Kauli ya Luhanjo: Sheria ya kuwalinda watoa taarifa za ufisadi iko wapi? TAKUKURU mpo?

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
275
Wana JF,

Juzi wakati Katibu mkuu kiongozi akimrudisha Jairo kazini alimalizia kwa kusema kuwa sasa serikali inajikita kumtafuta aliyetoa barua kwa wabunge na kumtaka Jairo afungue kesi ya kudhalilishwa kwa waliomsema (kwa fikira zangu mama Shelukindo). Kwa maoni yangu ni kuwa Luhanjo anamtishia mtoa taarifa.

Ninakumbuka wakati wa kupitishwa kwa sheria mpya ya kupambana na kuzuia rushwa, hili suala la kumlinda mtoa taarifa lilizungumzwa sana. Je, Shera zetu zinasemaje kuhusu usalama wa mtoa taarifa? Je kauli ya Luhanjo si kosa la jinai?

Naomba maelezo toka kwa wanasheria, na wale wote wanaochukia ufisadi.
 
Mimi naamini kabisa kuwa sasa ni wakati muafaka kwa Luhanjo kupumzika nyumbani aendeleze miradi yake ya shule kule Tegeta; kwani inaelekea the guy is now senile!! How can Jairo sue a member of parliament for defamation kwa kitu alichosema bungeni? Dosn't Luhanjo know that members of parliament are immune from prosecution for anything they utter within the bunge compound? As a Chief Secretary, he should know more than this.
 
Luhanjo wala asipoteze muda, kaanze na Januari Makamba atapata ukweliw a bbarua ilitokaje
 
Back
Top Bottom