Kauli ya naibu wa nishati na madini

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,483
1,364
Wakuu ningependa tujadili kauli ya katibu wa nishati na madini aliyoitoa jana kupitia ITV habari wakati akielezea sababu ya kutembea na baadhi ya vitu alivyoibiwa ikiwepo passport na vitu vingine, kuna kauli aliyoongea ambayo ni "VIPESA" kwamba analazimika jutembea na vipesa kidogo ambazo zilikuwa TZS 1,000,000 pamoja na dollar 4,000. Je kauli ya vipesa ni kiswahili ambacho kipo au ni kauli ya zarau?
Karibuni mtoe hoja
 
Wakuu ningependa tujadili kauli ya katibu wa nishati na madini aliyoitoa jana kupitia ITV habari wakati akielezea sababu ya kutembea na baadhi ya vitu alivyoibiwa ikiwepo passport na vitu vingine, kuna kauli aliyoongea ambayo ni "VIPESA" kwamba analazimika jutembea na vipesa kidogo ambazo zilikuwa TZS 1,000,000 pamoja na dollar 4,000. Je kauli ya vipesa ni kiswahili ambacho kipo au ni kauli ya zarau?
Karibuni mtoe hoja

Vipesa=Vijisenti. Hata kwetu wapo, hawajaisha!
 
Inategemea; kama ukiweza kumiliki Tshs billion 2, ukiibiwa Tshs million 1, obvious unaweza kusema :''nimeibiwa vijisenti''. Hii ni kauli ya dharau kwa wasionacho.
 
Kweli Baba Riz anawasaidizi makini sana

Yaaani ndo maana kila kitu hata mgomo wa wafagiaji inabidi aingilie kati. Wasaidizi wake wanafanya mambo wale matapeli wa pale nje ya Bills cha mtoto. Utafikiri sio mawaziri.
 
Tangu jana mimi namtambua kwa jina la VIJIPESA naona katika familia amezaliwa mtoto mwingine happy birthday VIJIPESA
 
Kwa asiyejuwa Kiswahili kusema vijipesa au vijisenti inakuwa ni mwao, kwa Waswahili ni neno la kawaida kabisa na hata ukitembea na mabillioni inatakiwa usijikwaze kwa kusema natembea na "mapesa" au "mabillioni". Hata bwana "mapesa" aliomba msamaha wakati fulani kwa kauli yake hiyo.

Nna uhakika wote ambao mnashangazwa na hilo neno, Kiswahili si lugha mama kwenu.

"Nimejidundulizia vijisenti vyangu nikajijengea kibanda changu mtaa wa Mahiwa", Kumbuka hiyo ni prime area Kariakoo Dar. Na hilo ni jumba la vyumba sita ambalo kiwanja tu kwa sasa ni millioni 800.

Ni utamu wa Kiswahili.
 
Kaibiwa na kiburudisho alichokiokota mjini kasoro bahari haingii akilini chumba katika hoteli kubwa kama hiyo aingie mwizi ndio maana jana usiku polisi walikamata changudoa kibao Moro labda yote ni kumpata muhusika wa tukio ambae sidhani kama ni mjinga kiasi cha kuonekana viwanja vya Moro tena atakuwa kahamia mji mwingine,na labda tunaye jijini leo.
 
Wakati wa Jairo Sakata alipewa Mil4 kama posho ya kupitisha Bajeti ya siku moja na hajafanyiwa lolote hata baada ya kamati ya Bunge kubaini ubadhirifu huu. ataacha kuongea pumba kwamba alikuwa na VIJIPESA?
 
Ukimsikiliza vizuri yule dogo,(Mh Adam Malima) utajua anamlinda meneja wa hoteli asihojiwe wala asisumbuliwe na polisi maana anajua siri itavuja kuwa yule binti mweupe alietaka aletewe ajiburudishe nae ndie aliemuacha(kumuibia) sasa ukiwasumbua wale waliomletea siri itafichuka!!!aibu sana wakati kwa hali ya kawaida meneja na walinzi wa hoteli wangekuwa ndani sasa........muda ukifika tutajua yote subiri siku mbili au tatu hivi
 
huyu malima na mwanaasha lwao moja,hawajatofautiana kitu.serekali ya kishkaji ndio matokeo yake hayo
 
Hapa natetea matamshi tu: haya majibu mimi huwa nayapata sana, mfano ni huyu mama niliyemuuliza hivi: hii ni mimba ya ngapi? 'ni ya tisa' alinijibu na kisha nikamuuliza,unao watoto wangapi? 'Tutoto tunane tu'
Nadhani kwa mila zetu ni mwiko kuonyesha una vitu vingi...tumalaria tunane tu!
 
Kwa asiyejuwa Kiswahili kusema vijipesa au vijisenti inakuwa ni mwao, kwa Waswahili ni neno la kawaida kabisa na hata ukitembea na mabillioni inatakiwa usijikwaze kwa kusema natembea na "mapesa" au "mabillioni". Hata bwana "mapesa" aliomba msamaha wakati fulani kwa kauli yake hiyo. Nna uhakika wote ambao mnashangazwa na hilo neno, Kiswahili si lugha mama kwenu. "Nimejidundulizia vijisenti vyangu nikajijengea kibanda changu mtaa wa Mahiwa", Kumbuka hiyo ni prime area Kariakoo Dar. Na hilo ni jumba la vyumba sita ambalo kiwanja tu kwa sasa ni millioni 800. Ni utamu wa Kiswahili.
kuna mijitu mingine mnadharau za kishamba
 
Starehe gharama,safi sana machangu's wa moro anajitia mtoto wa mjini,tena nawapa issue huwa wk end frm ijumaa watendaji wengi wa jk wanakuja moro kupasha,endeleeni hadi wakome,hivyo vijisent alikuwa na nyingi zaidi ya hizo kwani alitoka kushikishwa mbeya na kuwaahidi wananchi uongo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom