Kauli ya Rais imevunja Katiba; kwa kuingilia uhuru wa Mahakama

Sheria ni Taaluma ambayo sii lazima ikubaliane na Logics. Kwako wewe, 1+1=2, ndivyo wengi wajuavyo,lakini kwa wanamahesabu watakwambia 1+1= depends on the Base. Kuna technicalities nyingi sana, tena controversial katika suala zima la Ushahidi. Kwa Laymen n Women hawataweza kutaelewa kwakuwa kwao 1+1=2!
Ujue mkuu haya mambo ya watu washeria kujidai wana complicate mambo ndo hayo ya mkwere kila mtu anamuona hafai, pia mara nyingi mahakimu wanaenda kinyume na sheria kwa kufata tu hekima.
 
Kweli wabongo tuna gubu, katika yote aliyoongea umeona umkosoe tu? msifie basi hata kwa mazuri aliyozungumza. Binafsi sijaona kama amewapangia maamuzi majaji naona kama amewapa mkakati wa kazi tu bado maamuzi yatatolewa na majaji na kwa kufata sheria za nchi.Tatizo wapiga dili wengi walizoea ikulu kama kimbilio lao.

Hata Mungu muumba kakuumba ili utende wema na mazuri jambo ambalo ni wajibu wako!!

Ukitenda baya (au sema makosa), yatatafutwa hayo makosa ili uhukumiwe kwayo.

Kufanya nema kwa matendo na kauli ni wajibu wa Rais au kiongozi yeyote na mara afanyapo kinyume (baya au kosa) kwa kauli au kwa kutenda, atawajibika kwalo!!

Katiba ni superior na iko juu ya Rais. Kwenda kinyume nayo ni defamation!!
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa Uzi huu. Umegonga kunako. Ila pia tegemea mashabiki maandazi kama hao, wanaoishi kama makinda ya ndege siku zote, chochote kisemwacho they do not question it, they swallow it as it is. Siku wakiambiwa leo mnaenda Kibla wataenda tu! Nauona Ushabiki na Ufuasi kama ule alioupata Kibwetere kwa wafuasi wake aliokuja kuwaangamiza baadae.
Asante mkuu, barikiwa sana.
 
Una mawazo mgando kweli wewe. Ungekua wewe ungesema NDIYO UMETUKWAZA, unaamini ungethubutu. Acha uongo wako hapa!

Kwa hiyo unategemea wamfanye nini Raisi wa JMTZ? Sana sana kama kuna kosa lolote alilofanya watataka awaombe msahamaha jambo ambalo tayari alishalifanya jana kwa kusema mwishoni wa Hotuba yake kwamba ,,kama nimewakwaza naomba mnisamehe", sasa kuna nini tena cha kujadili hapo?
 
Hata kama anavunja katiba bora avunje ila ndege zije Tanzania aiseee
 
Ulitaka aongee namna gani????? Kitu gani kipya alikisema pale? Tatizo wengi wetu tumezoea kuishi kinafiki (kusifia watawala) na ndo maana umasikini utatuandamaa milele.

Na alisema jana, kuna watu watasema hapa nimeingilia mahakama.
 
Jambo la msingi kabisa ilikua ni kujizuia kutumia matamshi ya aina ile, lile lilikua ni kosa la kiufundi, nadhani kuna ulazima chama cha wanasheria wa Tanganyika kulijadili hili na kulitolea tamko, ni makosa likiachwa liendelee.

Wala halikuwa kosa la kiufundi mtu mwenye kesi yake ruksa kuilalamikia mahakama.Kesi za serikali mwenye kesi zake ni Raisi na pale alikutana na wenyewe walioshika hizo kesi akaitumia hiyo nafasi kutoa malalamiko yake! Hata mimi ningekutana na majaji ningetoa malalamiko yangu.ILikuwa sehemu sahihi ya kulalamika na kuelezea kesi ambazo wamezikalia mafaili yake

Huoni hata jaji mkuu aliiilalamikia serikali kuwa bajeti ya mahakama haitoshi? Je kulalamika huko kwa jaji mkuu ni kuingilia utendaji wa serikali la hasha!!!

Halafu hukumu hutolewa kwa kuzingatia sheria na ushahidi hivi wewe kwa akili yako ya uanasheria koko unaosema umesomea unategemea jaji au hakimu aamue kesi kwa ku-base kwenye ya aliyosema raisi? Anaweza andika kwenye judgement kuwa nakupeleka jela kama raisi alivyosema?

Ujumbe wa Raisi umefika ndio maana majaji NA wanasheria walimshangilia sana wanajuana wenyewe na wanajijua vizuri.

Wewe nafikiri ni katika wale waliokuwa wamenuna sana wakati Raisi anahutubia pale.Utakuwa mfuasi wa Lowasa kidonda cha kupigwa chini hakijapona bado .Pole sana.
 
