Kauli ya Nahodha yamgeukia ‘kaa la moto’

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Kauli ya Nahodha yamgeukia ‘kaa la moto’
Friday, 07 January 2011 20:13

Hussein Issa na Hassan Mohamed
WASOMI wamekosoa kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, kuhusu vurugu zilizotokea Arusha kuwa ni tatizo la kisiasa, linahitaji suluhisho la kisiasa. Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wasomi hao walisema vurugu hizo haziwezi kusuluhishwa kisiasa kwa sababu kilichofanyika ni ukiukaji wa haki za binadamu.

Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdallah Safari, alisema vurugu za Arusha hazikusababishwa na mambo ya siasa, kwani zilitokea baada ya uvamizi wa polisi kwenye maandamano ya amani ya Chadema.

“Sikubaliani na kauli ya Waziri Nahodha kuwa vurugu hizo zisuluhishwe kisiasa. Hakuna suluhisho la kisiasa, kwa sababu vurugu hazikuwa za kisiasa, vurugu hizo zimesababishwa na polisi na tayari suala hilo liko mahakamani,” alisema na kuongeza: “Uhuru wa kuandamana ni haki ya kikatiba, polisi wanaarifiwa tu kuhusu hilo sio kuomba ruhusa, hivyo hawana nguvu kisheria za kuzuia maandamano.” Profesa Safari alisema inapofikia hatua ya polisi kuua raia, suluhisho la kisiasa haliwezi kuwepo, badala yake, suala hilo lishughulikiwe kisheria.

Kwa upande wake, Profesa Chris Maina, ambaye pia ni Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisisitiza kuwa dola inapaswa kuhakikisha haki za kikatiba za raia zinatimizwa, ikiwamo kuandamana na kutoa maoni yao. “Suala la msingi hapa ni haki za binadamu kuzingatiwa, watu waheshimu haki za kikatiba,” alisema Profesa Maina.

Hata hivyo, Mhadhiri mwingine chuoni hapo, Bashir Ali, aliunga mkono kauli ya Waziri Nahodha kuwa, vurugu hizo zinapaswa kusuluhishwa kisiasa, huku akipinga waziri huyo kugeuka msuluhishi suala linalohusu wizara yake.

“Naunga mkono kauli hiyo, lakini Nahodha hatakiwi kusema hayo, Waziri Mkuu ndiye anayepaswa kulitolea tamko kwa sababu yeye (Waziri Mkuu) ndiye kiongozi wa shughuli za serikali,” alisema Ali. Ali alisema serikali inapaswa itoe kauli kuhusu sakata la umeya wa Arusha na suala la katiba mambo ambayo ndio malalamiko ya Chadema yaliyosababisha maandamano hayo.

 
Serikali yasalimu amri kwa CHADEMA


*Yakubali kutatua mgogoro kwa mazungumzo

Na Reuben Kagaruki
SIKU mbili baada ya kutokea vurugu zilizosababisha watu wawili kuuawa na polisi kwa risasi, sita kujeruhiwa huku viongozi wa kitaifa na wabunge wa CHADEMA wakikamatwa, serikali imesalimu amri na kutangaza kushughulikia mgogoro wa
Arusha kisiasa ili kuupatia ufumbuzi.

Uamuzi huo ulitangazwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Shamsi Vua Nahodha, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu vurugu zilitokea mkoani Arusha juzi zikihusisha polisi waliokuwa wakidhibiti wafuasi wa CHADEMA waliodaiwa kuandamana kupinga uchaguzi wa meya, uliofanyika bila kufuata taratibu.

"Serikali imedhamiria kukutanisha wanasiasa wa pande husika (CCM na CHADEMA) ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Arusha, kwa kuwa wakati wa pande mbili kuridhiana umewadia," alisema Bw. Nahodha.

Alipoulizwa serikali ilikuwa wapi kushughulikia mgogoro huo hadi isubiri damu imwagike, Bw. Nahodha alisema hiyo ilitokana na kuwapo kwa nadharia na taaluma za aina tatu za kusuluhisha migogoro.

Alisema kabla migogoro haijatatuliwa ni lazima wahusika wakuu waamini kuwa kuna mgogoro.

"Pia kabla ya kutatua mgogoro huo ni lazima upate watu wanaokubalika kuutatua," alisema na kuongeza kuwa kigezo cha tatu ni kujua ni watu gani wanahusika.

