Kazi kwako Kikwete!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
..unamtaka Ballali arudishwe au hutaki arudishwe ili madhambi ya ufisadi yasijulikane!?
Posted Date::1/28/2008
Marekani yasema serikali ikimtaka Dk Ballali atarajeshwa Tanzania
*Yasema pia itasaidia kurejesha fedha zilizoibwa BoT

Na Dennis Msacky
Mwananchi
BALOZI wa Marekani nchini, Mark Green amesema kwamba serikali ya nchi yake inaweza kumrejesha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daud Ballali endapo serikali ya Tanzania itaomba arejeshwe.

Akizungumza na wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam, Balozi huyo alisema suala la kumrejesha Ballali nchini kwa ajili ya kujibu tuhuma za ufisadi wa mabilioni ya fedha uliofanyika BoT uko mikononi mwa Serikali ya Tanzania.

"Kwanza kabisa hatuna uhakika kwamba Ballali yuko Marekani, lakini hata hivyo ni wajibu wa serikali kutuambia kama wanataka kumrejesha na sisi tutawasaidia kufanya hivyo," alisema Balozi huyo.

Alisema tokea awali nchi yake ilishasema kwamba itashirikiana na Tanzania katika vita yake dhidi ya rushwa, hivyo wako tayari kumrejesha Ballali kama yuko Marekani kwa matibabu au kwa shughuli zozote.

Viongozi wa serikali, na wa BoT wamenukuliwa mara kwa mara wakisema kwamba Ballali yuko nchini Marekani kwa ajili ya matibabu, lakini wameshindwa kutaja hospitali anayotibiwa jambo ambalo limekuwa likizua maswali mengi kuliko majibu.

Kwa nyakati tofauti, pia ubalozi wa Marekani nchini umenukuliwa ukisema kwamba umekuwa ukisoma katika vyombo vya habari kuhusiana na Ballali kuwako nchini Marekani, lakini hauna uhakika.

Pia kumekuwa na madai kwamba Ballali ni raia wa Marekani, licha ya kufutiwa viza aliyopewa kwa wadhifa wake wa gavana wa BoT.

Akizungumzia hilo, Balozi Green alisema kwamba kama Ballali angekuwa raia wa Marekani basi asingeweza kuomba viza.

"Hakuna raia wa Marekani ambaye anaomba viza na hana haja ya kuomba viza, hivyo Ballali si raia wa Marekani. Viza ya Ballali aliiomba mwaka jana," alisema Balozi huyo.

Kabla ya kurejea Tanzania, Ballali alikuwa akifanya kazi nchini Marekani kwa zaidi ya miaka 20 katika mashirika ya kimataifa. Ballali aliondoka nchini miaka ya 70 kwenda Marekani wakati huo akiwa Mkurugenzi wa Utafiti wa BoT.

Kuhusiana na nchi ya Marekani kusaidia kurejesha fedha zilizoibwa BoT kama zimewekwa katika mabenki ya nchi hiyo, Balozi alisema kwamba nchi yake ipo tayari kufanya msako katika mabenki na kurejesha fedha zote ambazo zitabainika kwamba zilichukuliwa kutoka BoT.

"Marekani itasaidia kutafuta fedha zote ambazo zimeibwa na kuzirejesha nchini, hiyo ni sera yetu kwamba haturuhusu fedha za aina hii kuwako katika nchi yetu," alisema.

Alisema kama serikali ya Tanzania inajua kwamba baadhi ya Sh133 bilioni zilizoibwa BoT zimepelekwa katika mabenki ya nchi basi watoe taarifa ili waweze kuzirejesha nchini.

Akizungumzia ujio wa Rais wa Marekani nchini, Balozi Green alisema kwamba utasaidia sana kuitangaza Tanzania katika ramani ya kimataifa kwa kuwa hata vyombo vya habari vya nje vitakuwa vikifuatilia msafara wake.

Alisema anaamini kwamba ziara ya George Bush itasaidia kukuza utalii wa Tanzania. "Naamini kwamba ujio wa Rais Bush utasaidia kukuza uchumi wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano uliopo," alisema.
 
Kama akiamua kuachana na uraia wa Tanzania watampata?

Kama bado ni raia basi wakimtaka watampata tu, huwezi kuukana uraia baada ya kufanya ufisadi ili uendelee kula kuku zako.
 
..viongozi wa ngazi za juu, President's apointees, husafiri kwa kutumia pasi za KIDIPLOMASIA. pasi hiyo inawapa kinga ya kidiplomasia/diplomatic imunity.

..nadhani walichofanya Wamarekani ni ku-revoke diplomatic immunity kwa Daudi Balali. Kwa msingi huo akipatikana na kosa ndani ya USA basi atashitakiwa kama msafiri mwingine.

..sasa hiyo haina maana ya kwamba Visa yake imesitishwa, or he is subject for deportation.

..sina uhakika...nadhani hicho ndicho kinachoendelea hapa.
 
Tunamuhitaji Balali hapa nyumbani kwao Tanzania .. NOW!!

Anathamni kubwa Kwasabu we will probe him in.. out.. inside out..upside down..Mpaka awaseme wenzake...! walioshirikiana/waliomshirikisha! We will crack him come rain come what....!We need the valuable National secreat he is keeping
 
Back
Top Bottom