Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

Observer2010

Senior Member
Oct 29, 2010
195
44
Baada ya vyombo vya habari vilivyokuwa vimenunuliwa na genge la mtandao kumsakama sana kwa habari nyingi za kumponda. Mkapa aliwahi sema maneno machache sana kuwa Watanzania tutamkumbuka.

Kwa kweli hali ya nchi iliyopo saizi hakika jamaa tutamkumbuka tu, tutake tusitake. Nchi kila kitu kinaenda hovyo, na wanaonufaika ni wachache waliokuwa vinara wa hilo genge. Hakika sipati picha itakapofika 2014 hali itakuwaje. Saizi hela haina thamani kabisa, naamini soon BOT itaprint note zingine za elfu 20 na elfu 50. Ki ukweli buku 10 haina thamani tena. Ukishachenji imeisha.

Nchi huwa haiongozwi kwa blabla bali inahitaji commitment ya hali ya juu sana.

Kila la kheri.....
 
Mimi namkumbuka kwa yale niliyoyaona kama vile shule alizojenga kwenye kila shule iliyokuwepo, maji ya ziwa victoria kuweza kutumiwa na wakazi wa maeneo yale, bila shaka na mengi mengine.
 
Ndiyo, tutamkumbuka kwa jinsi alivyofisadi nchi yetu na kuwawezesha mafisadi wenzake kuendeleza libeneke. Ni Mkapa huyu huyu aliyekuwa akiapa kila kukicha kuwa "over my dead body," kuhusu Kikwete kuukwaa urais. Sasa atueleze ilikuwakuwaje?
 
Kwa watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri wakiona wenzao wanafanya kazi wanachukulia kirahisi na kuona wao wanaweza kufanya vizuri zaidi. Mkapa alikuwa mchapakazi sana na ana uwezo mkubwa sana wa kufanya maamuzi. Kilichotokea wanamtandao wakadhani wao wanauwezo zaidi na wakabeza aliyofanya Ben. leo wako wapi? Angalia deni la taifa, Ben alilipunguza sana na nchi ikawa inakopesheka. leo deni linatisha. Tunarudi kule kwa mwinyi ambapo Tz hatutakopesheka tena.
 
Akumbukwe kwa nini naye huyo? Kuna tofauti gani ya maisha baina ya utawala wake na ule wa Mwinyi na Kikwete? Rumba bado ni kali tu na Tanzania hatujawahi kuwa na ahueni ya maisha hata siku moja. Na hapo wala sijagusia mambo mengine….
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yeah,ni lazima akumbukwe,hapa duniani kukumbukwa ni lazima iwe kwa mema ama mabaya
kila kiongozi ana mabaya yake na mazuri yake,Nitamkumbuka Mzee Mkapa kwa project 3.
1,Ni kuhusu ule mladi wa maji ziwa victoria
2.uwanja mpya
3.Barabara ya kwenda MWANZA
 
Ndio rais pekee alidhamilia kutuondoa kwenye mnyororo wa ukoloni wa utegemezi kwa wazungu, alilipa madeni na nchi ilipiga hatua mpaka wakasema injini ya uchumi imewashwa bado kupaa! Sikusikia tamko la masheikh wala la maaskofu!, akisema fungeni mkanda tufanye kitu tunamuelewa na anafanya kweli!, migomo iliyopo niliwahi kuisikia kipindi cha mwinyi, sio nyerere wala mkapa!
 
Mwizi tu huyu! hajajibu tuhuma mbali mbali zinazomkabili ikiwemo kufanya biashara akiwa Ikulu, kuhusiana na ufisadi wa Rada, ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi, wizi wa Kiwira, kuuza nyumba na Serikali kwa bei ya kutupa, wizi wa mabilioni ya EPA, Meremeta, Kagoda ambavyo vilifanyika akiwa madarakani. Kuwaleta Net Group na kuwakabidhi management positions za TANESCO na kuwalipa mabilioni chungu nzima pamoja na kuwa hawakujua lolote lile kuhusu umeme kisha kuwashinikiza kusaini mkataba na kampuni yake ya wizi ya kiwira wa shilingi bilioni 326. Angekuwa china angepata habari yake.
 
Unapokuwa kiongozi kuna makosa ya direct na indirect swala la kumwachia kiti jk ni jopo zima la ccm twambie ungekuwa wewe ungekataa kwan chama ni chake ofcourse ana mabaya yake kama binadam lakin huyu wa sasa da kazidi ishu kama epa ningumu kumuhusisha ben direct
 
Hata Mwinyi nae alitamka maneno hayo-hayo wakati anazunguka nchi nzima kuaga wananchi kuwa 'MTANIKUMBUKA'.
 