"Kwa sasa naamini kuwa wahusika wakuu wanaamini hapa (Arusha) kuna tatizo," alisema, Bw. Nahodha.

Hata hivyo alisema jitihada za siri zimekuwa zikifanyika kusuluhisha mgogoro huo, lakini hazikutoa matokeo yaliyotarajiwa na sasa kilichobaki ni kuutafutia ufumbuzi kwa uwazi.

Alipoulizwa na waandishi wa habari ni lini suluhu hiyo itapatikana, Bw. Nahodha alijibu;

"Nadharia ya kusuluhisha migogoro ni lazima wasiwepo watu ambao wana haraka, ni vigumu kusema usuluhishi utatumia muda gani, sana sana itategemea weledi wa wale wasuluhishi na wahusika."

Alipoulizwa ni kwa jinsi gani wananchi watamwamini yeye, hasa kwa kuzingatia tukio la mauaji ya juzi mkoani Arusha ni la pili kutokea kwake akishikilia nafasi nyeti serikalini, baada ya lile ya Januari 21, 2001 akiwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambapo wafuasi 21 wa CUF waliuawa; Bw. Nahodha alijibu;

"Mbona unihukumu kuwa mimi nimechangia maridhiano ya kikatiba Zanzibar iliyounda Serikali ya Kitaifa ambayo waandishi wa habari mnasifia?

"Mbona hamnisifii kwa mema? Hivyo ndivyo maisha yalivyo, ndiyo maana kuna wakati bahari inachafuka na kutulia."

Alisema Tanzania ni nchi yetu wote, hivyo tuna wajibu wa kuilinda amani iliyopo.

Akieleza kiini cha vurugu za juzi, Bw. Nahodha alisema viongozi wa CHADEMA hawakufuata ushauri wa polisi wa kuwataka kufanya mkutano peke yake na kuacha maandamano.

Alisema polisi walizuia maandamano hayo baada ya kubaini hayatakuwa na mwisho mwema. "Viongozi wa CHADEMA hawakufuata ushauri wa polisi na badala yake waliendelea na dhamira ya kuandamana," alisema na kuongeza kuwa baada ya wafuasi na viongozi wa CHADEMA kuandamana polisi walilazimika kuwatawanya.

Alisema baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao hawakukamatwa, walikimbilia kwenye mkutano ulioendelea vizuri, lakini baada ya kumalizika waliamuru wafuasi wao waende polisi kuwatoa wenzao waliokamatwa.

Bw. Nahodha alisema ili kuepusha shari baada ya kuona magari yakipigwa mawe, nyumba na vibanda kuchomwa moto, polisi walilazimika kuepusha shari.

Alisema katika vurugu hizo watu wawili waliuawa, na wengine sita kujeruhiwa. Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema alithibitisha watu hao kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Bw. Mwema alisema wakati wa kushughulikia tukio hilo watafuata utaratibu wa kisheria na iwapo wao (Jeshi la Polisi) wakishitakiwa wataenda kujitetea. Bw. Mwema alielezea kusikitishwa na vifo vya watu hao.

"Hata akifa mtu mmoja au kuumia ninasikitika, hatuna sababu ya kuficha idadi ya waliokufa...sisi hatupendi mtu afe au kujeruhiwa," alisema wakati akijibu swali kuhusu tetesi kwamba waliokufa katika tukio hilo ni 10.

Alipouzwa madai kuwa hivi sasa anatumika kisiasa, Bw. Mwema alijibu; " Natumika kwa mujibu wa sheria, sheria hizo hizo ndizo zinatumika kutuhukumu."

Kauli hiyo ya IGP iliungwa na Bw. Nahodha ambapo alisisitiza kwamba hajaona kama, Bw. Mwema anatumika kisiasa. "Kama anatumika kwa namna fulani kusaidia chama fulani hilo sijaliona," alisema Bw. Nahodha.

Bw. Mwema alipoulizwa sababu za kuongeza askari mkoani Arusha kutoka Chuo cha Polisi Moshi, Ukonga Dar es Salaam na Manyara, alikanusha askari wa Ukonga kupelekwa Arusha.

"Hakuna askari waliotoka Ukonga, lakini kuweka askari wa akiba kwa ajili ya kukabili yaliyotokea, sio kosa," alisema.

