WAKUU,
Huyu jamaa alifanya kazi nzuri sana kuweka jiji safi na pia kuongeza mapato ya jiji. Jambo moja{ miongoni mwa mengi ] la kukumbukwa aliloacha ni pamoja na ujenzi wa High School ya Benjamin Mkapa. Swali ni je, kwa nini Muungwana kamuacha?
Mkuu ni kweli kwamba Keenja alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya Jiji na siyo Mkurugenzi, alijitahidi kufanya hayo uliyosema, lakini ni vizuri ikaeleweka kuwa licha ya opportunity alizokuwa nazo lakini alishindwa kufanya makubwa zaidi kitu ambacho naamini kabisa kuwa ndo weakness point iliyomfanya muungwana amteme.
Kwa mfano Huyu jamaa alipokuwa Jiji alishindwa Kuheshimu utawala wa Sheria ambapo alikuwa akijichukulia sheria mkononii.e kufukuza wafanyakazi bila kufuata utaratibu.
Pia alikuwa hafuati taratibu za manunuzi. Mathalani hata hayo majengo ya BM High School pamoja na majengo yote yaliyojengwa wakati wake, aliyajenga kwa kutumia Mafundi wa Mtaani bila ya kutangaza Zabuni maarufu kama Force Account. Matokeo yake ni kwamba majengo hayo hayawezi kuongezwa hata floor moja zaidi kwa sababu ya kutokuwa na kiwango kinachotakiwa.
Lakini huyu jamaa licha ya kutokuwa na Madiwani ambao mara nyingi huwa ni kikwazo katika maamuzi mengi, alishindwa kusimamia vizuri mapato ya jiji. Unaambiwa kipindi cha huyu jamaa, kiwango cha wizi kiliongezeka maradufu kwa vijana wake wa Accounts. Hii ni kwa sababu ya tabia yake ya kuchota hela bila ya kufuata kanuni, ambapo vijana hao nao walikuwa wakiongeza tarakimu kwenye transanction za jamaa.
Kama hiyo haitoshi, ukifuatilia kwa makini, katika kipindi cha Keenja, licha ya mapato makubwa yaliyotokana na Service Levy, maendeleo yanayodaiwa mengi yalikuwa ni katika manunuzi ambapo alitumia mwanya huo kujinufaisha kwa kufanya "RoyalBlue"]UMAHALU[/COLOR]. Mathalani ununuzi wa Ubungo Bus Terminal, Majengo ya Kilitex, na mengine mengi.
Na hata alipoteuliwa kwenye Baraza la Mkapa, ni kati ya Mawaziri waliochangia kumharibia BM kwani alishindwa kuperform hasa katika Wizara ya Kilimo. Japokuwa anajitetea kuwa alishindwa kwa sababu hakutegemea kupewa Wizara hiyo bali TAMISEMI, lakini ukweli unabaki palepale kuwa huyu jamaa yuko after Money zaidi kuliko maslahi ya Taifa na ndiyo sababu wananchi wa jimbo lake hivi sasa hawataki hata kumsikia.
Mkuu labda useme mwingine na siyo Keenja.