Kauli ya JK Kuipongeza Marekani kufuatia kifo cha Osama yaja?

Usisahau kuwa ugaiidi wa siku za nyuma iulikuwa ni wa maslahi zaidi kuliko religious ideology. Osama ndiye ameingiza hili akitaka kuungwa mkono na kwa bahati mbaya tunaona mnavyomuunga mkono hata kwenye udhalimu usio na chembe za imani.

Kwa nini unanihusisha na wanaomuunga mkono Osama? Nini kimekufanya unihusishe na huyo muuaji? Kama maswali yangu yamekufanya unidhanie hivyo utakuwa umekosea sana.

Kama aliyekumbwa ni baba au mama yako, kaka au dada usingetamka haya.
Mimi nimeona nikiwa kazini Aug 1998, nimesikia kishindo na nimebeba majeruhi ndani ya hospitali. Inaniwia vigumu na napata uchungu sana kwa maneno yako. Ungemuona yule bibi aliyekuja kuchukua maiti ya kijana wake au yule mama aliyeaachwa na watoto mayatima, neno bahati mbaya ungeliona tusi.

Unanihukumu kimakosa sana. Maneno yangu yepi hayo yanayokupa uchungu? Daaah haya bana.
 
................What is so special to Osama when comes a question of justice, while we know thousands have been denied the same!.............

Hili ni swali ambalo walio wengi........huwa wanajifanya hawalioni
 
Kwa nini unanihusisha na wanaomuunga mkono Osama? Nini kimekufanya unihusishe na huyo muuaji? Kama maswali yangu yamekufanya unidhanie hivyo utakuwa umekosea sana.
Unanihukumu kimakosa sana. Maneno yangu yepi hayo yanayokupa uchungu? Daaah haya bana.

Nyani Ngabu,
Ninaposema kuunga mkono nina maana ya hisia za yeye kutofikishwa mahakamani. OBL alitumia 'rule of the jungle' na wala hukujihusisha na kitu kinachoitwa 'justice'. Amesababisha maafa kwa watu wake na kila kona ya dunia.Hakuwahi kutumia sheria pale alipotoa adhabu hata kwa wale waliokuwa katika himaya yake. Kwanini watu wadhani hakutendewa haki ili hali yeye hakutoa?

Maneno yanayonitia uchungu ni 'sisi wengine tutakumbwa kwa bahati mbaya'. Kama nilivyosema huko nyuma, Aug 1998 nilihudumia wahanga wa mabomu. Zaidi ya hayo nilishuhudia ndugu jamaa na marafiki wakilia na kutoa kauli zilizoniliza. Watu wale sikuwajua, lakini nilivyokuwa nawasikia wakitweta, kauli zao, simanzi na majonzi nililia. Ni kitu ambacho mtu hawezi kuthubutu kukiita 'bahati mbaya!

Leo watu hawaogopi mechanical failure ya vitu kama ndege bali maovu ya OBL. Kama alikuwa na justification za vita angepigana na wahusika, lakini kumuua mlinzi au mpitia njia, msafiri n.k haitoshi kusema ni 'bahati mbaya'. Mtu anapanga kulipua ndege yenye watu 500 ili kuua wabaya wake 10, hii ni bahati mbaya kweli?

Neno bahati mbaya kwa wale waliofikwa na mabalaa ubalozini kenya, Dar, sept 11, London 7/7 achilia mbali afghanistan, Iraq n.k halikubaliki hata kidogo. Dunia imejaa hofu na dhalili kwa sababu ya huyu bwana. Nimewahi kushuhudia msafiri mmoja mashariki ya kati akipekulia vema kwasababu umbile lake nyeti lilionekana kuzidi kiwango na kujenga hofu kama amebeba zana za mauaji.
Tunaposema 'kukumbwa kwa bahati mbaya' ni njia laini ya kuhalalisha uovu na hapo ndipo hisia ya kile nilichokiona ikirudi kwa kasi ndani ya fikra zangu na kuamsha uchungu.
 
