha chai 1
Sukari 1/3 cup
Kungu manga 1/2 kijiko cha chai (sio lazima)
Mdalasini kijiko cha chai 1
Curry powder kijiko cha chai 1
Kitunguu swaumu kijiko cha chai 1
Tangawizi kijiko cha chai 1
Chicken stock kijiko 1/2 cha chai
Pilipili mtama 1/2 kijiko cha chai
Mdimu/limau moja
Pilipili hoho 1/2 kila rangi

Jinsi ya kupika
Muoshe kuku wako vizuri as iwe na ngozi muweke viungo vyote mbandike jikoni isipokuwa usiweke pilipili hoho.

Mwache achemke na hayo maji yakikauka muweke pembeni apoe.

Kama utakuwa haujapata kuku wa kusaga umechemsha kuku mzima basi akipoa mnyambue nyambue au asage katika blender, muweke pembeni.

Saga siagi na sukari pamoja na mayai 3, yakichanganyika weka unga na baking powder.

Ikichanganyika vizuri weka katika chombo cha kuchomea, chukua kuku wako changanya na mayai 3 mimina juu ya ule unga wako wa keki uliopo katika chombo cha kuchomea, halafu piga yale mayai matatu yaliyobakia ya changanye na pilipili hoho mimina juu.

Weka katika oven moto 350.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom