:A S 114:kawambwa Must Go
Hii WIZARA YA ELIMU mkitaka kupima ugumu wake basi awekwe LOWASSA ndo mtaelewa matatizo yake.....ni wizara inayomgusa kila mwananchi ni wizara yenye migogoro isiyoisha....Walimu wanamgomo baridi yani wanafundisha kishikaji matatizo yao yanaeleweka ikiwamo ya maslahi duni na wengine ni voda fasta.....Bunge linahusika kwa kufuta baadhi ya mitihani hasa ya darasa la nne na kidato cha pilli...kwa hayo yote KAWAMBWA anahusika vipi baba wa watu? upole wake isiwe tatizo basi apewe ata MAGUFULI chini ya migogoro iliyopo uone kama kuna jipya...upole wa mtu sio tija mbona SHEIN nae ni mpole lakini mlinganishe na unaemjua......
Big up Mkuu, hatimaye hata wabebaji, Chama chake ambacho ndiyo kiko madarakani kimemtangaza rasmi kuwa ni MZIGO KWA TAIFABora wewe umemuona kama mzigo wa Taifa, mimi namwona kama mzigo wa Misumari/mzigo wa Moto pia - Haubebeki na unamuumiza mbebaji. JK amejitahid kumbeba kwa mbeleko za kila aina ili afike naye anakotaka kufika naye ila huyu Mzee anazichana. Sa sijui anataka kushuka kwenye hiyo mbeleko au hajui maana ya kubebwa!! Mi simuelewi huyu mzee, akumbuke yote haya anayofanyiwa na JK ni kwa cost ya walipa kodi wa Tanzania. Mimi nadhan ilipaswa atumie busara yake ya kawaida tu kustep down na kupisha wengine sio hadi asubiri amuumize mbebaji!!!
Natofautiana na wewe mkuu.
Yote uliyoyasema juu ya Kawambwa hayana mshiko.
Matatizo ya Wizara ya Elimuyapo hapo siku nyingi sana hata kabla ya yeye kuteuliwa wizarani pale.
Kwa mantiki ya usomi, vijana wa sekondari hukaa shuleni miaka minne, kupata DIV 4 si matokeo ya mwaka mmoja, ni accumulation of failures.
Ni vema ukatueleza wizara iliyoexcel kwa kipindi hiki katika utendaji, kipindi ambacho serikali nzima ina ukata wa kutisha.
Kweli Kawambwa hana machachari wal kujivuna au kupenda mapambano na malumbano, kwa tunao mfahamu hebu mchokoze.