SlidingRoof;1928755]Kama taifa tunajivunia utawala wa sheria na kwa hili sidhani kama it was right kuunga mkono U.S Govt kwenye hii unlawful killing of Osama Bin Laden
Not true Sir! Obama has opposed the water boarding before he walked in to 1600 Pen ave. It is in the record, that’s why the first executive order he signed was to shut down Gtimo to pave a way for judicial proceeding.
Yesterday on the briefing of congress the CIA director hinted that initial information was obtained in 2003 when Khalil sheikh Mohamed was subjected to water boarding, however the info was inconclusive and needed other pieces to complete the puzzle. The Rep King (Republican) hyped the info as sole means which led the mission to success, just to score the political point. FYI security is an agenda to Republican; unfortunate Obama seems to pre empty them.It is now clear that, better intelligence community, additional of resources were the tools for success.
Just because Americans did it does not mean kuwa its right. InfactThe theoretical restraint on extra-judicial murder/execution is in theory based on international law ambayo sisi kama taifa tumetia saini sasa iweje leo tukawafuata hawa jamaa blindly kuunga mkono uhuni kama aliyofanyiwa Osama.
That is the rule of the jungle. Tit for tat, again did OBL exercised your doctrine?
Binafsi niko tayari ku engage with anyone on this kwa sababu naamini strict adherence to international law is of the utmost critical importance and is what separates us from the animals, including freepers.
So where do you put OBL, in human or animal category before we embark into more discussion
Tusiwe na Slave mentality na inferiority complex za kufikiri kuwa everything Americans does are right
Yes, but we should not hate them when they do what is right for their country and world in general.
Look here, thousands have been murdered by OBL, no one was subjected to the rule of the law, the number includes his own liutenants killed by air drone. What is so special to OBL to spark the uproar.

 
Nyani Ngabu,
Ninaposema kuunga mkono nina maana ya hisia za yeye kutofikishwa mahakamani. OBL alitumia 'rule of the jungle' na wala hukujihusisha na kitu kinachoitwa 'justice'. Amesababisha maafa kwa watu wake na kila kona ya dunia.Hakuwahi kutumia sheria pale alipotoa adhabu hata kwa wale waliokuwa katika himaya yake. Kwanini watu wadhani hakutendewa haki ili hali yeye hakutoa?

Maneno yanayonitia uchungu ni 'sisi wengine tutakumbwa kwa bahati mbaya'. Kama nilivyosema huko nyuma, Aug 1998 nilihudumia wahanga wa mabomu. Zaidi ya hayo nilishuhudia ndugu jamaa na marafiki wakilia na kutoa kauli zilizoniliza. Watu wale sikuwajua, lakini nilivyokuwa nawasikia wakitweta, kauli zao, simanzi na majonzi nililia. Ni kitu ambacho mtu hawezi kuthubutu kukiita 'bahati mbaya!

Leo watu hawaogopi mechanical failure ya vitu kama ndege bali maovu ya OBL. Kama alikuwa na justification za vita angepigana na wahusika, lakini kumuua mlinzi au mpitia njia, msafiri n.k haitoshi kusema ni 'bahati mbaya'. Mtu anapanga kulipua ndege yenye watu 500 ili kuua wabaya wake 10, hii ni bahati mbaya kweli?

Neno bahati mbaya kwa wale waliofikwa na mabalaa ubalozini kenya, Dar, sept 11, London 7/7 achilia mbali afghanistan, Iraq n.k halikubaliki hata kidogo. Dunia imejaa hofu na dhalili kwa sababu ya huyu bwana. Nimewahi kushuhudia msafiri mmoja mashariki ya kati akipekulia vema kwasababu umbile lake nyeti lilionekana kuzidi kiwango na kujenga hofu kama amebeba zana za mauaji.
Tunaposema 'kukumbwa kwa bahati mbaya' ni njia laini ya kuhalalisha uovu na hapo ndipo hisia ya kile nilichokiona ikirudi kwa kasi ndani ya fikra zangu na kuamsha uchungu.


tonachotofautiana ni kitu kifuatacho wewe unaamini Osama katenda hayo aliyoyatenda na kwa hiyo anastahiki hukumu hii iliyomfika, lakini hujiulizi swali, je ni kweli katenda hayo wanayomtuhumu nayo?. Utajuaje kwamba vidhibiti vyote na ushahidi wote waliokuwa nao ikiwemo hizo video zake ni vya kweli kama humfikishi mbele ya vyombo vya sheria?. maana mahakama ndo hudhibitsha ushahidi au huukataa

kama tukifuata logic hii ya kwako, basi kuna watu na mataifa wana ushahidi wa kutosha wa Joji Bushi kuua raia wasio na hatia huko iraq, nao wanaweza kujipa sheria mkononi, kisha wakautangazia ulimwengu kwamba haki imetendeka.

au wengine watawakamata wauza viungo vya albino hatari na kuwaua bila kuwafikisha mahakamani , kisha watatangaza haki imetendeka.