Katika hatua nyingine, wananchi mbalimbali wamelaani kitendo hicho, akiwamo Mhadhiri Msaidizi wa chuo cha Diplomasia jijini Dar es Salaam, Bw. Abdallah Majura aliyesema Jeshi la Polisi limeirudisha Tanzania hatua kadhaa nyuma kwa kutumia nguvu nyingi badala ya kuacha mgogoro wa uongozi wa Arusha kutatuliwa kwa mazungumzo.

Mhadhiri huyo alisema Tanzania imeshapiga hatua ndefu mbele kwa kusaidia kutatua migogoro mikubwa nje ya nchi, lakini kitendo hicho kimemsikitisha kwa serikali kushindwa kutatua mgogoro huo mdogo wa ndani.

"Ninakilaani kabisa kitendo hiki, polisi wanatakiwa kupewa elimu maalumu katika kutatua migogoro na kilinda haki za binadamu. Napendekeza turudi chini katika mazungumzo na ikiwezekana uchaguzi uliozua mgogoro ufanyike upya," alisema Bw. Majura.

Naye Catherine Malila alipiga simu cha habari na kulaani hatua hiyo ya polisi, akisema bunduki hazikuwa zinastahili kutumika kwa watu wanaopigania haki ya kidemokrasia, na kama ni muhimu zingetumike kwa mafisadi wanaofilisi uchumi wa nchi.




19 Maoni:

blank.gif

HAMISI said... WANAOTAKIWA KUSHTAKIWA HAPA NI POLISI WALIOWARUSHIA RAIA RISASI HADHARANI KAMA MAJAMBAZI. KITENDO CHA KUWAPIGA RISASI RAIA WAKIWA WANAANDAMANA NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI KWANI KOSA LA KUANDAMANA ADHABU YAKE SI KIFO.POLISI WOTE WALIOWARUSHIA RAIA RISASI WALIPASHWA WAPANDISHWE KIZIMBANI KWA KUTUMIA EXCESSIVE FORCES KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI.
MIMI KM MWANASHERIA NILITEGEMEA CHADEMA WANGEWAFUNGULIA POLISI HAWA KESI ZA MAUAJI THE NEXT DAY KWANI NI KINYUME NA HAKI ZA BINADAMU NA PIA NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI KUWAPIGA RISASI RAIA ETI KWA KOSA KUANDAMANA.KIKWETE ANA HASIRA ZA WATU KUMKATAA KWENYE UCHAGUZI ULIOPITA KUTOKA USHINDI WAKE WA ASILIMIA 84 MPAKA 60 KWAHIYO ANAJARIBU KUTUMIA MABAVU KUWATAWALA WATANZANIA WA ARUSHA WALIOMKATAA KWA USANII KAMA MUGABE WA ZIMBABWE BAHATI MBAYA WATANZANIA HATUTAMRUHUSU KUFANYA HIVYO KWANI KUANZIA SASA TUTAANZA KUKUSANYA MIKANDA YOTE YA MASHAMBULIZI YAKE ANAYOYAFANYA DHIDI YA RAIA TAYARI ANA DAMU MIKONONI MWAKE KWAHIYO BADO ATAENDELEA NA OPERATION YAKE YA KUUWA RAIA ILI KUMFIKISHA KWENYE MAHAKAMA ZA KIMATAIFA.

January 6, 2011 9:08 PM
blank.gif

Anonymous said... huyo Mwema hana ufahamu wowote yeye hawezi sema anaumia kuona mtu anaumia.Police wa tanzania ni aibu bora vibaka kuliko police si lolote ni wendawazimu wasio jua wanafanyanini.Na huyo kikwete mtu wa visasi tuuuu.Na raisi mchovu kuliko wote waliotangulia hana maana wala nini.na sidhani akija marekani atatamani kukutana na Oboma tena .mjinga alikuja huku anajifanya kondoo kumbe mgaidi tu.Police nimakosa kumshambulia mtu asiyefanya vulugu.
January 6, 2011 10:24 PM
blank.gif

JOJAS BRAND said... Mh.Nahodha, ninakupongeza kwa kauli yako nzuri yenye faraja.Lakini ninaomba ukae na Mh.Makamba umfunde awe na kauli nzuri aache kauli za kihuni wakati yeye ni Mzee na heshima zake.Na istoshe ni Katibu mkuu wa CCM kitaifa.
Mh.Nahodha ninaomba ufunde Afande Mwema aache kutumiwa na CCM afuate Job discription zake zinavyo muongoza.

