Kauli ya ki-hujuma iliyotolewa na CHADEMA dhidi ya CUF

Cuf (ccm-b) bara watangaze rasmi kwa umma kuikana cuf (ccm-b) visiwani kuwa hawana ushirika nao na wachague viongozi wao wapya wakifanya haya tutawaonea huruma kidogo tunajua wananjaa tu cuf hawana uwezo wala sifa ya kutetea watz kwani walisha kosa sifa ya kuwa wapinzani kwa kuamua kuwa taaisis ya kiislamu kwa ajili ya matakwa ya kiislamu............
 
Mi hata sipati picha hawa ccm b wanamaanisha nini?Mtatiro politics is about conviencing and if you cant convience him/her confuse him/her.Mi naona Chadema muwaache tu mana hamjawashawishi huo upuuzi na kumbukeni ilani yenu ni kuwatumikia wananchi na siyo kulazimisha ndoa na kila mwanaume.Chadema hawataki basi kwani lazima?Mtatiro umeproove we bado mchanga sana kwenye siasa.
 
hivi katibu mkuu wa kafu yupo wapi ili tumpe na yeye kamati au kiongozi ya kambi ya upinzani bungeni?au ni ule usemi ukisikia kimya ujue kashiba .
 
MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA KAULI YA KI-HUJUMA ILIYOTOLEWA NA CHADEMA DHIDI YA CUF.




Jumatano, 02 FEBRUARI 2011, 1100hrs, DAR ES SALAAM

Ndugu waandishi wa habari,

Chama cha wananchi CUF kimesikitishwa sana na kauli iliyotolewa na CHADEMA siku ya jumatatu tarehe 31 Januari 2011 kupitia kwa katibu mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa kuwa "CUF siyo chama cha upinzani Tanzania tena eti kwa sababu kiko serikalini Zanzibar" na kwa hiyo CHADEMA hawawezi kushirikiana na CUF katika kuunda kambi ya pamoja bungeni.

Tunapenda kuwataarifu watanzania wote kuwa sisi pia hatuwezi "KUWALAMBA MIGUU" viongozi wa CHADEMA kwani hakuna faida yoyote wala umuhimu ambao wao wameonesha kwetu tangu tulipojaribu kila namna kuwafanya wafanye kazi kwa umoja na vyama vingine na kugonga ukuta.

Mara zote CHADEMA wamekuwa na historia ya kuvisaliti vyama vingine vya upinzani huku wakikimbilia kwa umma kuomba waungwe mkono wao peke yao. Mwaka 2007 CUF iliongoza UANZISHWAJI wa USHIRIKIANO WA VYAMA VINNE VYA UPINZANI Tanzania. Vyama vilivyosaini ushirikiano huo mbele ya vyombo vya habari ni pamoja CUF, CHADEMA, NCCR na TLP.

