Kauli ya Mch. Mtikila kuhusu katiba mpya hii hapa

Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila amesema Chadema ilikurupuka na kudandia hoja ya Katiba mpya ya nchi bila kuzingatia maslahi ya Watanzania na kuonya kuwa mchakato wa kuunda Katiba unaweza kushindwa kama utafanywa kwa lengo la kukidhi matakwa ya watu wachache wanaoshinikizwa na wageni.

Akizungumza kwa simu jana, Mtikila alisema si viongozi wa Chadema wenye dhamira ya dhati ya uundaji wa Katiba mpya kwa maslahi ya Watanzania, kwa kuwa wanataka Katiba iundwe, kwa maslahi binafsi kwa lengo la kuendeleza zama za ukoloni.

“Mimi nilipojaribu kuzungumzia Katiba mpya na haja ya kuwa na Serikali tatu, watu waliniona kichaa, jambo ambalo lilisababisha kampeni ya kutaka Katiba kuwa ngumu na isiyo na mafanikio … sasa watu hao hao wanataka Katiba mpya kwa maslahi yao,” alisema.

Hata hivyo Mtikila alimwomba Rais Kikwete, asisahau kumjumuisha kwenye Tume atakayoiunda kwa kuzingatia kuwa ametumia muda mwingi kudai Katiba mpya ya nchi akiwa na dhamira ya dhati.

Huyu naye! Mtu mzima hovyooooo...Si bora anyamaze tu kama hana cha muhimu cha kuongea badala ya kukurupuka na kuishutumu CHADEMA kwa tuhuma ambazo hazina kichwa wala miguu!?

mtikila ni fisadi hastahili kabisa kuwepo katika Tume ya Katiba. Kama mtakumbuka alishawahi kuumbuliwa na Rostom Aziz kuwa naye Mtikila huenda kuchukua hela ya ufisadi toka kwa RA, na hadi leo hajapinga! Mchungaji haaminiki bora apotezewe tu

Actually alikiri kuwa Rostam alimpa zile pesa kama rafiki yake.
 
Kama Wananchi Hatumuelewi Mtikila Nani Anamwelewa? Mtikila Tutafurahi Kama Mwanasiasa Ungechukua Retirement Mapema. Hakuna Haja ya Nani Kaja na Ideas kwa Mara ya Kwanza, Inaonekana Mtikila Anataka Credit na Chadema Mpeni Kama Anataka ili Akampumzike. Lengo Kubwa Siku Zote ni Kuleta Usawa na Maendeleo kwa TAIFA Letu.
 
Vongozi wengine bwana sasa kama alianzisha yeye kwanini asiungane na wanaodai katiba mpya leo? Kama anataka nae ajumuhishwe kwenye tume hiyo kwanini aseme katiba hiyo ni kwa manufaa ya Chadema? Sasa akiwemo humo itakuwa manufaa ya nani?

Huyu Mzee sijui huwa anawaza nini kweli akili zikizidi huwa zinapitiliza
 
Msimlaumu kama tetesi ninazosikia ni kweli huyu 'Mchungaji' alikuwa mesenja shirika moja la ndege, hivyo kuna mgogoro kwenye upeo.
 
"Hata hivyo Mtikila alimwomba Rais Kikwete, asisahau kumjumuisha kwenye Tume atakayoiunda kwa kuzingatia kuwa ametumia muda mwingi kudai Katiba mpya ya nchi akiwa na dhamira ya dhati."

Marekebisho ya Katiba huamuliwa na wananchi wote na si tume au kikundi cha watu wachache!
 
Kinachofanywa na JK ni kuzima hoja hii maana Watanzania ni wasaulifu tutasahau kesho tu kwani nijuzi tu tuliibiwa kura sasa tumesahau na sasa hivi mambo kama ya EPA na ufisadi mwingine tunaendelea kusahau.
Swala la kuunda tume sina Inamani nalo na itafika 2015 bado tunaangaliana Watanzania na kuulizana Katiba ipo wapi?
 
we Mzee sikia.
Ulishaambiwa ya Kaisari mpeni kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.
Sasa ya huku tuachie wa Kaisari, we endelea na upande huo huko.
Injili Siasa pamoja ni sawa mafuta na maji, ukijaribu kuchanganya wala havichanganyikani
 
Tatizo la Mtikila ni kuwa yeye anajiona anajua saana kila kitu. Mtikila ana hulka ya udikteta na ndiyo maana hata chama chake kimedumaa. Tatizo lingine la Mtikila ni wivu hataki kuona mtu mwingine anapata mafanikio. Mwaka 1995 Mrema alivyotoka CCM na kuingia NCCR ni Mtikila huyu huyu aliyesimama kidete kumshambualia Mrema na NCCR mpaka akatengeneza kanda za kuibomoa NCCR na Mrema mradi ambao uliinufaisha CCM kuliko yeye na chama chake.Kwa hili la katiba nilitegemea Mtikila aipongeze Chadema kwa kuipeleka hoja hii katika viwango vya kuweza kutekelezeka, lakini yeye anawaponda, haya ni makengeza ya akili. Siku zote kazi anayoifanya Mtikila kushambulia wapinzani inainufaisha CCM sasa sijui kama yuko kwenye payroll ya CCM au vipi.Mtikila anahitaji afanyiwe maombi maaluma ya kufunguliwa(deliverance) vinginevyo ataishia kuokota makopo.
 
jamani tuwe na focus kwenye objective,haya mambo ya kuanza ku-deal na individuals yanapoteza muda na lengo.he is playing his game,muacheni mapambano ya katiba yaendelee.
 