January 6, 2011 10:53 PM
blank.gif

Anonymous said... Ama kweli kuna watu na watu. Hivi hawa watu wanaomtaka IGP Mwema na Waziri Nahodha wajiuzulu kutokana na fujo za huko Arusha zilizosababisha vifo vya watu WAWILI TU wanasema kutoka moyoni au mchezo wa siasa tu?
Sikusikia kelele kama hizi za kumtaka IGP Mahita kujiuzulu pale wazanzibari ZAIDI YA ISHIRINI walipopigwa risasi na polisi kule Pemba kwenye maandamano kama hayo

Hivi wa Pemba si watu au uraia wao ni daraja la pili? IGP Mwema na Nahodha msijiuzulu. Mliofanya ni tone kwenye bahari ya waliofanya wenzenu na hakuchukuliwa hatua yoyote.

January 6, 2011 11:34 PM
blank.gif

Anonymous said... Polisisiem na Usalamapinduzi wa Taifa ndio wanavunja amani ya nchi hii.
January 7, 2011 12:08 AM
blank.gif

Anonymous said... Huyu waziri na Mwema nadhani mpaka sasa hawajatambua kwamba watanzania kadhaa wameuliwa kwa kupigwa risasi na polisi. Hiyo ni jinai. Ni kitendo ambacho maneno matamu hayatafuta. Nani alitoa amri ya kutumia risasi? Waaandishi wa habario hawakuuliza swali hilo. Nani alitoa amri ya kutumia risasi dhidi ya wanatanzania waliokuwa wakiandamana na kupeleak maafa na majeruhi ? Kama ni Kikwete, au huyo Waziri au Mwema - wanapaswa kufunguliwa mashtaka ya jinai. Hakuna lingine.
January 7, 2011 12:45 AM
blank.gif

Anonymous said... Bwana Nahodha - the police using live bullets shot dead innocent demonstrators and at the same time caused widespread mayhem including serious injuries. Someone has to be accountable for these crimes. Who gave the orders to use live bullets. Who, we ask ? This is a serious matter. That the people demonstrated is not an excuse to shoot them. The dead should not have died in vain; justice must be seen to be done.
January 7, 2011 12:59 AM
blank.gif

Anonymous said... Maridhiano sawa lakini baada ya maridhiano wale wanaohusika na mauaji ya raia wasio na hatia wapelekwe kwa Bw. O Campo kule The Hague, na tuanze na Benjamin kwa mauaji ya makumi ya watu kule Pemba mwaka 2001
January 7, 2011 1:13 AM
blank.gif

Anonymous said... Watu wa Pemba waliopigwa risasi ilikuwa jinai. Na inafaa jinai hiyo na nyingine huko Zanzibar zifuatiliwe na mashtaka kufunguliwa. Haikuwa haki.Hoja kwamba kwa kuwa hayo yalijiri Unguja basi tufumbe macho kuhusu Arusha ni udhalimu wa kijinga. Mnasema kuwa wale watu waliouliwa Arusha ndiyo waliowauwa watu huko Pemba na kwingineko. Wote ni victims. Hatua kaliya kisheria isipochukuliwa dhidi ya serikali kuhusu maafa ya Arusha basi ngoma itakuwa ile ile iliyoanzia, pengine, Pemba. Mhalifu ni mhalifu, yeye si mjumbe au mwakilishi wa eneo lolote.
January 7, 2011 1:25 AM
blank.gif

Anonymous said... Nahodha ulikuwa wapi kujua kama kuna tatizo Arusha au ulikuwa nje ya nchi ndo umekuja jana hufai wewe,Mwema na polisi wake wajinga waliofeli wakapata zero ndo wameona kuwa Police ndo kila kitu ni mambumbumbu wa sheria na wasiojua kusoma na kutafsiri vifungu vya sheria ni ibara gani na kifungu kipi ambacho kinasema polisi wana haki ya kutoa vibali vya mikutano kama si ujinga wao wajue wajibu wao ni kulinda raia na mali zao si kuzuia mikutano Mwema elewa baba liishia darasa la ngapi wewe yaani unazidiwa busara na kamanda Polisi aliye isoma katiba na akaruhusu maandamano,hivi sasa nyie mnalinda viongozi na mali zao,hufai bora hata Mahita.
January 7, 2011 1:33 AM
blank.gif

