Kazi ya Uspika ni ya ushawishi zaidi na wala siyo kutumia rungu.........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Nimepima kauli za Spika mpya Mheshimiwa Anne Makinda na kugundua silaha anayoitegemea kuzima mijadala bungeni ni kifungu cha 90 (13) ambacho kinasema kauli ya spika ni ya mwisho anapoamua kufunga mijadala bungeni...................Kifungu hicho hicho ndicho kilitumiwa na Spika mstaafu Samweli Sitta kuzuia mjadala wenye masilahi makubwa kitaifa wa Richmond........................

Swali la Tundu Lissu lilipaswa lijibiwe kabla ya kura ya kumthibitisha PM lakini Spika akaamua kulihairisha hadi baada ya uchaguzi na akalijibu visivyo huku akilikumbusha Bunge mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 90(13)............huo siyo uongozi wa pamoja ambao Spika aliuahidi hata kidogo.........Ni ubabe tu........

La msingi swali la Lissu lilihusu kanuni za uendeshaji wa Bunge kulingana na kifungu cha 53 (a)-(c) ambavyo kwa pamoja vimebainisha ya kuwa mijadala inayoanzishwa na serikali lazima itoe nafasi kwa kiongozi wa upinzani kutoa kauli yake...........

Hili halikufuatwa kwenye uteuzi wa kura ya kulithibitisha jina la PM......na Mheshimiwa Tundu Lissu aliomba ufafanuzi ambao Mheshimiwa Spika alighaili kuutoa bali aliahidi kuutoa baada ya kura kupigwa na matokeo kusomwa na PM kupewa muda wa kushukuru ndipo Spika alirudia kuishughulikia hoja ya Mheshimiwa Tundu Lissu......................

Tatizo hapa ni kuwa Spika hakutoa umuhimu kwa hoja ya Mhe. Lissu kujibiwa kabla ya kura tajwa.........kwani kama utaratibu ungebainika umekosewa yaamanisha ya kuwa zoezi zima la kura lingerudiwa ukiachilia mbali majibu ya Spika aliyoyatoa baadaye kukosa mashiko katika kubeza hoja tajwa...........haya ni matumizi mabaya ya wakati...


Spika alijitetea ya kuwa serikali haipo kwa kuwa baraza la mawaziri halijaundwa.......What a nonsense......lakini hoja ya uteuzi wa PM ilitoka serikalini sasa ilikuwaje aikubali kuipokea na kuifanyia kazi kama Raisi na Mwanasheria Mkuu bado siyo serikali?........................tukumbuke ya kuwa hata baada ya bunge kuvunjwa serikali hiyo hiyo ilituambia bado yenyewe ipo kazini sasa sijui ni lini Mheshimiwa Spika aliivunja hiyo serikali...............

Ukiachia mbali hilo, Mheshimiwa Spika alitafuta kuegemea kwenye kanuni nyingine ambayo inagongana na kanuni ya 53(c)....kiutaratibu huwezi ukaikuza kanuni moja kwa kuziathiri haki ambazo tayari zimekwisha kutolewa na kanuni nyingine isipokuwa kama kuna kanuni inayoelekeza hivyo.........yaani haki zilizotolewa na kanuni moja huwezi ukazififilisha kwa kutumia kanuni nyingine...........................pengine kwa Mheshimiwa Spika kwa vile ni mbumbumbu wa sheria ndiyo maana ameshindwa kuona ukweli huu..................na ndiyo maana maombi ya Mheshimiwa Anne Kilango Malecela ya kuua mjadala wa kulithibitisha jina la PM aliupa uzito kinyume na sheria za kuliongoza bunge hilo.......hususani ukizingatia ya kuwa ni maombi ya mbunge wa CCM dhidi ya haki za Kiongozi wa upinzani kutoa maoni yao......CCM hawana sababu ya kuwapunguzia wapinzani hakl zao za kimsingi za kutoa maoni ambazo wamepewa na kanuni......


Mwishowe Spika alipoona hoja zake binafsi za utetezi hazina mashiko akakimbilia kuficha makosa yake kwenye kifungu cha 90(13) kuwa kwa vile alikwisha kufunga mjadala tajwa basi uamuzi wake ni wa mwisho........................

Hilo lilikuwa ni kosa..............udikteta kamwe hautafanikisha malengo ya Spika mpya kuleta maelewano bungeni....................But what do we expect from a political party that came to power through a backdoor? We should expect more of the same...................dhuluma on top of dhuluma to continue besieging this otherwise great nation.......
 
Back
Top Bottom