Kauli ya rais imeingilia uhuru wa mahakama, simple as that, ipo wazi kabisa hiyo.
Nakubaliana nawe kabisa wengi wetu tunatizama ulichokiandika katika muonekano wa kawaida, ni vigumu kukielewa, kwasababu wewe umeelezea madhara ya kauli ya Mheshimiwa Rais kwa mtazamo wa kisheria, kwa hiyo wengi wetu tunajibu kwa jazba na ushabiki.
 
Kwa hiyo unategemea wamfanye nini Raisi wa JMTZ? Sana sana kama kuna kosa lolote alilofanya watataka awaombe msahamaha jambo ambalo tayari alishalifanya jana kwa kusema mwishoni wa Hotuba yake kwamba ,,kama nimewakwaza naomba mnisamehe", sasa kuna nini tena cha kujadili hapo?

Hawawezi kumfanya chochote, ila nimeshangaa kwa Mkuu wa nchi kuuliza swali alilowauliza, kwa akili ya kawaida tu kuna mtu angejibu kweli umetukwaza? Hivyo itoshe tu kusema maneno ya mkuu wa nchi huchukuliwa kwa uzito mkubwa kuliko mtu yeyote, hivyo ni budi washauri wake wakamsihi kujizoeza namna ya kuongea hasa pale jambo linapokuwa ni public. Mambo yakiwa inhouse siyo shida,shida ni inapoonwa na public!
 
Tatizo unaishi kwa kukariri na ushabiki badala ya kufikiri...kwa kina, sio lazima uishi kwa kushabikia kila kitu
 
Hawawezi kumfanya chochote, ila nimeshangaa kwa Mkuu wa nchi kuuliza swali alilowauliza, kwa akili ya kawaida tu kuna mtu angejibu kweli umetukwaza? Hivyo itoshe tu kusema maneno ya mkuu wa nchi huchukuliwa kwa uzito mkubwa kuliko mtu yeyote, hivyo ni budi washauri wake wakamsihi kujizoeza namna ya kuongea hasa pale jambo linapokuwa ni public. Mambo yakiwa inhouse siyo shida,shida ni inapoonwa na public!

Sisi tumemkubali Raisi Magufuli kama alivyo, na kila analolifanya kama jana ndivyo tunavyozidi kumkubali kwanza tangia Hotuba jana sijakutana na MtanZania yoyote yule wa kawaida ambaye ndiyo mpiga kura hata wale waliopigia kura Upinzani hakufurahishwa na Hotuba ya Raisi Magufuli na kama kuna chochote alichofanya jana ni kuongeza zaidi Imani wananchi tuliyonayo kwake!

Hivyo kama kuna ambao hawakufurahishwa ni wachache sana tena sehemu kubwa yao hawaishi TanZania na hawapigi kura, wao wanaishi Marekani na kutaka Raisi wa TanZania awe kama Raisi Marekani bila kuelewa kwamba TanZania siyo Marekani na kila nchi inafanana na Kiongozi inayemchagua na ndiyo maana sisi wengi wetu tumependezwa na aliyoyasema ila kwa mtu ambaye labda siyo Mtz na haishi TanZania hawezi kutuelewa lkn siyo muhimu kwetu, muhimu kwetu sisi tumemkubali jinsi alivyo na kama kesho uchaguzi kurudiwa Magufuli atashinda kwa asilimia zaidi ya 85%
 
Sisi tumemkubali Raisi Magufuli kama alivyo, na kila analolifanya kama jana ndivyo tunavyozidi kumkubali kwanza tangia Hotuba jana sijakutana na MtanZania yoyote yule wa kawaida ambaye ndiyo mpiga kura hta wale walipigia kura Upinzani hakufurahishwa na Hotuba ya Raisi Magufuli na kama kuna chochote alichofanya jana ni kuongeza zaidi Imani wananchi tuliyonayo kwake!

Hivyo kama kuna ambao hawakufurahishwa ni wachache sana tena sehemu kubwa yao hawaishi TanZania na hawapigi kura, wao wanaishi Marekani na kutaka raisi wa TanZania awe kama Raisi Marekani bila kuelewa kwamba TanZania siyo Marekani na kila nchi inafanana na Kiongozi inayemchagua na ndiyo maana sisi wengi wetu tumependezwa na aliyoyasema ila kwa mtu ambaye labda siyo Mtz na haishi TanZania hawezi kutuelewa lkn siyo muhimu kwetu, muhimu kwetu sisi tumemkubali jinsi alivyo na kama kesho uchaguzi kurudiwa Magufuli atashinda kwa asilimia zaidi ya 85%

Sawa
 
Mimi muanzisha mada nimemuelewa sana na kwa kweli kuna mambo hayako sawa. Ile ni kama Decree sasa Majaji na Mahakimu watatoaje hukumu ikiwa mkuu wa Nchi katoa hisia zake tena kwa Public? Nafikiri watu wa Sheria watusaidie kuliweka sawa jambo hili. Mahakamani ni sehemu pekee ambapo hata kama mtu kakosa vipi lazima utetez ufanyike, akithibitika kosa anahukumiwa kwa stahiki ya adhabu imfaayo.

