Wapi nitapata mafundi wazuri wa Kaunda suti

GYNEOCOLOGIST

Senior Member
Sep 13, 2016
171
110
Kiukweli kaunda suti ikishonwa na fundi anayeijulia inatoka poa saaaana na hasa ikivaliwa na mtu mwenye mwili wa wastani, yaani si mnene. Naomba kujuzwa ni wapi walipo mafundi wazuri wa hii kitu, nataka nibadili mwonekano wangu toka tishits na jeans hadi kaunda suti
 
Nilikuwa na fundi wangu moja hivi sema yuko mbali kidogo kwa sasa.
Akirudi nitajitahidi niku PM mawasiliano yake.
 
Yaani watanzania tumelala sana, soko linatangazwa hapa usawa wa Magufuli hakuna anayechangamkia tenda...hata marafiki au ndugu wa mafundi hawawafanyii connection.
 
Wakuu mwenye picha atuwekee tuone zinakuwaje hizo suti!
1481056879171.jpg
 
Jamani kuna wakaka wanajua kuvaa, na walibarikiwa mwili mzuri, kuna siku nilipishana na mkaka mama yaanguuu weeeeee! alikuwa kapiga suti ya maana imekaa mahala pake, koti limesimama mahala pake, kapiga SAA ya maana, kanyoa poa sana, yababaa weee, mrefu mweusi Fulani hivi, manina zakee, alikuwa anatoka dukani tukapishana mlangoni mweee! Nilisema moyoni " sifa na utukufu viwe kwako
Ee Mungu" niligeuka Mara moja tu, nikajihakikishia huu sio udhaifu wangu.sikugeuka kwa Mara nyingine kha!
 
Kiukweli kaunda suti ikishonwa na fundi anayeijulia inatoka poa saaaana na hasa ikivaliwa na mtu mwenye mwili wa wastani, yaani si mnene. Naomba kujuzwa ni wapi walipo mafundi wazuri wa hii kitu, nataka nibadili mwonekano wangu toka tishits na jeans hadi kaunda suti
Yuko mmoja pale kinondoni A, ila nawasiwasi km hajhamia Dom maana kuna mheshimiwa mmoja alitaka ahamie kule.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom