Bigirita
Platinum Member
- Feb 12, 2007
- 15,986
- 7,366
mkuu, sihitaji kuongeza neno.
LIKE.
LIKE.
Hizi ni kauli za kawaida kwa watawala hasa wanaotawaliwa wanapokuwa ni wajinga na wasiokuwa na uwezo wa kuchukua hatua. Tutaendelea kuzikia kauli za kudhalilishwa hadi tutakapo amka usingizini! Tunadanganywa na kudhalilishwa kwa kuwa tumeshaharibiwa na shule za kata. Ndio maana tunaambiwa eti kuna "utawala bora!" Hakuna nchi iliyoendelea duniani ikiwa inatawaliwa. Wakati tunahitaji "viongozi bora", tuliowapa dhamana wanasema wanatutawala "kwa ubora" na sisi tunafurahia na kuwapongeza. Ndio maana wanatudharau na kutuona wajinga mwisho wanaropoka wanavyotaka maana wanajua hatuna jeuri ya kuwachukulia hatua.
Vyovyote vile, tutatukanwa na kudhalilishwa hadi tutakapotoka usingizini na kuchukua hatua madhubuti ya kuchagua "viongozi" bora na sio "watawala" wanaolewa madaraka na kuishia kututawala kama wakoloni kwa majigambo eti ni "utawala bora!"