Mimi namkumbuka kwa haya yafuatayo;

1. Heshima ya mfanyakazi ilirudi.
2. Mkate wa AZAM 350/= shilingi za kitanzania.
3. Nauli ya dala dala kati ya shilingi 100-150 na wanafunzi 50 tu. Na katika hili alikazia kama hamtaki kufanya biashara hii wekeni magari yenu uwani na sisi tutatafuta namna ya kuwasaidia watanzania.
4. Thamani ya shilingi ilipanda na tukawa na akiba ya kutosha sana pale HAZINA, lakini sasa hata mishahara ya wafanyakazi mmmnh................!.
 
Swali kwa hawa watawala wetu,
a) Je tutawakumbukaje? Kama watawala ama!
b) Je tutawakumbuka kwa mema (mengi/machache) waliyoyufanyia?
c) Je tutawakumbuka kwa maovu (mengi/machache) waliyolifanyia taifa?
d) Tutawakumbuka kwa kuuendeleza na kuuenzi Muungano?
e) Tutawakumbuka kwa 'ruksa' au kwa 'zama za ukweli na uwazi' au...'kujivua gamba' ?

Naomba kuwakilisha mnidadavulie.
 
FOR sure President Benjamin Mkapa wa an intelligent person, more focused, pragmatic and with clear vision.During his leadership the national economy prospered, he controled economic shocks such as inflation.And above all, President Mkapa maintained a highest level of discpline within his party.Nowadays things are falling apart in every aspect of life, poor eduation quality, skyrocketing commodity prices, rampant corruption and indiscipline within the state machinery.Kwa kweli tuna kila sababu ya kumkumbuka Mkapa.
 
1.Alivunja mfumo wa ukusanyaji mapato kwa kuanzisha TRA. 2.Uwanja mpya wa Taifa. 3.Daraja la Rufiji, 4. Mtandao mzuri wa barabara.5.Kulipa madeni ya nchi, 6. Kukua kwa thamani ya shilingi, 7. Hakukua na mfumuko wa bei,8.Hazina ya kutosha pale BOT,9.Ajira kutokana na ubinafsishajia na makampuni mapya,10.Makundi hayakuwepo,11.Mrradi wa maji ziwa victoria,,12.ujenzi wa majengo pacha BOT,13.Migomo haikuwepo kabisa,14.Mfanyakazi na mkulima aliheshimiwa,15Mengine mengi
 
alijenga heshima ya taifa kimataifa...hakuleta migawanyiko ya kidini 'mimi ni rais watanzania wote,waislam, wakristo na wapagani....,' alidhibiti mfumuko wa bei..
 
Kweli mkuu! Kwa uchumi wa TZ Benjamin namfagilia. Alichukua nchi ikiwa na mfumuko wa bei 2 digits ukashuka mpaka 1 digit (asilimia 5 kama sikosei) tena huyu alikuwa mwandishi wa habari. Mchumi kachukua nchi mfumuko wa bei unapanda kila kukicha! Kibaya zaidi mimi naona wanatudanganya BOT inatoa statistics kuwa ni 1 digit asilimia 7 au 9 hivi wakati bei zinapanda kila kukicha. Mkapa alikusanya sana pesa na uchumi ulipanda kiasi, ila waliozifaidi ni wao wenyewe hivyo kwa kweli mtz wa kawaida kama mimi hakunufaika sana na hayo mazuri ya mkapa. Ila angalau mfumuko wa bei ulishuka sana. Mkapa pia aliuza mashirika yote pamoja na Julius kupiga kelele sana mei mosi kule Mbeya (sikumbuki mwaka) kuwa wakumbuke angalau mazuri ya awamu ya kwanza wayaendeleze alikuwa na deaf ears! Na yeye kauza nchi!!!!
Kwa watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri wakiona wenzao wanafanya kazi wanachukulia kirahisi na kuona wao wanaweza kufanya vizuri zaidi. Mkapa alikuwa mchapakazi sana na ana uwezo mkubwa sana wa kufanya maamuzi. Kilichotokea wanamtandao wakadhani wao wanauwezo zaidi na wakabeza aliyofanya Ben. leo wako wapi? Angalia deni la taifa, Ben alilipunguza sana na nchi ikawa inakopesheka. leo deni linatisha. Tunarudi kule kwa mwinyi ambapo Tz hatutakopesheka tena.
 
Back
Top Bottom