Ndugu waandishi wa habari,
Moja kati ya masharti makubwa ya ushirikiano huo ilikuwa ni kuhakikisha kuwa vyama hivi vinne vinakiunga mkono chama chenye nguvu mahali fulani kila unapotokea uchaguzi wowote mahali hapo ili kuhakikisha kuwa upinzani unakuwa na wabunge wengi watakaopigania maslahi ya Watanzania.
a) Ulipotokea uchaguzi wa marudio Jimbo la Tunduru ambako ni ngome ya CUF, vyama vya NCCR na TLP walijitokeza kuisaidia CUF kushinda jimbo hilo lakini Chadema walijifanya POPO wakasaliti makubaliano waliyoyaweka na vyama vingine wakapeleka mgombea TUNDURU ambako hawana tawi wala serikali ya mtaa wakaishia kupata kura chache mno huku JIMBO LIKIENDA CCM.
b) Ulipotokea uchaguzi mdogo wa Kiteto CUF kwa sababu tunajua nini maana ya ukombozi,tulisahau dhambi waliyotufanyia chama popo(Chadema) katika jimbo la Tunduru,pamoja na sisi kuwa na madiwani Kiteto tuliamini Chadema wangeweza kufanya vizuri sana katika jimbo hilo kuliko CUF hivyo tukaenda kuwaunga mkono,tukamtuma Mjumbe wa Baraza kuu la Uongozi Taifa Mhe. Masoud (MB) pamoja na watendaji wawili kwenda kuwasaidia Chadema katika kampeni zao,tukapigana kufa na kupona pamoja nao japo baada ya kura CCM walishinda.
c) Ulipokuja uchaguzi mdogo wa Tarime, pamoja na CUF kuwa na wafuasi wengi Tarime tukaahidi kulinda heshima ya marehemu Chacha Wangwe(tunamheshimu sana) tukaamua kutofautiana na viongozi wetu wa wilaya waliolazimisha tuweke mgombea kutokana na Chadema kugawanyika lakini CHAMA TAIFA tukasema ni muhimu tuwaache Chadema kwa mujibu wa makubaliano ya vyama vyetu na pia kwa kumuenzi marehemu ambaye alikuwa mbunge wa Chadema. CUF taifa ikamtuma Mjumbe wa Baraza kuu la Uongozi Taifa Mhe. Karume Mgunda(Katibu wa CUF wilaya ya Rorya ambaye kwa sasa yuko gerezani kwa kesi ya kubambikiziwa) na kuwataka viongozi wa wilaya watoe ushirikiano kwa Chadema na Mhe Karume akawekwa katika watu muhimu waliokuwa wakimnadi Mhe CHARLES MWERA katika timu ya Kampeni ya chadema na akawasaidia kufa na kupona hadi jimbo la TARIME likabaki upinzani.
d) Uchaguzi mdogo wa Mbeya vijijini ndio ulizidi kutujulisha kuwa Chadema wanacheza karata zao za siri dhidi ya CUF, pamoja na kutokuwa na mtandao wowote katika jimbo husika chadema waling'ang'ana kuweka mgombea pamoja na kujua CUF ndiyo yenye NGUVU Mbeya vijijini, vyama vyote vikaweka wagombea ambapo mgombea wa chadema alikosea kujaza fomu na hivyo akawekewa pingamizi kutoka kwa mgombea wa ccm na Yule wa CUF. Baada ya kuenguliwa mgombea wa chadema walitangaza kuvunja ushirikiano na CUF(ambao waliuhitaji ili kuinufaisha chadema tu) na kisha wakaweka kambi mbeya vijijini na kuwasihi wapiga kura bora waichague ccm kuliko CUF, na matokeo ya hila na ghilba zao, wapiga kura hawakuichagua CUF.
e) Ulipotokea uchaguzi wa Busanda CUF ilihujumiwa na haikuwa na mawakala vituoni hivyo Chadema wakaitumia fursa hiyo kujihami na kuomba wapigiwe kura za CUF jambo ambalo walifanikiwa japo jimbo lilichukuliwa na CCM.

Ndugu waandishi wa habari,
Pamoja na UNDUMILAKUWILI wote huo wa Chadema, pamoja na kutangaza kuvunja uhusiano na CUF bado walipita kila kona ya nchi kuwarubuni viongozi wa CUF wasisite kuungana nao katika ngazi za chini na walifanikiwa kuwanasa baadhi ya viongozi wetu kwa kutumia kila njia hata kama ni kuwapa fedha na zawadi.

Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 CUF imepata wabunge wawili wa kuchaguliwa Tanganyika na wabunge 22 wa kuchaguliwa Zanzibar ambapo ukijumlisha wa kuchaguliwa na viti maalum 10 CUF inakuwa na jula ya wabunge 34 katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Pamoja na kuwa na wabunge 34, kikanuni CUF haiwezi kuunda kambi ya upinzani bungeni, ni chadema ndiyo wenye uwezo huo. Mwishoni mwa mwaka jana CUF iliiomba Chadema iweze kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ili kuwa na kambi ya upinzani imara zaidi na yenye nguvu, chadema walikataa kabisa suala hili kwa maelezo kuwa "wao chadema wako tayari kuungana na CUF tu katika kambi ya upinzani na kuwa hawaviamini vyama vya NCCR,TLP na UDP". Na maelezo haya yariripotiwa na vyombo vya habari.

