Kauli ya Mh. John Mnyika Juu ya Ongezeko la Posho Bungeni.

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
Wadau sina haja ya kupiga porojo bali soma mwenyewe uone jinsi serikali inavyojidhalilisha. Sihitaji kuichambua taarifa hiyo kwa sababu inajieleza.

Msimamo wangu juu ya suala zima la Posho! Kufuatia habari tarehe 28 Novemba kuhusu ‘kupanda kimya kimya kwa posho za wabunge kwa zaidi ya asilimia 150' tarehe 29 Novemba 2011 nilitoa kauli yangu kama mbunge na katibu wa wabunge wa CHADEMA kuhusu suala husika.

Katika kauli hiyo nilieleza kuwa: "Wabunge wa CHADEMA hatujapokea taarifa rasmi kwamba masharti ya kazi ya ubunge yamebadilika na kwamba viwango vya posho vimeongezwa. Wala kamati ya wabunge wa CHADEMA haijawahi kuridhia ongezeko lolote la posho ya vikao (sitting allowance) kwa wabunge. Napenda kutumia fursa kusisitiza msimamo wetu wa kutaka posho za vikao (sitting allowance) ziweze kufutwa kwa wabunge na katika mfumo mzima wa malipo ya wakati wa kazi miongoni mwa watumishi wa umma".

Hivyo, kama mbunge na katibu wa wabunge wa CHADEMA nilitoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete kwa niaba ya Serikali na Spika Anna Makinda kwa niaba ya Bunge kutoa kauli kuhusu suala hili ili kuondoa hisia zinazojengeka kwamba ‘wabunge wote tumekaa bungeni na kukubaliana kujiongezea posho ya vikao'. Kufuatia Spika Makinda kutoa kauli na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari tarehe leo tarehe 7 Novemba 2011 naomba kutoa msimamo wangu kama ifuatavyo: " Ongezeko la posho ya vikao lilofanyika linapaswa kusitishwa kwa kuwa limefanyika kinyume na taratibu na pia halina uhalali wowote kimantiki na halijazingatia uhalisia wa maisha ya wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla; nyongeza hiyo ya posho ya vikao ni haramu (Illegitimate).

Bado narudia kutoa mwito kwa Rais Kikwete kutoa kauli wake na wa Ikulu na Ofisi ya Rais kwa ujumla unaacha ombwe lenye athari kubwa kwa serikali na kwa bunge mbele ya wananchi ambao kwa mujibu wa katiba ibara ya nane ndio wenye mamlaka na madaraka. Aidha, kauli ya Spika Makinda kwamba nyongeza hiyo ya posho za vikao ni kwa sababu ya kupanda kwa gharama za maisha mkoani Dodoma haina ukweli, wala mantiki na ina mwelekeo wa upendeleo. Nyongeza hiyo ya posho ya vikao ni matumizi mabaya ya madaraka na ni dharau kwa walipa kodi wanaohangaika na kupanda kwa gharama za maisha na athari za ubadhirifu wa fedha za umma.

Ni udhaifu kufikiri kwamba suluhisho la kupanda kwa gharama za maisha ni kuongeza posho za kikao; tatizo la kupanda kwa gharama za maisha linapaswa kushughulikiwa kwa kuchukua hatua dhidi ya matatizo ya kiuchumi katika nchi ili kuweza kuwa na tija kwa wananchi wengi ambao ni waathirika zaidi wa kupanda kwa gharama za maisha kuliko wabunge. Pia, utetezi wa Spika Makinda kuhalalisha upandishaji wa kinyemela wa posho za vikao kwa wabunge haina maana kuwa kama sababu ingekuwa chanzo ni kupanda kwa gharama maisha ingepandishwa posho ya kujikimu (subsistence allowance) ambayo imebaki pale pale 80,000 .