Anonymous said... Makamba umeamkaje hadi kuanza kutumia Biblia?au una taka viongozi wa dini nao waongee kwa kutumia biblia mtaanza kusema kuna udini,au wewe unaona uchaguzi wa mayor Arusha ulikuwa sahihi kwa wewe tunafahamu ulichofukuziwa ualimu wako hata communication skills hujui una kauli mbovu kama mwendawazimu nenda kasuluhishe basi kule Arusha na si porojo CCM(Chama Cha Majambazi) kinawafia mtake msitake mwisho wenu umewadia.
January 7, 2011 1:41 AM
blank.gif

Anonymous said... Huko kwa Ocampo na Slaa apelekwe,kuna mali za watu na roho za watu zimeteketea.
January 7, 2011 1:57 AM
blank.gif

Maulana said... wananchi msiwe na hasira na police, tulaumu tulikojikwaa sio tulikoangukia. police ni watanzania kama sisi,ni wadogo, wapwa na binamu zetu, huwa tunahenya nao na familia zao katika huduma mbovu mbalimbali zinazotolewa na serikali ya CCM. Walichokifanya police kupiga watu risasi sio kwa matakakwa yao wenyewe, kwani nature ya kazi ya askali yoyote ni kupokea na kutekeleza amri kwanza na kuhoji baadaye. kuna chain of command inayoanzia kwa wanasiasa (CCM)kwenda kwa amiri jeshi mkuu (mwenyekiti wa CCM taifa)kupitia Waziri wa mambo ya ndani kwenda kwa IGP Mwema kwenda kwa kamanda wa police mkoa wa Arusha kwenda kwa makamanda mbalimbali wa mkoa na wilaya kwenda kwa vijana (police) ambao wanatekeleza amri ya kuchapa na kuua. hivyo wa kulaumiwa hapa sio police ila CCM. maana kama A=B na B=C basi A=C. Ukiangalia chanzo cha mgogoro wenyewe ni uchaguzi wa Meya wa jiji la Arusha ambao CCM ilishauchakachua kama kawaida yake. Hata zile taarifa za kiintejensia alizodau IGP huwenda zilitolewa na makada wa CCM nani anajua? Si wangeacha maandamano yafanyike na kumpiga risasi yule tu anayefanya vurugu wakati wa maandamano?
January 7, 2011 2:36 AM
blank.gif

Anonymous said... Wewe (mwandishi)Kagaruki haufahamiki. Umeona wapi serikali kusalimu amri? Mbona unapandikiza chuki baina ya serikali na raia wake. Umesomea wapi wewe. Rekebisha articles zako na uwache tabia na ukereketwa wa kipuuzi!
January 7, 2011 2:42 AM
Steven said... CCM, Kikwete and his government will pay for every drop of innocent blood spilled in this fracas. There was no reason to prohibit the demonstration and after all who gave the police to act against the very constitution they swore to safeguard? The constitution says of freedom to meet, demonstrate and express views while the police who have of recently demonstrated to be CCM bootlickers act the opposite.
Shame to Kikwete and his government! we want an independent inquiry on what transpired at Arusha. It is disgusting and in fact a great shame to see Mr Mwema the IGP defending this ruthless act by his Police. In the culture of good governance The Minister of Home Affairs, IGP, and Arusha RPC could have resigned to pave way for an independent inquiry but not here in Tanzania. Where is the good governance trumpeted several times by Mr Kikwete? The International Court of Justice should take action on all involved.

January 7, 2011 4:39 AM
blank.gif

Anonymous said... Tanzanians, this a day of mourning, a day of shame. Our fellow citizens have been cut down by the ruthless CCM machine.The killers are not even remorseful. As I write, nobody has been charged for murdering or severely injuring our people for ostensibly demonstrating. When did peaceful protest become an act deserving of capitol punishment.We are indeed living in very dangerous times.And,to make it worse, the CCM leadership is going about its business -smiling- as if nothing serious has happened! I hope and expect men and women of moral substance will resign from the CCM cabinet imediately otherwise they will be complicit of the Arusha massacre and blood-letting. Pinda ,Tabaijuka - where are you. Those who are supporting the CCM action should be ashamed ;in fact I don't have time for them because they are exhibiting sub-human tendencies. Ewe Mola tulinde kutoka katika shari ya wakatili, nyamaume na mijitu isiokuwa na mipaka katika maisha. Amin,Amin ,Amin.
January 7, 2011 6:31 AM
blank.gif