Ndugu waandishi wa habari,
Pamoja na msimamo huo wa chadema bado CUF tuliwasihi Chadema waweze kushirikisha vyama vyote kama ilivyokuwa ikifanya CUF wakati ilipokuwa ikiongoza upinzani bungeni ili kuwa na upinzani imara zaidi. Chadema walikataa kwa msisitizo na walituomba CUF ijiunge katika kambi yao(chadema) bila vyama vingine, tulipolitafakari suala hili sisi CUF kama chama kisichotaka kuchezea akili za watanzania tuliona hakuna maana ya kuwatenga vyama vingine kwa sababu dhaifu ya kushangilia ugomvi uliopo kati ya mwenyekiti wa Nccr aliyewashtaki Chadema mahakamani hivi karibuni kwani tunaamini "UMOJA NI NGUVU na UTENGANO NI UDHAIFU" .

Kutokana na hali hiyo iliwabidi wabunge wa CUF na NCCR wawaandikie Chadema kuwaomba wahusishe vyama vingine katika kambi yao na Chadema walikaa kimya bila kujibu chochote.

Baada ya kuona Chadema wana masharti magumu sana katika kuruhusu vyama vingine vya upinzani kujiunga kwenye kambi rasmi ya upinzani ambayo wao ndiyo wana nguvu ya kuiunda kikanuni, wabunge wa CUF na wale wa NCCR waliomba wawe na kambi ndogo ya upinzani ili waiache Chadema ifaidi "matunda ya kumiliki kambi ya upinzani" jambo ambalo Spika wa bunge alieleza halitawezekana.

Ndugu waandishi wa habari,
Baada ya yote hayo ndiyo jana Chadema wametoa kauli ya "KINAFIKI" eti wao hawawezi kushirikiana na chama kinachoongoza dola,yaani CUF na kuwa wao Chadema wako tayari kushirikiana na Nccr na kina Kafulila "sisimizi" , Juzi Nccr ndio walikuwa kikwazo kwa Chadema kushirikiana na vyama vingine, hata mwezi haujapita Chadema wamegeuka eti leo CUF ndiyo adui, "Chadema ni chama popo sana", hawajui wanachofanya,wamelewa madaraka na kuchanganyikiwa vibaya baada ya kupata majimbo 20 Tanganyika, sasa hawana haja na CUF na vyama vingine,wanadhani majimbo 20 ndio Ukombozi wa Tanzania umemalizika. "Ni sawasawa na masikini sana anayeamka ghafla anajikuta tajiri,hajui namna gani atatumia utajiri wake,anaanza kuwatukana majirani zake alioishi nao kwa shida na raha katika umasikini wao,anawatukana majirani huku anaendelea kuponda mali na wasichana warembo katika kijiji hichohicho,siku moja mali zinaisha……hadithi ya tajiri mjinga inaishia hapo."

CHADEMA wanaishambulia sana CUF hivi sasa, wanataka kuwaaminisha watanzania kuwa kitendo cha CUF kuwa katika serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ni dhambi kubwa mno na kuwa Watanzania wasiiunge mkono CUF Tanzania bara jambo ambalo ni ndoto za alinacha na kamwe halitatokea kwani watanzania wa sasa hawadanganywi kwa propaganda zisizo na maana.

Ndugu waandishi wa habari,
Chadema wanafanya hivi kimakusudi kwani wanaamini kama CUF ikifa bara wao watapumua mno, Chadema wamekuwa waoga mno,wanaiogopa CUF, wanajua CUF kina mtandao mkubwa na kina mbinu ya kujiimarisha bara na hatimaye kuongoza nchi, Chadema hawataki hili litokee,wanasali na kuomba na kufanya kafara ili CUF ife bara lakini tunawaambia wasubiri CUF ife na wao watakufa na kuiacha CUF.

Kitendo cha chama cha siasa kuwadharau Wazanzibari, kudharau maamuzi ya wananchi wa Zanzibar katika nchi yao, kudharau katiba ya Zanzibar ni kitendo cha "kijinga mno" ni sawa na "kitendo cha Padre kuvua joho, kukiuka kiapo na kukimbilia kula raha na wachumba"

Wazanzibar ndio walioamua kwa kupiga kura kuwa wanahitaji serikali yao, ya umoja wa kitaifa

Leo ni mwendawazimu yupi anakuja kudai ati CUF kuwa katika mfumo wa serikali iliyoamuliwa na wananchi katika upande mmoja wa nchi ni dhambi? Hivi Chadema ni muhimu kuliko wazanzibari? Hivi wakati makumi ya wananchi walipokuwa wakiuawa katika kila chaguzi za Zanzibar Dr Slaa na Chadema waliwahi kwenda kukinga mapanga na silaha za uchaguzi zisiwakate?