Aidha kufuatia kauli ya Spika Makinda, hatua za kinidhamu zinapaswa zichukuliwe na Rais Kikwete dhidi ya Katibu wa Bunge Dr Thomas Kashilillah ya kutoa taarifa potofu kwa umma kwa kukanusha kwamba ofisi ya bunge haijaongeza posho kwa wabunge na pia kwa kufanya malipo kinyume na taratibu. Kugongana kwa kauli baina ya Spika na Katibu wa Bunge ni ishara ya kuwepo kwa jambo ambalo linafichwa kuhusu suala hilo la nyongeza haramu ya posho za vikao kwa wabunge na pia ni ushahidi wa taratibu kukiukwa hali ambayo inahitaji kauli kutoka kwa mwenye mamlaka kwa mujibu wa sheria kuhusu masuala ya posho za wabunge ambaye ni Rais.
Pia, katibu wa wabunge anapaswa kutuomba radhi wabunge kwa kauli yake kwamba mabadiliko ya posho za vikao yametokana na mkutano wa wabunge tarehe 8 Novemba 2011 kuiomba serikali ipandishe posho hizo za vikao.

Binafsi nilikuwepo kwenye mkutano huo wa tarehe 8 Novemba 2011 na hakuna uamuzi wowote ambao ulifikiwa wa kuiomba serikali ipandishe posho za vikao. Kilichotokea ni kwamba katika kuchangia maelezo ya serikali na ya bunge kuhusu masuala mbalimbali ya bunge na serikali yaliyojiri baada ya mkutano wa nne wa Bunge na mpangilio wa mkutano wa tano wa bunge, wabunge walipewa fursa ya kujadili taarifa hizo. Katika kujadili taarifa hizo wapo wabunge wachache waliotoka nje ya hoja za msingi na kuzungumzia kuhusu nyongeza ya posho ya vikao; hata hivyo mkutano huo wa wabunge haukufanya maamuzi yoyote na wala haukukamilika. Kabla ya majina yetu wengine kufikiwa kuweza kuchangia Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye kwa nafasi yake ya kiongozi wa shughuli za serikali bungeni ni mwenyekiti wa mikutano ya wabunge alieleza kwamba muda umemalizika hivyo mkutano na kwamba tarehe nyingine ingepangwa kwa ajili ya kuendelea kujadili masuala mbalimbali yaliyohojiwa na pia kuweza kutoa fursa kwa wabunge wengine kuweza kutoa maoni yao kuhusu masuala hayo. Katika hatua hiyo Waziri Mkuu Pinda alisoma majina yetu na kueleza kwamba mkutano huo wa wabunge ungeendelea katika tarehe nyingine lakini haukufanyika mkutano mwingine; hivyo katika mkutano wa tano wa bunge uliomalizika wabunge ambao mimi nilishiriki wabunge wote hatujawahi kukaa na kujipangia nyongeza ya posho za vikao kama inavyoelezwa hivi sasa wala.

Pia, wabunge hatujawahi kupatiwa nakala ya muktasari au kumbukumbu wa vikao vya kamati ya uongozi au vya tume ya bunge ambavyo vimekaa na kupitisha nyongeza ya posho ya vikao kutoka 70,000 mpaka 200,000 kama Spika alivyonukuliwa na vyombo vya habari. Ni muhimu watanzania wakazingatia kwamba mwenye mamlaka ya kupandisha posho za wabunge ni Rais na natoa mwito kwa Rais kukataa kupandisha posho za vikao kwa wabunge na badala yake azifute kabisa. Watumishi wote wa umma ikiwemo wabunge hatustahili kulipwa posho za kukaa kwenye vikao vyetu ambavyo mwisho wa mwezi tunalipwa mshahara kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Kufuatia hali hii, kwa kuwa sasa imeshatoka kauli rasmi ya bunge yenye kudhihirisha kwamba posho za vikao zimepandishwa kinyemela badala ya kufutwa kama tulivyotaka awali; tutaitisha kikao cha wabunge wa CHADEMA ili kukabaliana hatua za ziada za kuchukua kwa kuwa ofisi ya bunge na serikali wanaendelea kuingiza posho za vikao kwenye akaunti za wabunge hata baada za kuzipinga."

Katika kauli yangu ya tarehe 29 Novemba 2011 nilieleza kwamba ni vyema umma ukafahamu kwamba Sheria ya Utawala wa Bunge (National Assembly Administration Act) ya mwaka 2008 kifungu cha 19 kinataja aina ya posho ambazo zinaweza kutolewa kwa wabunge kama ambavyo Rais ataeleza kwa maandishi.