Pamoja na uchungu mkubwa alio nao Mh Rais, lakini ajitahidi mambo mengine awaagize watendaji waandamizi INHOUSE! DPP kwa mfano uliotolewa wa Meno ya Tembo, lakini lazima uchunguz ukamilike, hii inasaidia kuipu
nguzia hasara serikali kama mtuhumiwa akishinda kesi hasa kama mashtaka hayakupangiliwa vema!

Ni ombi letu wanaomshauri Mh. wamsaidie ili kulinda hadhi yake!
Sasa mtu amepelekwa mahakamani kwa kosa la kukwepa kulipa Kodi nalo mpaka upelelezi akati ushahidi upo kabisa kuwa Jamaa hawajalipa Kodi! Hampo serious na hii nchi hata kama Hamumpendi Magufuri hapana sio kihivyo

Na yeye alisha sema mapema kabisa najua mtasema naingilia Mahakama......kwa akili ako fupi tuu ulitaka wakwepa kodi nao wajitetee akati sheria ipo wazi kuwa lazima ulipe Kodi! Alitoa kabisa na Mfano wa Wa wafanya biashara wawili yule anaye lipa kodi na yule asie lipa kodi! Hata kama Ni sheria hapo na nyinyi mmezidi sasa Mnakuwa na huruma hadi kwa wakwepa Kodi! Ukienda mahakamani kwa kosa la kukwepa kodi.....utafungwa tuu labda utumie rushwa ndo maana alimtahadharisha Mapema jaji mkuu
 
Siasa weka pembeni, ile kauli haikutakiwa kutolewa pale, kuna hatari watu kupoteza haki zao, kisa kufikia malengo ya kukusanya trilioni moja,
Wewe ni........ Haki gani mkwepa kodi anaipoteza so wewe unaunga mkono mtu kutokulipa kodi akati mama ntilie huku wanabanwa na kulipa kodi watu wenye vibanda....kosa la kukwepa kulipa Kodi unataka ufanye kama kesi ya Mirathi? Nani amekuroga wewe
 
Sasa mtu amepelekwa mahakamani kwa kosa la kukwepa kulipa Kodi nalo mpaka upelelezi akati ushahidi upo kabisa kuwa Jamaa hawajalipa Kodi! Hampo serious na hii nchi hata kama Hamumpendi Magufuri hapana sio kihivyo

Na yeye alisha sema mapema kabisa najua mtasema naingilia Mahakama......kwa akili ako fupi tuu ulitaka wakwepa kodi nao wajitetee akati sheria ipo wazi kuwa lazima ulipe Kodi! Alitoa kabisa na Mfano wa Wa wafanya biashara wawili yule anaye lipa kodi na yule asie lipa kodi! Hata kama Ni sheria hapo na nyinyi mmezidi sasa Mnakuwa na huruma hadi kwa wakwepa Kodi! Ukienda mahakamani kwa kosa la kukwepa kodi.....utafungwa tuu labda utumie rushwa ndo maana alimtahadharisha Mapema jaji mkuu
Kumbuka kua mpaka unaamua kumpeleka mtu mahakamani hicho unachompelekea mahakamani kinaitwa "tuhuma" na yeye anaitwa "mtuhumiwa" sio mhalifu hayo ni macho ya kisheria hivyo mpaka pale mahakama itakapothibitisha kua hizo tuhuma ni sahii basi anakua sio mtuhumiwa tena bali ni mhalifu na anatakiwa kupewa hukumu kulingana na tuhuma alizotuhumiwa nazo, sasa hizo ndio taratibu za kule mahakamani, na inabidi zifuatwe...
 
Kuna kesi tayari zinazoendelea, kumbuka hilo, na malengo hapa ni kukusanya fedha, na mahakama imeahidiwa bilioni 200, na nyingine kununulia ndege, ukiacha ushabiki, ambao hata mimi pia kama mwana ccm natakiwa kutetea kauli ya rais, na kufikiri kwa kutumia milango yote ya fahamu utaona ninalolisema, pale Rais kashauriwa vibaya, hakutkiwa kuongea vile.
Ameshauriwa vibaya na nani tena akati kakwambia kuwa Hotuba alioandikiwa hajaisoma kasema yale kutokana na mtazamo wake
 
Back
Top Bottom