Anonymous said... You didn't see Slaa and Mbowe laughing when they came out from court as if there is nothing happened? ooh God punish these peoples who are pretending to be with poor while they rob from poor their house wives because of their wealth from our tax. Aaamin
January 7, 2011 9:54 AM
blank.gif

Anonymous said... I am not supporting Mbowe or Slaa at all. In fact, I think some of their politics is odious,divisive and dangerous. What I am supporting is the right to demonstrate, the right to life and the right to the due process of law.I believe the govt mismanaged the demostration and as such we have to live with the consequences of their ineptitude. Lives, some very young, have been lost. Is there any justification. Who was incharge and is there a case of incomptetence,lack of pre-planning or foresight. Oh no, I am not in the Mbowe/Slaa mad bandwagon but I will support their rights (and of their supporters) though I disagree with their style and brand of politics. As for their laughing, I think it is all a show off, "You see, we are out" - gangster style. I wouldn't bother, it is to be expected from the lot. Maybe the deaths and the mayhem to them is a "political gain". Still that does not stop me and you to fight for RIGHTS and JUSTICE. The standards of many politicians are very low; I am sure you don't want to be judged by those sub-standards. - Mohamed
January 7, 2011 11:32 AM
blank.gif

Anonymous said... Sasa Mimi (Makamba) nawapa pole walioathirika na maandamano hayo lakini pia nalilia mali za CCM zilizoharibiwa. Gari la katibu wangu wa Mkoa limevunja vioo na ofisi yetu imeharibiwa vibaya," alisema Makamba mwisho.

Hii ni kauli ya kiongozi anaeongoza watu. Yaani ndugu zangu watanzania tunakubali upumbavu huu. Kweli watu wameuwawa, wamejeruhiwa bila sababu yeye analilia mali wakati hiyo mali imeharibiwa baada ya polisi kupoteza amani. Na isitoshe Roho ya mtu, uhai wa mtu haupatikani lakini yeye analilia magari, malandicruza. Ninaomba watanzania mtafakari mnisaidie kumjibu. Makamba upo njia ya parapanda .........

January 7, 2011 12:37 PM
 
Wananchi CCM na Jeshi la Polisi. Katiba Mpya Ikipigiwa Kura na Wananchi Hili Swala la Mauaji Tutajua Nani Alitoa Ruhusa. Sasa Hivi Pigeni Danadana Tutaonana Mahakama ya Uhakika Sio Hizi za CCM.
 
Kauli ya Nahodha yamgeukia ‘kaa la moto'
Friday, 07 January 2011 20:13

Hussein Issa na Hassan Mohamed
WASOMI wamekosoa kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, kuhusu vurugu zilizotokea Arusha kuwa ni tatizo la kisiasa, linahitaji suluhisho la kisiasa. Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wasomi hao walisema vurugu hizo haziwezi kusuluhishwa kisiasa kwa sababu kilichofanyika ni ukiukaji wa haki za binadamu.

Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdallah Safari, alisema vurugu za Arusha hazikusababishwa na mambo ya siasa, kwani zilitokea baada ya uvamizi wa polisi kwenye maandamano ya amani ya Chadema.

"Sikubaliani na kauli ya Waziri Nahodha kuwa vurugu hizo zisuluhishwe kisiasa. Hakuna suluhisho la kisiasa, kwa sababu vurugu hazikuwa za kisiasa, vurugu hizo zimesababishwa na polisi na tayari suala hilo liko mahakamani," alisema na kuongeza: "Uhuru wa kuandamana ni haki ya kikatiba, polisi wanaarifiwa tu kuhusu hilo sio kuomba ruhusa, hivyo hawana nguvu kisheria za kuzuia maandamano." Profesa Safari alisema inapofikia hatua ya polisi kuua raia, suluhisho la kisiasa haliwezi kuwepo, badala yake, suala hilo lishughulikiwe kisheria.

Kwa upande wake, Profesa Chris Maina, ambaye pia ni Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisisitiza kuwa dola inapaswa kuhakikisha haki za kikatiba za raia zinatimizwa, ikiwamo kuandamana na kutoa maoni yao. "Suala la msingi hapa ni haki za binadamu kuzingatiwa, watu waheshimu haki za kikatiba," alisema Profesa Maina.