Katika kipengele (d) sheria imetaja orodha (i) mpaka (iii) ya posho ambazo wabunge wanastahili kulipwa za usafiri, kujikimu na wasaidizi. Katika orodha hiyo hakuna Posho ya Kikao (Sitting Allowance) ambayo inalipwa hivi sasa kwa kuwekwa kwenye akaunti za wabunge moja kwa moja ambayo kamati ya wabunge wa CHADEMA tunataka ifutwe mara moja kama sehemu ya mchakato wa kubadili mfumo mzima wa malipo ya posho kwa watumishi wa umma.

Kifungu 19 (d) (iv) kimempa mamlaka Rais ya kutoa posho zingine kwa wabunge kwa kadiri atakavyoelekeza; kifungu hiki kimetoa mwanya wa kutolewa kwa waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais wa tarehe 25 Oktoba 2010 wenye kumbukumbu na. CAB111/338/01/83 masharti ya kazi ya mbunge ambao umeeleza viwango vya posho mbalimbali ikiwemo kutoa posho ya vikao (Sitting Allowance).
Hivyo, ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge zinapaswa kuwaeleza watanzania iwapo waraka huo umebadilishwa na sababu za wabunge kutojulishwa kuhusu mabadiliko hayo. Aidha tarehe 29 Novemba 2011 nilieleza kuwa, iwapo mabadiliko hayo yamefanyika ni muhimu yakasitishwa kwa kuwa zitakwamisha utekelezaji wa mpango wa kufuta posho za vikao (sitting allowance) na kupunguza matumizi ya serikali kama ilivyoelezwa katika Ilani ya CHADEMA ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 pamoja na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano uliopitishwa bungeni mwaka 2011.

Izingatiwe kwamba uchumi wa nchi hivi sasa unasuasua, serikali ina hali mbaya ya fedha kutokana na kupungua kwa kiwango cha fedha kinachopatikana katika kodi na washirika wa kimaendeleo ukilinganisha na mahitaji ya bajeti; na hivyo kukopa kibiashara kwa ajili ya kuziba nakisi iliyopo. Kupungua kwa uzalishaji, kiwango cha fedha pamoja na kuongezeka kwa ubadhirifu katika matumizi ya rasilimali za umma kunachangia katika mfumuko wa bei hali inayohitaji mpango wa dharura wa kunusuru uchumi wetu ukaohusisha pamoja na mambo mengine kubana matumizi ya serikali. "

Binafsi natarajia serikali ije kwetu wabunge na mpango wa kukabiliana na ongezeko la gharama za maisha kwa wananchi badala ya kutuletea mpango wa kutuongezea wabunge posho za vikao huku mwelekeo wa uchumi na utekelezaji wa mipango ya maendeleoukiwa kwenye hali tete". Kamati ya wabunge wa CHADEMA ilikubaliana posho hizo zifutwe kwa kuwa Ilani ya CHADEMA ya mwaka2010 imeeleza kwamba lengo la msingi ni kuondoa posho za vikao (sitting allowance ) hatua ambayo itaambatana na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma kuendana na ujuzi, nafasi, wajibu ili wafanyakazi walipwe kwa haki kwa kile wanachofanya kwa haki. Uamuzi huu ungewezesha pia kuelekeza fedha zaidi katika miradi ya maendeleo.

Ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge zizingatie kuwa Serikali ya CCM imeridhia msimamo huo na kuuingiza kwenye Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano 2011/2012-2015/2016 uliosainiwa na Rais Jakaya Kikwete tarehe 7 Juni 2011 ambao kwenye ukarasa wa 17 unatamka bayana kwamba posho za vikao na nyinginezo zinapaswa kufutwa au kuwianishwa hivyo kuziongeza ni kupuuza mpango huo.

John Mnyika (Mb) 07/12/2011
Source: .
Nawasilisha kwa majadiliano zaidi.
 
Kweli hii ni dharau ya hali ya juu kwa wananchi wote kwa ujumla ambao kimsingi ndio waajiri wao!
Sijui tunakoelekea ni wapi jamani nchi hii.
Asante sana kwa taarifa!
 