Wazanzibari wameamua serikali wanayoitaka, wamefanya uchaguzi wa amani, wanaendelea kuishi kwa amani; na siku wakiichoka serikali yao wataiondoa na kuamua nyingine wanayoitaka,wao ndio wana mamlaka juu ya serikali yao.

kwa maslahi ya nchi yao ya Zanzibar kwa kujali amani maendeleo na ustawi wa taifa lao. Wazanzibari ndio walioamua kuwa chama kitakachoongoza katika uchaguzi kitatoa rais na mawaziri na cha pili kitatoa pia makamu wa kwanza wa rais na mawaziri. Wakapiga kura, wakatoa maamuzi haya, wakayaingiza katika katiba yao ya Zanzibar katika mabadiliko ya 10 ya katiba. Ndugu waandishi wa habari,
Hivi tujiulize, siku watanzania(bara) wakipiga kura wakasema wanataka serikali itakayoshirikisha vyama vyote vya siasa, Chadema itahama nchi au itabakia na kushiriki katika serikali ili kufuata matakwa ya wananchi? Hii dhana ya Chadema kuwa, chama cha siasa kina nguvu kuzidi maamuzi ya wananchi wameitoa wapi?

Ina maana Chadema iko juu ya wananchi? Je walitaka CUF ilipopata nafasi ya pili Zanzibar ikiuke matakwa ya wananchi na kukataa kuingia serikalini ili CUF iwafurahishe Chadema ambao Zanzibar hawana hata mjumbe wa mtaa wala tawi?

Nani asiyejua kuwa Zanzibar ni nchi na kuwa iko katika muungano na Tanganyika katika kuitengeneza Tanzania? Nani asiyejua kuwa CUF ni chama chenye nguvu na mtandao Zanzibar na Tanganyika na ni chama cha pekee cha upinzani chenye wabunge kutoka pande zote za muungano? Nani asiyejua kuwa Chadema ni chama kilichoko Tanganyika peke yake? Nani asiyejua kuwa Chadema kinaumizwa sana na mafanikio na utulivu wa kisiasa Zanzibar yaliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na busara na viongozi wa CUF ambao hawakuweka maslahi ya chama mbele katika kulinda uhai na maisha ya wazanzibar?

Ndugu waandishi wa habari,
Tunatambua kuwa Chadema na Dr Slaa wangependa sana kuona CUF inakataa matakwa ya wananchi ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili machafuko yatokee Zanzibar, tunajua CHADEMA na Dr Slaa wangependa kuona historia za mauaji wakati wa uchaguzi zinajirudia Zanzibar kwani hawana wafuasi na wanachama huko. Chadema hawana nia ya dhati na Zanzibar.

"CUF tunaamini Chadema wamewadharau wazanzibari,wanawaona hawana maana,wanadharau maamuzi yao,wanaona hawawezi kufikiri na kujiamulia mambo yao wenyewe,hilo hatunalo shaka".

Sisi kama chama chenye nguvu kubwa kabisa Zanzibar tutazidi kuheshimu maamuzi ya wananchi walio wengi kila mara bila kujali kama Chadema watakasirika au la, CUF haipo ili kuitumikia Chadema na kufuata matakwa ya yao. Tupo ili kuwatumikia watanzania,kuwatetea katika madhila yote na manyanyaso wanayofanyiwa.

Tutaendelea kuwa katika serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar na kulinda maamuzi na matakwa ya wananchi wa Zanzibar lakini kwa upande wa Tanzania bara ambako katiba iko wazi,kuna chama kimoja kinachoongoza dola na vingine vyote vikiwa vyama vya upinzani, tutaendelea kuheshimu matakwa ya kikatiba yaliyopo Tanzania bara.

