Elections 2010 Kaulimbiu za Kampeni 2010

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
Wakati umewadia kwa wachambuzi wa siasa kuanza kubashiri yatakayojiri - na kutoa mwelekeo wa hali ya kisiasa - wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010. Moja ya masuala ambayo yatakiumiza na pengine yameshaanza kukiumiza chama tawala kichwa ni maandalizi ya kaulimbiu ya kampeni.

Zifuatazo ni kaulimbiu ambazo zinaoneka zimechuja na hazirekebishiki:

1. Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya!
2. Maisha Bora kwa Kila Mtanzania!

Na zifuatazo ni kaulimbiu ambazo zikirekebishwa zinaweza kuuzika:

1. Tanzania bila Umaskini Inawezekana!
2. Kilimo Kwanza na Uhakika wa Chakula!

Kaulimbiu zifuatazo ndizo zinaweza kuamsha ari ya wapiga kura wazalendo:

1. Rudisha Rasilimali kwa Wananchi!
2. Tanzania bila Ufisadi Inawezekana!

Je, chama tawala kitakuwa tayari kujisafisha kwa kaulimbiu za kimapinduzi?
 
kwa chama tawala naona hapo hakuna ambayo inawafaa labda watumie kaulimbiu "tukiwakamata mafisadi nchi itayumba" mungu tubariki sisi ambao wepesi wa kusahau kwa zawadi za kanga na tshirt za kidumu chama chetu
 
basi hamjifunzi pemba ambako ccm haina chake huko kwani wapemba walijua mapema kuwa ccm maana yake ni chama cha mafisadi na leo ndio mnaona mkipewa fulana na ghanga tu mnakipigia wengine wakipewa mbega ndio mchezo umeisha wapemba hata mkiwapa nini wao msimamo haubadiliki wanajitahidi kupeleka askari na vitisho kibao lakini wapi mbona sehemu nyengine hakupelekwi askari ila pemba tu huu ni uonevu lakini ccm ijue haitotawala maisha kwani utawala ni wamungu tu iko siku itabaki historia kuwa kilikuwapo ccm mungu ilani ccm
 
1. Fanya Uamuzi Sahihi Amani Idumu!
2. Pinga Umaskini, Chagua Maendeleo!
 
ila tatizo kubwa kwa watanzania licha ya kudanganywa na kaulimbiu nyingi lakini hatuchukui uamuzi sahii
 
Back
Top Bottom