Makinda anasema gharama za maisha zimepanda Dodoma!hapo ndo najiulza ina maana zimepanda kwa wabunge tu?je wananchi wengne wa kawaida hapo dodoma gharama ziko vile vile?shame on u bibi kiroboto
 
Kweli hii ni dharau ya hali ya juu kwa wananchi wote kwa ujumla ambao kimsingi ndio waajiri wao!
Sijui tunakoelekea ni wapi jamani nchi hii.
Asante sana kwa taarifa!

Nachelea kusema hili ni kosa lingine ndani ya muda mfupi bibi Kiroboto anaisababishia serikali yake badala ya kuikoa!!!! Kosa la kwanza ni jinsi alivyoendesha mjadala wa katiba bungeni kwa upendeleo.
 
Makinda anasema gharama za maisha zimepanda Dodoma!hapo ndo najiulza ina maana zimepanda kwa wabunge tu?je wananchi wengne wa kawaida hapo dodoma gharama ziko vile vile?shame on u bibi kiroboto
Kama ndiyo ametumwa na serikali aje ajenge hoja dhaifu vile basi bila ya shaka serikali itakuwa inashauriwa na watu waliojaa matope kichwani mwao.
 
Itisha maandamano.
Wasiposikia mzikate kama alivyofanya Zitto.
Yaani siku zinavyozidi kwenda ndiyo vinvyoona siasa inavyozidi kubinywa kutokana na kuchemka kwa serikali!!!! Maandamano mpaka kibali kitoke Ikulu indirect, unafikiri kuna kuandamana tena? Wewe jiulize Al Shabab hawapo 9 - Dec ambayo ni miaka 50 ya uhuru?
 
Ningekuwa housegirl wa Bi Mkora angeniongeza na mimi.
Sasa hapo!!!!!!!!!!!!!
Wamehalalisha,
traffic police kuomba rushwa,
Walimu kuuza ubuyu darasani,
Madaktari na manesi kuomba rushwa na kuiba dawa kupeleka kwenye pharmarcy na dispensary zao,
Mahakimu nao wakazane kurefusha kesi ili wapate chochote,
Wahasibu na wagavi , 'ten percent ',
Wahandisi kujenga vimeo wapate kinachobaki,
Wakulima kuuza mahindi nje,
Dadapoa kutumia 'carol light' afu kukubali bila kinga,
Wafanyabiashara kukwepa kodi na kuingiza magendo,
Wale maofisa nani nani kupanga dili za kuibia ofisi zao,
BAADA YA HAPO, KWISHINEI TANZANIA.
''Hivi tutaendelea kuangaliana hivi hivi. Kama hajafa mtu, siju!!!!"
 
Kweli hii ni dharau ya hali ya juu kwa wananchi wote kwa ujumla ambao kimsingi ndio waajiri wao!
Sijui tunakoelekea ni wapi jamani nchi hii.
Asante sana kwa taarifa!

ebwana 2mwondoeni huyo Jamaa kwani hatufai!
 
Makinda anasema gharama za maisha zimepanda Dodoma!hapo ndo najiulza ina maana zimepanda kwa wabunge tu?je wananchi wengne wa kawaida hapo dodoma gharama ziko vile vile?shame on u bibi kiroboto
...........Makamuzi upo right, kama wale mafisadi waliomweka pale (hapa namnukuu Sitta, mzee wa CCJ), maana walijiridhisha na kichwa chake kwamba wangekimudu, kwa kifupi mama huyu ni mvivu wa kufikiri, iwe ni kwa makusudi ama kwa kutofahamu.
 
Mheshimiwa Mnyika
Nimesoma liturugia yako hapa na sijaona mahali ulipokiri kuwa ulilipwa posho ya shs laki 2 katika kikao kilichopita. Kama hujalipwa hiyo fedha, hujapata barua kuhusu kubadilishwa viwango vya posho na kama hakuna jambo kama hilo lilijadiliwa bungeni, unatoa wapi ujasiri wa kutamka yote uliyotamka kwenye liturugia yako hii. Je kuna evidence yeyote umeweza kusite kuonyesha kweli umuzi ulishafanyika na utekelezaji tayari, au na wewe umendandia gari na kuwa "nasikia nasikia"? WHERE IS EVIDENCE HON MNYIKA?, TELL US DID YOUR ACCOUNT GOT CREDITED WITH THE NEW RATES OR NOT? I JUST WANT A SIMPLE ASNWER YES! OR NO!

