Kauli ya Yusuf Makamba mnaionaje?

Freetown

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
883
73
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Yusuf Makamba alisema ushindi wa mwanawe, Bw. January Makamba katika Jimbo la Bumbuli ulikuwa wa lazima na iwapo angeshindwa ilikuwa ni fedheha kwake na kwa chama hicho.
Alisema kijana wake alipokuwa akigombea kuchaguliwa na chama hicho kukiwakilisha katika Uchaguzi Mkuu hakuwa January kama January bali alikuwa mtoto wa Katibu Mkuu wa CCM, hivyo ilikuwa lazima ashinde.

Source-Majira
 
Hivi huyu mzee huwa hana washauri wa kumshauri kabla ya kuongea! haya ni maneno gani ya kusema mbele za waandishi wa habari, si ni wazi anaeleza kuwa January amebebwa pamoja na rushwa zote na rough alizocheza!
 
Hapa ni wasi wasi na katibu mkuu wa Chama. Huu ULAZIMA wa mwanawe kushinda una walakini. Huu ndo ubabe wa baadhi ya viongozi wetu!! Tutake tusitake angeshinda tu! angefanya 'mambo' kama hakuyafanya.
 
anatakiwa astaafu kabla hajaharibu tena..! alishawahi kuharibu zanzibar...! he never learns..! he has to learn it the hard way..!
 
Amakweli kale ka-msemo "Mume wa mama ni baba"; ndivyo inavyoonekana CCM Vs Makamba. Ila hakika ni kipimo duni cha uongozi kama alisema hivyo, meaning chama ni chake na familia kwani angeshindwa ingekuwa aibu kwa familia.
 
Tatizo shule, huyu mzee elimu yake ni ndogo kulingana na nafasi anayoshikilia katika CCM, tofauti kabisa na mtangulizi wake Mangula, huyu ni mropokaji, na nafasi yenyewe hii kapewa kishikaji tu na JK kutokana na mchango wake katika kamati ya uwanga na uchawi mwaka 2005. Hana lolote anachoringia ni uchawi na kujikomba kwa wakubwa.
 
Hiyo kauli kaitoa tu baada ya kura za maoni Je ubunge itakuwaje? Si anatuonyesha namna watakavyofanya katika uchaguzi wa mbunge!
 
Hivi huyu mzee huwa hana washauri wa kumshauri kabla ya kuongea! haya ni maneno gani ya kusema mbele za waandishi wa habari, si ni wazi anaeleza kuwa January amebebwa pamoja na rushwa zote na rough alizocheza!

Mtoto wake mwenyewe si mtaalam wa kuwatayarishia wengine vya kuongea(JK)?
 
Akina Mangula wanalia sasa. Muda ukifika na yeye ataona raha ya UBABE aliosaidia kuujenga.
 
njia pekee ni kusimamisha mgombea makini na mahili wa upinzani ili huyo mtoto wa makamba akose ubunge hilo litakuwa fundisho tosha
 
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Yusuf Makamba alisema ushindi wa mwanawe, Bw. January Makamba katika Jimbo la Bumbuli ulikuwa wa lazima na iwapo angeshindwa ilikuwa ni fedheha kwake na kwa chama hicho.
Alisema kijana wake alipokuwa akigombea kuchaguliwa na chama hicho kukiwakilisha katika Uchaguzi Mkuu hakuwa January kama January bali alikuwa mtoto wa Katibu Mkuu wa CCM, hivyo ilikuwa lazima ashinde.

Source-Majira

Bravo Makamba: That is the NAKED truth!

Ameokoka na anamwogopa Mungu: Ameongea UKWELI mtupu: Au mlitaka aseme uongo?
 
Haaaa Pole Shelukindo lakini JK atakupa Ubunge, Ila Kwa January Mmmmm Mimi namjua ni mtu wa kawaida sana nimefanya naye vikao vingi ni mtu wa kujituma ambaye ninaweza kusema hapo Jimbo limepata mtu.
 
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Yusuf Makamba alisema ushindi wa mwanawe, Bw. January Makamba katika Jimbo la Bumbuli ulikuwa wa lazima na iwapo angeshindwa ilikuwa ni fedheha kwake na kwa chama hicho.
Alisema kijana wake alipokuwa akigombea kuchaguliwa na chama hicho kukiwakilisha katika Uchaguzi Mkuu hakuwa January kama January bali alikuwa mtoto wa Katibu Mkuu wa CCM, hivyo ilikuwa lazima ashinde.

Source-Majira
yale yaleeeeeeeeeeeeeeeeeee! Masikini akipata....hulia mbwata mbwata!!
 
huyu mtu sijui JK alimtoa wapi! Bila shaka Jk atakuwa anaona aibu tu kumwondoa, nahisi baada ya uchaguzi hatamrudisha tena. Real hana sifa za nafasi aliyonayo. alitakiwa awe Mzee wa propaganda kama Tambwe Hiza, kwani hachagui hata lakusema.
 
Back
Top Bottom