Hatari ninyoiona katika lojiki ya Mwanakijiji ya kwamba magaidi wajisalimishe, kisha waende mahakamani ili kujisafisha dhidi ya accusation zinazowakabili, ni katika kujaribu kuonyesha kwamba sheria ni kwa upande mmoja, wakati upande wa pili unaweza kuact kivyovyote vile maadam ni taifa kubwa, hatari ya lojiki hii ni kwamba unaweza kuwa labeled gaidi na kusingiziwa maadamu unawawekea "usiku" wakubwa katika masilahi yao, na kabla hujapinduka wakawa wameshakumaliza tayari, halafu wakautangazia ulimwengu kwamba haki imetendeka!.

hii ishu ya Osama ilikuwa ni trial kwa taifa la marekani, ya uwezo wa kuuphold rule of law and justice hata katika wakati ambao ni mgumu kwa taifa.

Maadam Osama alikuwa Mtuhumiwa, dont tell me with surelity kwamba una uhakika wa yeye kuyafanya hayo Unayomuaccuse nayo!!!. Na vile vile mimi sina Uhakika wala ushahidi kwamba hakufanya hayo wanayosema kayafanya, ndiyo maana ninasema, namna ile walivyomshitaki, MILOBADAN SLOVEC, CARLOS THE JACKAL, SADDAM HUSSEIN, NORIEGA, CHARLES TAYLOR na wengineo wengi, basi OSAMA maadamu hakuresist alipouwawa, na pia hakuwa na silaha wakati wanampiga risasi, naye ilibidi ashitakiwe ili apate haki inayomstahili, kama ni kunyongwa anyongwe, kama ni kupigwa sinadano ya sumu apigwe, kama ni kufungwa kifungo cha maisha afungwe, and yes kama ni kuachiwa huru aachiwe!. isije ikawa labda kumbe walikuwa wanamuaccuse kumbe wala hausiki, au labda anahusika lakini siyo mastermind wa september 11, au pengine anahusika asilimia 100 na hivyo kunyongwa, au kufungwa kifungo cha maisha.
 
Gamba la Nyoka;1933904]tonachotofautiana ni kitu kifuatacho wewe unaamini Osama katenda hayo aliyoyatenda na kwa hiyo anastahiki hukumu hii iliyomfika, lakini hujiulizi swali, je ni kweli katenda hayo wanayomtuhumu nayo?. Utajuaje kwamba vidhibiti vyote na ushahidi wote waliokuwa nao ikiwemo hizo video zake ni vya kweli kama humfikishi mbele ya vyombo vya sheria?.
Hakuwa tayari kutokea mbele ya sheria na miaka nenda rudi amekuwa wa kujificha, ingethibitikaje kuwa si kweli anayosingiziwa!Mimi naamini utawala wa sheria hata katika vita 'rules of engagement' lakini kwa gaidi sidhani kuwa kuna sheria kwasababu gaidi ni adui usiyemjua hadi pale anapokudhuru.
Elewa kuwa ugaidi si sawa na kibaka, hawa ni watu wanaoweza kubadili sura ya dunia kwa dakika na namna ya ku deal nao ni tofauti.
Maadam Osama alikuwa Mtuhumiwa, dont tell me with surelity kwamba una uhakika wa yeye kuyafanya hayo Unayomuaccuse nayo!!!. Na vile vile mimi sina Uhakika wala ushahidi kwamba hakufanya hayo wanayosema kayafanya, ndiyo maana ninasema, namna ile walivyomshitaki, MILOBADAN SLOVEC, CARLOS THE JACKAL, SADDAM HUSSEIN, NORIEGA, CHARLES TAYLOR . isije ikawa labda kumbe walikuwa wanamuaccuse kumbe wala hausiki.
Unakumbuka Noriega na Saddam Hussein, watu wameishutum marekani kuwa haki haikutendeka kwasababu wameshatakiwa tu na marekani na kuhukumiwa wakiwa mikononi mwa marekani. Hili la Osama lingeleta taabu tu, mara peleka the Hague, yaani chuki dhidi ya marekani ndiyo inaundiwa justification.

Nakumbuka kuna jambazi ametusumbua sana mtaani, kila tukimfikisha polisi tunaambiwa ushahidi, hatuna! lakini tunajua anasuka mipango yote kudhuru watu. Tumeishi kwa hofu miaka zaidi ya 5 na huyu bwana. Kila akifunguliwa mashtaka tunaambiwa tulete ushahidi, yaani yeye akivunja au vithibitisho! tunashindwa kesi, na kila akirudi mtaani wale wote waliosimamia kesi anawarudi sawia.
Siku moja usiku saa 5 mtu mmoja akapiga yowe la mwizi kwa huyu jamaa akiwa anatembea watu wakamshukia jambazi hadi mauti. Kuanzia hapo tunaishi maisha ya raha mstarehe. In fact ilikuja gundulika kuwa alifanya mauaji ya watu watano na ushahidi mwingi tu nyumbani kwake! Hatukuwa na ushahidi akiwa hai.