Hivi kwa nini inakuwa vigumu kusema kuwa fedha hizo zililipwa na kuingizwa katika account yako wakati wa vikao vya bunge lilomalizika Dodoma? Nimesoma FB ya Zito, lituguia ndio hiyo hiyo haisemi kuwa fedha ziliingia kwenye account ya mheshimiwa Zito au la. Kama fedha ziliingia kwenya account yenu ni wapi mlihoji mabadiliko hayo, sana sana nakumbuka mlihoji mabadiliko ya kusign karatasi ya posho. Kwa nini jambo hili halikujadiliwa kwenye Kamati Kuu ya CDM iliyokutana na kuamua kupeleka wanywa juice Ikulu na kutujia na two paragraph ya upuuzi mliokubaliana, ambapo wewe ulitia sign. (Mnyika, I have faith on you before, but baada ya kusign kile kikaratasi wewe na Nchimbi, nilikushusha to the lowest level ever, umeyumba, umepwaya na umepoteza muelekeo. I pray wananchi wa ubungo walione hili ili kukufundisha adabu 2015)

Then najiuliza kama kweli ninyi CDM mna dhamira ya dhati ya kuikomboa nchi hii. Kama inakuwa vigumu kukiri kuwa fedha zililipwa na mkaona account imeshiba na hamkusema kitu,inawaondolea legitimacy ya kuja kusema misimamo ya kipuuzi na kizandiki leo baada ya habari kuvuja. Ukweli kukosekana kwa Dr Slaa Bungeni ni janga la taifa hili, angekuwa yeye angeshasema na kuuliza swali hilo bungeni pindi pale angeona fedha zimeingia kwenye account. Mnyika, Zito, Mbowe and all CDM hypocrites mnabwabwaja after the effect, vyombo vya habari vimewaumbua shame on you and i wish you all loose in the coming election ndio mtajua kwa nini tuliwachangua. I wish tungeweza kuchangua ngombe wakaenda bungeni, maana labda hao wangepiga kelele tukasikia!!
Nitafurahi ukinipa jibu moja tu, kuwa viwango vipya vimeshalipwa na wewe mheshimiwa Mnyika ulipewa hizo fedha, THEN utakuwa umepata uhalali wa kumtaka raisi amuwajibishe Dr Kashishila na Spika kukiuka kanuni ya 19.. whatever uliyosema, tofauti ya hapo ni wastage of time and nitaamini kauli ya Dr Kashishila.
 
Wabunge wa ccm watavimba matumbo yao sasa maana ile awali walikuwa wamevimbiana matumbo.
 
BONGOLAND bwana! Yaani hawa wasanii waliokubuhu wanaturejesha kwenye mjadala wa POSHO badala ya mjadala wa KATIBA MPYA!!!!!!!!!!!!! Akina Kanumba mko wapi - changamkieni hii filamu ya karne angaa tujiliwaze kwa kuangalia maigizo asilia.
 
Naona umerukia kumshambulia Mnyika na kujatibu kuonyesha mapungufu yake lakini hujafanikiwa!!! Na hii ndiyo kawaida ya wafuasi wa CCM kuacha mada na kujikita kujadili watu kama mlivyofanya bunge lililopita badala ya kujadili katiba mnamjadili Tundu Lissu!!!

Kiukweli Mnyika amejieleza vizuri na ana hoja nzito kama umeshindwa kuziona basi endelea na ushabiki wako.
 
Wabunge wa ccm watavimba matumbo yao sasa maana ile awali walikuwa wamevimbiana matumbo.

Watapasuka na kuzidi kunsinzia tu bungeni wewe unafikiri 200,000.00 mchezo bado per diem 80,000.00 na 50,000.00 ya mafuta yaani full kipupwe.
 
Kama tutakuwa na wabunge jasiri kama Mnyika 20 hakika viongozi wetu walafi hawatakuwa na amani hata kidogo.
Hongera Mnyika kwa kutoa kauli yako ambayo imekaa vizuri na itaisaidia serikali yetu.
 
Back
Top Bottom