Hata hivyo, Mhadhiri mwingine chuoni hapo, Bashir Ali, aliunga mkono kauli ya Waziri Nahodha kuwa, vurugu hizo zinapaswa kusuluhishwa kisiasa, huku akipinga waziri huyo kugeuka msuluhishi suala linalohusu wizara yake.

"Naunga mkono kauli hiyo, lakini Nahodha hatakiwi kusema hayo, Waziri Mkuu ndiye anayepaswa kulitolea tamko kwa sababu yeye (Waziri Mkuu) ndiye kiongozi wa shughuli za serikali," alisema Ali. Ali alisema serikali inapaswa itoe kauli kuhusu sakata la umeya wa Arusha na suala la katiba mambo ambayo ndio malalamiko ya Chadema yaliyosababisha maandamano hayo.


Polisi wanapaswa kujua kuwa hizo bunduki hazinunuliwi na fedha za Rostam na Kikwete bali kodi za Watanzania Mwema Umemwaga damu nawe utalipa hiyo damu mbele ya haki
 
Hao ni wasomi uchwara. Kama si vurugu za ki-siasa mbovu ya chadema ni nini? haya waingie tena mitaani, waone cha mtema kuni.

Mi post mireeeeefu, nani mwenye time ya kuisoma hiyo? come with short posts, straight to the point!
 
Polisi wanapaswa kujua kuwa hizo bunduki hazinunuliwi na fedha za Rostam na Kikwete bali kodi za Watanzania Mwema Umemwaga damu nawe utalipa hiyo damu mbele ya haki

Damu zilizomwagika zimesababishwa na viongozi wa Chadema, msitake kurusha.
 
Damu zilizomwagika zimesababishwa na viongozi wa Chadema, msitake kurusha.

Kiongozi gani wa cdm aliyerusha risasi na kuua? Umeamua kupayuka tu ili mradi na wewe uonekane kuchangia!
 
Tabia ni kama mimba huwezi kuificha hao ndo ccm bwana wameonyesha jinsi walivyo madikiteta
 
Kauli hiyo ya IGP iliungwa na Bw. Nahodha ambapo alisisitiza kwamba hajaona kama, Bw. Mwema anatumika kisiasa. "Kama anatumika kwa namna fulani kusaidia chama fulani hilo sijaliona," alisema Bw. Nahodha.


There is a swahili saying "........ haoni kundule" how can the minister in charge of internal security and of the ruling party admit that the police are impartial!!
 
Hao ni wasomi uchwara. Kama si vurugu za ki-siasa mbovu ya chadema ni nini? haya waingie tena mitaani, waone cha mtema kuni.

Mi post mireeeeefu, nani mwenye time ya kuisoma hiyo? come with short posts, straight to the point!
Cha mtema kuni utakiona wewe mpinga maendeleo. Unataka Watanzania wakae kimya mpaka lini? Wamechoshwa na uongozi mbaya wa kikwete. Tunataka mabadiliko katika jamii yetu.
 
kauli ya Vuai yageuka mimi? ha ha ha ha ha ha amegusa pabaya! teh teh teh teh teh
 
Nahodha anataka kusema mauwaji ya kisiasa ni halali? Wanavyo tuibia kisiasa kwa kuilipa Door Ones (DOWANS) -Mradi wa Chama "No 1" vivyo hivyo wanataka kuhalalisha mauaji ya raia! Hii ni JINAI!
 
Damu zilizomwagika zimesababishwa na viongozi wa Chadema, msitake kurusha.


Zomba, Acha Ushabiki na Umbumbumbu, Kwenye Ukweli Kuwa mkweli kama unahofia kuachishwa kz Nyamaza,Usijipendekeze kupita kiasi Uta*******************kwa.
 
Polisi wanapaswa kujua kuwa hizo bunduki hazinunuliwi na fedha za Rostam na Kikwete bali kodi za Watanzania Mwema Umemwaga damu nawe utalipa hiyo damu mbele ya haki

Hawa ni watu wanaotakiwa washitakiwe kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai period. Lazima tuwe na katiba itakayo walazimisha watu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa watumikia wananchi na viongozi wanaojali wananchi na maslahi ya nchi yao. Hatuhitaji vyombo vya ulinzi na usalama vinavyo tumikia mafisadi na maslahi yao na mbaya zaidi wengi wao wakiwa wanatumiwa na mafisadi huku wamechoka mbaya.

 
Back
Top Bottom