Sisi kama tumeridhia utawala wa sheria kimataifa uangalie uniambie ni washeria kweli au maigizo. Kibaka akiiba kuku kafie keko, fisadi tunajadiliana namna ya kurudisha fedha!
 
Osama: Umetuletea balaa na tafran kubwa huku ughaibuni. Kabla ya Sept 11 kila kitu kilikuwa shwaaaaaariiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Umeleta balaa za deportations, E-verify, kero za airport, FBI misikitini, sheria mpya za makaratasi kule INS kila kukicha etc.
Familia zimetenganishwa, marafiki wamekuwa deported etc. Mungu akuchome moto mara trillion moja. Ukawe kuni zetu kwenye moto wa kiama.
ROT AND ROT IN HELL, B-ASTARD USAMA!!
 
Hata kama unamkuta mtu anamchinja mwenzie lazima aende mahakamani haki ikatendeke.

We unajuaje labda Osama angeonekana INSANE!! angeachiwa

I support My President in this
 
Hata kama unamkuta mtu anamchinja mwenzie lazima aende mahakamani haki ikatendeke.
We unajuaje labda Osama angeonekana INSANE!! angeachiwa
I support My President in this

Mhh! Kwa maelezo yako naona hakukuwa na haja ya kumpeleka mahakamani,kwasababu asingeweza kuonekana INSANE zaidi ya alivyokuwa.
 
Ni kweli kabisa, hata kama angekuwepo hilo lipo siku zote vichwani vya magaidi. Jambo moja la muhimu ni kuwa yule kiongozi aliye wa 'inspire' sasa hayupo, kama atatokea mwengine the time will tell. Ujumbe umefika kuwa hata atakayejificha chini ya godoro atafikiwa tu.
Lakini elewa kuwa si mashambulizi kwa marekani tu, Ubalozi ulipolipuliwa hapa Dar hakufa mmarekani hata mmoja, ni wale masikini walinzi na watafuta riziki wa kitanzania na kikenya. Iligusa jamii yetu na sijui unaweza kuwaambia nini wafiwa.

Ndege zinapolipuliwa hujui nani atakuwemo ndani, majengo na treni zikilipuliwa hujui utakuwa wapi na nani atakuwepo humo ndani. Sep 11 watu waliokufa katika WTO wengi ni foreigners na utashangaa uingereza ilipoteza watu wengi zaidi.
Mwanahabari Mohamed Amin alifanya kazi katika sehemu za hatari, kwa babhati mbaya akiwa ndani ya ndege ya Ethiopian airline iliyotekwa akawa mhanga wa ugaidi bila kutarajia.
Dhana ya kushangilia kuwa wamarekani watashambuliwa ina mapungufu sana kwasababu hakika katika ugaidi hakuna aliye salama.

Ngurvi,
Umenitouch sana na maneno yako. They are so inspiring. Umenikumbusha na huyo Mohammed Amini, ni kati ya waandishi niliokuwa nawadmire sana. Go to hell Osama bin Laden.....the hell that you belong to...
 
Sisi wenyewe hapa kwetu wanaotuhumiwa kukwapua simu tunawachoma moto bila huruma...halafu eti leo tunamhurumia Osama kuwa ameuwawa bila kufikishwa mahakamani!!
 
Sisi wenyewe hapa kwetu wanaotuhumiwa kukwapua simu tunawachoma moto bila huruma...halafu eti leo tunamhurumia Osama kuwa ameuwawa bila kufikishwa mahakamani!!

two wrongs does not make one right!!!!.

What was hard to bring un-armed Osama to court and let the due law process proceed? I'll give you the scenarios why I think it was Imperative to bring Osama to court.

1) What If Osama was a totally insane person?

2)What if the person they killed was mistaken to be Osama, wouldn't it be wise that he be captured alive so that he may prove himself before the court of law that he is not Osama?

3) What if the evidence put forward to implicate Osama was fake, wouldn't it be in accordance to the spirit of law that Osama prove himself not guilty by providing an evidence of his own?.


4)What if Osama really was the mastermind of September 11, wouldn't it be wise to capture him alive so that to extract intelligence from him, for the benefit of defeating terror?
 
Back
Top Bottom