Kila kitu kina mwanzo wake. Kinaweza kuanza kama wazo la mtu moja au kikundi cha watu fulani na kikapokelewa vizuri tu kama kipo kwa masilahi wa wengi. Bila kujali nani alikuwa wa kwanza kuanzisha hoja ya kupatikana KATIBA mpya,jambo lililopo mbele yetu watanzania hasa wanaoipenda nchi yao ni kushiriki kwa ukamilifu katika kufanikisha kupatikana katiba mpya .
 
Mchungaji mtikila ni mtu asiyetabirika na mara zote anaangalia namna ya kupata maslahi kutokana na hoja mbalimbali. Ameanzisha hoja nyingi sana nchini kuanzia Magabachori hadi wazawa lakini hazina nguvu wala mishiko sahihi kwa wachambuzi wa mambo. Huwa anaanza vizuri lakini anakorofisha mahali fulani huko njiani kabla ya kufika. Akiwa kama mtanzania anayo haki ya kuchangia uundaji wa katiba mpya lakini si mtu wa kumwamini kuwa ana nia ya dhati ya kusaidia watanzania. Tarime walimpiga mawe kwa usaliti wake!!!

Tatizo ni ndumilakuwili na anapenda kujinufaisha tumbo hao magabachori walimkatia chache na kumjengea nyumba akakaa kimya, alitumiwa na mafisadi mpaka wakaja kumuumbua kwa chaki alizokuwa wanamlipia hela, alitumika kisiasa kwenye uchaguzi mdogo Tarime na kulipwa na CCM. Huyu jamaa hafai na hatifai hata kidogo wala kumfikiria kuwepo kwenye kama zitakahusuka na mchakato wowote wa katiba. Atoe na kuchangia mawazo tu
 
Mtikila ni yule yule;Jana,leo na kesho.
Amekuwa hivyo, atakuwa hivyo hivyo kwa mazuri na mabaya. hawezi kubadilika milele.

Hapo Mwanzo alikuwa mpiganaji aliyesikika lakini hakuungwa mkono. Inawezekana hakuwa na mbinu bora kuwaelimisha watanzania wa kipindi kile

Bila kujua kama kuna watu wameanza kuelewa na kuona mbali yeye akawa bado anadhani watu wako usingizini akashiriki na mafisadi kwa mtego wa checque ya mil3. Akavuta na kurudi tena kwetu. Sema kweli hakuna kitu kibaya kama kuchezea akili watu, Watu wanamdefine the way wanaona iwe, hiyo ndiyo historia yake ilivyo na ndivyo itakavyokuwa.

Mchungaji anaona kuwa ameporwa hoja, kwa sababu anaamini kuwa ni yake. Yawezekana ndiyo maana alishindwa kuipaisha mioyoni mwetu. CDM wamekuja na NGUVU YA UMMA wakiamini kuwa hoja hii ni ya Umma, katiba si suala la mtu binafsi. Ni suala la kitaifa kwa watanzania wote.Ndiyo maana imekuwa Hot

Movement ilianzia Bungeni, Kususia kile Kikao kilichohusisha hotuba ya yule Mtalii,Tangazo rasmi la CDM kwa Nchi lilitoka kuwa Katiba mpya ndiyo kipaumbele. Mwacheni naye atoe yake. mazuri tuyachukue, yaliyochakachuliwa tuyaache.

Mtikila ni yule yule: Tunamfahamu vizuri mwanzo mwisho.:ranger:
 
Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila amesema Chadema ilikurupuka na kudandia hoja ya Katiba mpya ya nchi bila kuzingatia maslahi ya Watanzania na kuonya kuwa mchakato wa kuunda Katiba unaweza kushindwa kama utafanywa kwa lengo la kukidhi matakwa ya watu wachache wanaoshinikizwa na wageni.

Akizungumza kwa simu jana, Mtikila alisema si viongozi wa Chadema wenye dhamira ya dhati ya uundaji wa Katiba mpya kwa maslahi ya Watanzania, kwa kuwa wanataka Katiba iundwe, kwa maslahi binafsi kwa lengo la kuendeleza zama za ukoloni.

“Mimi nilipojaribu kuzungumzia Katiba mpya na haja ya kuwa na Serikali tatu, watu waliniona kichaa, jambo ambalo lilisababisha kampeni ya kutaka Katiba kuwa ngumu na isiyo na mafanikio … sasa watu hao hao wanataka Katiba mpya kwa maslahi yao,” alisema.

Hata hivyo Mtikila alimwomba Rais Kikwete, asisahau kumjumuisha kwenye Tume atakayoiunda kwa kuzingatia kuwa ametumia muda mwingi kudai Katiba mpya ya nchi akiwa na dhamira ya dhati.

nimependa maneno yake mwishooo....................katiba mpaka kieleweke
 
Back
Top Bottom