Ndugu waandishi wa habari,
"CUF tutaendelea kubeba matumaini ya watanzania, tutawatetea sana katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na chama chochote chenye malengo mazuri na ukuaji wa kambi ya upinzani Tanzania, tutawatetea watanzania bungeni na kokote bila woga na kwa nguvu zote bila kuwalamba miguu Chadema tukiwa nje ya kambi rasmi ya upinzani na kamwe hatutowasaliti watanzania".

Tutazidi kuwa chama cha kitaifa kwa kuzidi kupata wabunge wengi kutoka Bara na Zanzibar ,tutazidi kujiimarisha pande zote za nchi hadi tuione Tanzania njema "inayosubiriwa na watanzania wote". Chadema na watu wote wanaoitakia mabaya CUF watakufa na kukiacha chama hiki kikishamiri kama tegemeo la pekee la watanzania.

MUNGU IBARIKI AFRIKA,
MUNGU IBARIKI TANZANIA,
"HAKI SAWA KWA WOTE".
Imetolewa na;
Julius Mtatiro
Kaimu Naibu Katibu Mkuu(CUF) –Bara

Angalia hiyo red. Hili ndio tatizo la cuf, wameshindwa kujizuia hadi wamelitamka hadharani.
Ni sawasawa na mtu aliyeua, huwa anaweweseka hadi anajitaja kuwa ameua bila ya yeye mwenyewe kujijua kuwa amejitaja.

Cuf wanatakiwa wajiulize; pamoja na matamko yote hayo ya kuichafua chadema (ukijumlisha na yale ya waislamu), mbona watu hawawasikilizi? Hii ina maana kuwa wamedharaulika. Watanzania wa leo hawadanganyiki kama wao wenyewe cuf walivyotanabaisha kwenye hilo tamko lao.

ENDELEA KUTAPATAPA MTATIRO, CHADEMA TUNA WATU VERY POTENTIAL, WEWE HUNA SIFA HIYO. BAKI HUKO HUKO WAISLAMU WAENDELEE KUKUTUMIA. POLE SANA KIJANA UMEUVAA MKENGE.
 
Angalia hiyo red. Hili ndio tatizo la cuf, wameshindwa kujizuia hadi wamelitamka hadharani.
Ni sawasawa na mtu aliyeua, huwa anaweweseka hadi anajitaja kuwa ameua bila ya yeye mwenyewe kujijua kuwa amejitaja.

Cuf wanatakiwa wajiulize; pamoja na matamko yote hayo ya kuichafua chadema (ukijumlisha na yale ya waislamu), mbona watu hawawasikilizi? Hii ina maana kuwa wamedharaulika. Watanzania wa leo hawadanganyiki kama wao wenyewe cuf walivyotanabaisha kwenye hilo tamko lao.

ENDELEA KUTAPATAPA MTATIRO, CHADEMA TUNA WATU VERY POTENTIAL, WEWE HUNA SIFA HIYO. BAKI HUKO HUKO WAISLAMU WAENDELEE KUKUTUMIA. POLE SANA KIJANA UMEUVAA MKENGE.

Kina nani hawasikilizi? JF? au

Waislamu wanaingiaje hapa?
 
Inasikitisha kiongozi mkubwa wa chama kutoa kauli mbovu kama hii. Je inatusadikisha kuwa CUF hakina wasomi wenye upeo? Mtatiro anazidi kujimaliza hata kwa sie wachache tuliokuwa tukimtumaini kumbe nae ni kama wana CUf wengine. ila ni msomi what is wrong with hi?? Pengine tukitazame chama cha CUF kwa undani huende kina matatizo makubwa kuliko tunavyojua.... Wanasikitisha sana
 
Inasikitisha kiongozi mkubwa wa chama kutoa kauli mbovu kama hii. Je inatusadikisha kuwa CUF hakina wasomi wenye upeo? Mtatiro anazidi kujimaliza hata kwa sie wachache tuliokuwa tukimtumaini kumbe nae ni kama wana CUf wengine. ila ni msomi what is wrong with hi?? Pengine tukitazame chama cha CUF kwa undani huende kina matatizo makubwa kuliko tunavyojua.... Wanasikitisha sana

Jiangalie wewe kwanza kiundani unasema haaya kwa akili yako au umechanganya na ushabiki uliokuathiri akili yako

Kujiangalia inatakiwa iwe pande zote chadema na cuf?
 
Back
Top Bottom