Kauli ya Nasari imekuwa mtaji wa CCM wanadai katumwa na Dr. Slaa

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Source Star Tv

Nimemsikia kiongozi wa UVCCM akidai CDM ni hatari kwa taifa na Nasari katumwa na Dr. Slaa kwani ni kauli yake toka 1995 kuwa wataingia ikulu hata kwa kumwaga Damu.

Najiuliza 1995 Dr. Slaa alikuwa anagombea urais wa nchi gani?

Na wakazidu kwenda mbali kuwa CDM wanawagawa watanzania na wawaogope.

Na wamewataka CCM nchi nzima vijana na wamama waanze maandamni kulaani kauli za CDM .

Tujiandae kuona mukutano ya CCM mikoani kote.

My take:
CDM wamewaamsha CCM na wamepata pa kusemea tuone watafika wapi.
Nafikiri mda huu ulikuwa kuwakamata mafisadi papa ya CCM na kuyatupa sero sasa wanataka kupitisha upepo wapotezee kama kawaida yao Richmond, EPA..........
 
Source Star Tv

Nimemsikia kiongozi wa UVCCM akidai CDM ni hatari kwa taifa na Nasari katumwa na Dr. Slaa kwani ni kauli yake toka 1995 kuwa wataingia ikulu hata kwa kumwaga Damu.

Najiuliza 1995 Dr. Slaa alikuwa anagombea urais wa nchi gani?

Na wakazidu kwenda mbali kuwa CDM wanawagawa watanzania na wawaogope.

My take:
CDM wamewaamsha CCM na wamepata pa kusemea tuone watafika wapi.

wanatapatapa tu hao!
 
Walipolalia ccm ndipo chadema walikoamkia.
Watasoma namba awamu hii
 
Watawala wa CCM ni wagonjwa na kauli zao ni za kigonjwa kama wao.
 
Mtu akiishiwa sera utamgundua kwa kudandia vimaneno vidogo vidogo ili apate angalao pa kujishikiza.
 
Watanzania siku hizi wanajua tofauti ya mchanga na dhahabu, vichupa na almasi, CDM msiwajibu maana M/kiti alishasema pale pale kwamba hiyo siyo sera yenu, mbona hawasemi wabunge wa CCM mikoa yakusini walipodai wametengwa na wanataka kujitenga wahamie Msumbiji?
 
CDM 2005 ndo wameweka mgombea Urais kwa mara ya kwanza.
Hayo maneno ya 1995 sijui walimnukuu Dr Slaa wp!
Kweli ukiwa Kilaza hujifichi!
Hv Antony Mavunde(Mwenyekiti UVCCM-DOM alikuwepo kwenye hayo maandamano ya Dom?)
 
CCM walipotoa tamko kuwa Rais wa 2015 hatatoka kanda ya Kaskazini haikuwa kauli ya kuwagawa watanzania?
 
Ni uvivu wa kufikiri kuamini kwamba CCM itaokolewa na propaganda!! Wanatakiwa wajue kwamba watu hawana imani nao tena; hivyo uwezekano wa kufanikiwa kwa agenda yao ni mdogo sana!
 
wanadai Magamba wanataka kuandamana na wameshatoa maagizo kwa vijana wao ,wazee wao na wamama wao kupinga kauli ya Mhe.Nassari a.k.a Dogo janja .Nasubiri nione Magamba watakavyojiingiza kwenye mtego wa Makamanda ! Ndio pale msemo wa Uhondo wa ngoma utakapo kamilika .
 
CCM walipotoa tamko kuwa Rais wa 2015 hatatoka kanda ya Kaskazini haikuwa kauli ya kuwagawa watanzania?
muwasamee bure nimeona thinking capacity yao very low wanafikiri wataponyeka na fagio la chuma na sera yao ya kuwatisha wananchi siku hizi watanzania wanajua kichapo kipo palepale hawatoki kwani ujambazi wanaoufanya sio hatari kwa taifa?
 
kaka kichakare nimeiona asira yako mod akusamehe maana hii midudu ccm inakera mpaka unajikuta unaropoka mkuu jiandae na ban
 
Hiyo siyo issue, CCM walete nondo mezani tujadili wao hawana la kuongea wamebaki na uswahili. Watuambie mustakabal wa Rich, Dowans, Epa,Radar, Wanyama kwenda nje ya nchi, mikataba mibovu, kuuza ardhi ya nchi kwa wageni. Weka mezani watuambie A-Z
 
All in all,makamanda wawe makin na kauli zao zinaweza kuwa mtaji wa ccm. Kwa watu wenye fikra finyu!na humu jf pia kuna watu wanaandika vitu ambavyo vinakatisha tamaa watu wa eneo fulan au dini fulan kujiunga na M4C
 
Hiyo siyo issue, CCM walete nondo mezani tujadili wao hawana la kuongea wamebaki na uswahili. Watuambie mustakabal wa Rich, Dowans, Epa,Radar, Wanyama kwenda nje ya nchi, mikataba mibovu, kuuza ardhi ya nchi kwa wageni. Weka mezani watuambie A-Z
 
Mtaji wa sisiem nikurudisha mali za umma zilizo kwapuliwa!kwamtanzania mwenye akili timam hawezi kuvalia njuga kauli ya Nassari wakati kuna mafisadi papa wanatanua.
 
Back
Top Bottom