Kazi kwenu taifa stars; tumechoka na sababu za kila siku

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,955
22,128
Na Erasto Stanslaus

KOCHA Mkuu wa mabingwa wa Bara la Oceanic New Zealand, Ricki Herbert amesema atashusa kikosi kamili katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania, 'Taifa Stars' utakaochezwa leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

New Zealand watacheza mchezo huo wakiwa njiani kwenda nchini Afrika Kusini, kushiriki michuano ya Kombe la Mabara lililopangwa kufanyika mapema mwezi huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Herbert alisema mchezo huo kwao utakuwa wa kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.

Alisema mchezo huo, utakuwa mgumu kwao kutokana na kutowajua Tanzania, lakini anaamini utakuwa kipimo tosha kwa kikosi chake ambacho amekiandaa vizuri kukabiliana na Stars.

"Kwa kuwa hii ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, hivyo siijui kabisa kikosi na mtindo na mtindo wanaoutumia Stars, lakini naamini utakuwa mchezo wa ushindani na mzuri kwa pande zote," alisema Hurbert.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo alisema mchezo huo unafaida kubwa kwa kikosi chake kutokana na ubora wa wapinzani wao, pamoja na mtindo wao wanaotumia.

Alisema hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kucheza na timu ya Ulaya, hasa katika Bara la Oceanic, hivyo watakutana na mtindo tofauti kabisa na timu walizokutana nazo.

"Mchezo huu utakuwa mzuri na faida kubwa kwa Stars, ambapo itapata fursa ya kupata uzoefu zaidi kutokana na kukutana na mabingwa wa Bara, wanaokwenda kucheza Kombe la Mabara ikiwa ni pamoja na kupata mbinu na mtindo wanaotumia nchi za Oceanic," alisema Maximo.

Alisema katika mchezo huo, atawakosa nyota wake wawili, Nurdin Bakari pamoja na Jabir Azizi ambnao wote ni majeruhi lakini nafasi zao zitachukuliwa na kiungo Shaban Nditi.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa moja usiku na utachezeshwa na mwamuzi Oden Mbaga wa Dar es Salaam, akisaidiwa na Haji Makame na Ali Kombo wa Zanzibar, wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Israel Nkongo
 
Mpira ndio umeisha hivi punde. Taifa Stars wameshinda 2-1. Magoli yamefungwa na Tegete na Kazimoto. NZ walianza kupata bao kabla ya Tegete kusawazisha halafu Kazimoto kupata la ushindi dakika za mwisho. Hongera Tanzania.
 
Wadau huko nyumbani tupeni ripoti....stars vs NZL nani mkali?
hiki kimya ndio kusema tushatandikwa au...!
 
Tumeshinda 2-1, wamefunga mapema kipindi cha kwanza kwa penalti hivyo hadi mapumuziko 1-0, Mambo yamebailika kipindi cha pili. Jery Tegete kafunga moja baadaye Mwinyi Kazimoto kafunga dakika za majeruhi kwa shuti kali. Mpo.
 
Kwa tulioiona hii mechi wamecheza vizuri, hasa kipindi cha pili. Wanastahili pongezi, wanaonyesha ukomavu fulani hivi. Ila tathimini nzuri tutaipata baada ya New Zealand kucheza mechi nyingine za majaribio, na hata baada ya michezo hiyo ya mabara. Tutakapoona uwezo wao halisi, na kama watakuwa washindani basi bila ya shaka kiwango chetu kinazidi kukua.
 
But hawa wazungu sidhani kama wapo kwenye ulimwengu wa soka
Wapo kwenye ulimwengu wa soka kivipi!, hawa ni bingwa wa bara lao. Wakati sisi si bingwa hata wa kanda yetu, ila tathmini nzuri tutaipata watakapofanya majaribio mengine. Hasa watakapocheza na Italy, itatupa kujua kama ni washindani ki kweli au ni wenzetu. Kati yao kuna wanaocheza kwenye ligi kubwa tu, hivyo wako juu yetu. Tunastahili kujipongeza kwa hatua tuliyofikia, tukaze buti tu.
 
Jerry tegete alifunga kwa mkono mbona hatulijadili hili jamani...wengi wanakimbilia kuotea ..tuliokuwepo uwanjani...wizi mtupu goli lile...mabeki walijitahidi sana kumuonyesha mwamuzi amefunga kwa mkono wapiiiiiii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom