Kauli ya JK Kuipongeza Marekani kufuatia kifo cha Osama yaja?

He admitted himself that he planned and executed the 9/11 attacks.....

He also denied the participation in the attacks too!!. and there are videos for that!!.
so what should be believed, the denying video or the admitting one?, what about the authenticity of those tapes?, what if osama given nature of his intelligence training was trying to mislead USA from the real perpetrators who himself had no clue about, but supportive of their motives?
 
My Take:
Sijui kama tumechelewa au bado tunafikiria tutoe kauli ya namna gani. Kwa ufupi ingetakiwa tuwe miongoni mwa watu wa kwanza kutoa pongezi kwani mhusika wa uhalifu ulioua Watanzania 11 hatimaye hayupo tena baada ya kukutwa na kile ambacho kwa miaka mingi alikuwa akiwalazimisha kwa kutumia mafundisho na sera zake kiwakute wengine.

Ni matumaini yangu Rais atatoa kauli yeye mwenyewe kuelezea furaha ya Watanzania kuwa mhalifu nambari duniani amekutwa na haki. Haitaji kusema mengi au kuyapamba sana bali machache yenye kuonesha kuwa tunajalii kilichotokea.

Heshima kwako MM,

Hapo ndipo mara nyingi unafikia kujiuliza kama Tz kweli ni nchi yenye maono ya mbele, au kama ina viongozi wenye uwezo, au hata kuwa na ethos za uongozi. Kimataifa huwa (naendelea kuchunguza) haina rafiki ukiondoa China, Russia na India. Hata hapo EA marafiki zake ni wachache sana. Naifananisha na Pakistan na Saudia zilivyo kwa America, ila kwa Tz ni umaskini wao tu ndio unawafanya wailaghai America kwa kujipendekeza.

Na pia ni vizuri wakibaki kimya maana naelewa vizuri. Wakiongea wataharibu.[/QUOTE]

hapo mkuu, nakubaliana na wewe.
 
Hawa hawa watu wanaokataa OBL kafa, hata wanapoambiwa na Al Qaeda, ndiyo hao hao wanaoamini Babu wa Loliondo anaponya Ukimwi. Na ni waTZ kibao (labda 9/10, wanaofikiri hivyo)

Lakini hayanipi shida haya - nilishajiamuliaga kuwa IQ ya Tanzania iko chini kiasi cha kutisha. Hivi unajua Mtanzania mmoja akiingia China, National Inteligence Quotient ya taifa hilo hushuka kwa percentage kadhaa?
 
SlidingRoof,

You sound like one of Osama Bin Laden's right henchmen! You are totally wrong my friend.
There is no way you can defend the Killing of Osama Bin Laden,the International Terrorist who killed thousands including your fellow Tanzanians in August,1998.

Haiwezekani umtetee Osama kwa madai kuwa sisi kama Tanzania tume-sign mkataba wa sheria ya Kulinda uhai wa mtu. Hii sheria haiwezi kuwa applicable kwa mtu kama Osama. Huwezi kuvunja sheria hiyohiyo kwa KUWAUA WENGINE halafu udai the same LAW to spare your life. Never my dear! Who killed by the sword shall surely die by the sword, who killed by the bullet shall surely die by the bullet,same to the suicider bombers,etc.

The theoretical restraint on extra-judicial murder/execution is truly based on international law and it shall only appliies to those who obeys the same law. It's absurdity,inept and nonsense for someone claiming for the law to protect he/she while breaking the same law. There is no justification, not at all. Wewe unauwa wenzako kwa kuwalipua na mabomu,halafu ukibanwa na kukamatwa unasema wasikuue! Pambaf kabisa. Ina maana uliowaua walikuwa kuku au sisimizi???!!

Kusema kuwa sisi kama taifa tumetia saini sharia hiyo ati sasa iweje leo tukawafuata hawa jamaa blindly kuunga mkono uhuni kama aliyofanyiwa Osama ni upuuzi. Kumbuka kwamba Osama ni raia wa SAUDI ARABIA. Lakini haohao Saudia waliukana uraia wa huyu Osama Bin Laden na ndiyo maana hata alivyouawa juzi serikali ya USA walitaka waupeleke mwili wa Osama Saudia lakini serikali ya Saudia IKAKATAA kata kata!!!They were right! Kwanini wapokee mwili wa GAIDI???

Sasa kama Nchi ya SUADI ARABIA ambayo ni nchi yake OSAMA imemkataa, iweje wewe kama MTANZANIA UNAMTETEAJE OSAMA BIN LADEN??????Je, mlitaka aje azikwe Tanzania??

Waislamu wakereketwa amkeni muondoe tongotongo machoni na muache ushabiki wa kijinga!

Spoken like a true JAMII FORUMS Great THINKER
I wont engage with you in any meaningful conversation. Its impossible to do so considering how rude and offensive with your personal attacks not only to me but to Muslims as a whole
 
He admitted himself that he planned and executed the 9/11 attacks.....

Pretty bad when even the FBI admit they have no hard evidence that he was responsible for 9/11. Don't believe me? Check out the list of crimes he was wanted for on their website.
 
Now for the case of bin-laden, who was un-armed at the time of his killing, why deny him justice and convict him like saddam hussein, like noriega, like those who commited genocide against the jews, like those who perpetrated genocide in rwanda. At least to them justice was done and evidence of their wrong doing was proved!!!. But where has the allegations against osama been proved to convict him to death by bullet while un-armed?.

Gamba, I think you don't know the ABC of OBL. The Alqaida is well organized group with intelligence and crews. As opposed to vibaka of Manzese the Alqaida crews are erudite individuals who understand the world better than most of us.

Osama was not the docile person to be arrested like Kibaka of manzese! At the time the SEAL invaded the house it was D-day as no one new exactly what was inside the house. There was a chance the house could be blown completely by Osama or his team.
So to suggest that he would have been arrested under the situation known now, is a myth.I say it again, at the time of executing such a delicate mission what time one could have to negotiate with OBL to get into helicopter!understanding that he vow not to surrender to foreign force at any cost.
Instead of thinking on rule of law bla bla blah... you need to look at the issue in three angle dimension.
 
The American government has admitted that the mission was to kill him, not to capture him!. had they wanted to capture him alive they would!, i believe the SEALS have this training too! and all those possibilities of bombs had been taken into consideration in mapping this mission.
but it seems the mission had already been decided, KILL HIM EVEN IF HE OFFERS NO RESISTANCE!, and this is what makes us believe Justice at the rule of law has been denied to him. may be he would be proved not guilty how do you know otherwise?.

There are circumstances of some who are alleged terrorists have been acquitted, even though they had suffered years in Guantanamo
.
Osama was not on FBI wanted list for September 11, with the admission of FBI itself that it had no enough evidence to implicate him on those attacks, but yet many charges have been made on him with American politicians, why dont you ask yourself this question?
 
Kimsingi Wamarekani wameingia katika mtindo wa Israeli sasa kwamba maghaidi hawawezi tena kujificha wakitegemea kuwa wakikamatwa watatiwa pingu na kusomewa miranda! Kumbuka SEALs hawafanyi kazi chini ya taratibu za kawaida za kisheria; wao siyo polisi! Jamani, miaka yote hii drones za CIA na jeshi zimekuwa zikiwapopoa watuhumiwa wa ughaidi kila kona kuanzia Afghanistan, Iraq, Pakistan yenyewe na hata Yemen bila kuwafikisha mahakamani au kutishia kuwatia pingu na hakuna watu waliolalamika kuwa kwanini hawakukamatwa! SEALs hawahawa ndio walioenda kuiokoa ile meli iliyochukuliwa mateka na maharamia na waliwapopoa maharamia kwa snipers na kumkamata yule bwana mdogo; watu hawakulalamika kuwa kwanini hawakuwakamata!

Lakini watu walitegemea Marekani iende imbembeleze Osama ajisalimishe, ageuke nyuma, atiwe pingu aambiwe "u have the right to remain silent"! Really? Nimeuliza kama Osama alikuwa hana hatia ya ughaidi dhidi ya Wamarekani na kuwa walikuwa wanamsingizia kwanini kwa mahela yote aliyokuwa nayo asiajiri mwanasheria makini na kujisalimisha miaka tisa iliyopita ili "asafishe jina lake" na kupewa siku mahakamani kujitetea na kuhoji ushahidi ulioko dhidi yake? Kama kweli Osama alikuwa anatafutwa bila kuhusika na vitendo vya ughaidi dhidi ya Wamarekani kwanini hakufunga safari toka pale Abbottabad na kwenda Islamabad na kujisalimisha kwenye Ubalozi wa Marekani ili wamtie pingu na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria? Hata Sadam Hussein alipokutwa kwenye "shimo la sungura" alipojisalimisha alitiwa pingu japo hatima yake ilishajulikana hata kabla hajakamatwa.

Khaled Sheikh Muhammed alikamatwa na kutiwa pingu
Zakaria Mousawi alikamatwa na kutiwa pingu

wote hawa walifanyiwa hivyo baada ya kujikuta hawawezi kukwepa sheria tena na kujisalimisha. Kwanini Osama hakujisalimisha kabla ya SEALs kuishukia nyumba yake kama mwewe? Ni wazi kuwa Osama angeweza tu kuepuka risasi kichwani kama angejisalimisha kabla lakini Navy SEALs waliposhuka walikuwa na ujumbe mmoja tu. Kumnyamazisha milele. Hili ndilo Waisraeli wamekuwa wakilifanya muda mrefu sana kwa maghaidi wao. Sasa Wamarekani nao wamekuwa wakilifanya hivyo kwa miaka hii kumi sasa nje ya sheria za kawaida zaidi ya sheria za vita.

Osama he was a dead man walking. Kama yeye na mashabiki wake waliongoza kukata hukumu ya kifo kwa maeflu ya watu bila kuwatajia makosa yao au kuwapa nafasi ya kujitetea miongoni mwao wakiwemo Watanzania 11 ni wazi kuwa alishajikatia na yeye mwenyewe hukumu. Tunashukuru Wamarekani wameenda kuitekeleza hukumu hiyo. Next time the next terrorist wannabe itabidi wafikirie tena. Angekuwa amejifunga mkanda wenye mabomu ya kujilipua kama mashabiki wake walivyofanya labda angekufa na ushujaa fulani. Kwa mtu ambaye amewaongoza watu wengine kufa na maadui zao yeye mwenyewe hata ardhi ya jengo lake alishindwa kupanda mabomu.

Cha kushangaza inadaiwa alikuwa amejifungia kiunoni fedha zaidi ili ikibidi kutoroka basi atoroke mara moja! Hakuwa tayari kufa, ila alikuwa tayari kutaka wengine wafe kwa ajili yake! Well.. it didn't work.
 
Bottom-line Marekani ni ijiandae tu kushambuliwa tena. Inaweza isiwe leo, kesho, au keshokutwa lakini mtu utakuwa mjinga kubweteka na kudhania kwamba vita vimeisha. Hivi vita havitaisha ng'o.
 
Bottom-line Marekani ni ijiandae tu kushambuliwa tena. Inaweza isiwe leo, kesho, au keshokutwa lakini mtu utakuwa mjinga kubweteka na kudhania kwamba vita vimeisha. Hivi vita havitaisha ng'o.

mzee ni kweli lakini sasa hivi message imetumwa kwa maghaidi wote kuwa Marekani haitojificha tena kumfuata mtu yeyote mahali popote na wakati wowote.. imagine this.. hakuna mtu ambaye ameweza kuwakwepa maafisa wa usalama kama Osama; mfano wake alikuwa Carlos the Jackal.. lakini Carlos alikamatwa na kufikishwa mahakamani. Wamarekani wameamua kwenda njia ya Waisraeli.. wanaweza kuingia nchi yeyote kumchukua au kumlipua audi yao na baadaye wakaanza kuwachanganya watukwa stori mbalimbali..

Ukweli hata hivyo ni kuwa hakuna mtu ambaye anaweza kuwa inspiring figure ya caliber ya Osama. Ukiniuliza mimi labda yule Muqtadar Al-Sadr aamue kujivisha jukumu hilo. So far hajaonesha chuki ya magharibi kama aliyokuwa nayo Osama. Lakini kama Kushindwa kwa nazi Jerumani hakukuondoa hisia ya baadhi ya weupe kuwa ni bora kuliko wengine lakini kuondolewa kwa Hitler kuliiondolea dunia alama ya itikadi ile ya unazi. Kuondolewa kwa Osama kumeiondolea dunia alama ya wazi ya itikadi ya chuki - or as I call him - mamluki wa itikadi ya chuki.

Ninaamini kabla ya mwaka huu Zawahri na yule bwana mdogo kule Yemeni nao wataletwa mbele ya haki au haki itawafuata huko huko. Osama was a uniting figure kwa wale wenye kushikilia itikadi ya chuki dhidi ya Magharibi. Na amepoteza umuhimu wake mkubwa baadaya mwamko wa Waarabu wa mapema mwaka huu. Na dunia ikiwasaidia Waarabu kuingia katika zama za demokrasia, utu na usawa ndivyo watu kama kina Osama watakavyozidi kutoweka na kubanwa pembeni mwa jamii zilizostaarabika.
 
Bottom-line Marekani ni ijiandae tu kushambuliwa tena. Inaweza isiwe leo, kesho, au keshokutwa lakini mtu utakuwa mjinga kubweteka na kudhania kwamba vita vimeisha. Hivi vita havitaisha ng'o.

Ni kweli kabisa, hata kama angekuwepo hilo lipo siku zote vichwani vya magaidi. Jambo moja la muhimu ni kuwa yule kiongozi aliye wa 'inspire' sasa hayupo, kama atatokea mwengine the time will tell. Ujumbe umefika kuwa hata atakayejificha chini ya godoro atafikiwa tu.
Lakini elewa kuwa si mashambulizi kwa marekani tu, Ubalozi ulipolipuliwa hapa Dar hakufa mmarekani hata mmoja, ni wale masikini walinzi na watafuta riziki wa kitanzania na kikenya. Iligusa jamii yetu na sijui unaweza kuwaambia nini wafiwa.

Ndege zinapolipuliwa hujui nani atakuwemo ndani, majengo na treni zikilipuliwa hujui utakuwa wapi na nani atakuwepo humo ndani. Sep 11 watu waliokufa katika WTO wengi ni foreigners na utashangaa uingereza ilipoteza watu wengi zaidi.
Mwanahabari Mohamed Amin alifanya kazi katika sehemu za hatari, kwa babhati mbaya akiwa ndani ya ndege ya Ethiopian airline iliyotekwa akawa mhanga wa ugaidi bila kutarajia.
Dhana ya kushangilia kuwa wamarekani watashambuliwa ina mapungufu sana kwasababu hakika katika ugaidi hakuna aliye salama.
 
Nguvu ya ughaidi ni hofu; ndio maana inaitwa "terror" kwa sababu inatumika kuwafanya watu waishi wasijihisi salama na kutembea kwa woga na hata kubadili namna wanavyoishi. Kwa kiasi kikubwa tukio la Septemba 11 limeibadili siyo Marekani tu bali dunia nzima, imebadilisha mahusiano ya watu na watu na hata jamii ya watu hao hao. Katika hili tunaweza kusema kuwa Osama "alifanikiwa" sana kuwa jinamizi lisiloonekana nyuma ya migongo ya Wamarekani na watu wengine duniani. Ni mara chache mtu anapanda ndege leo hii bila kuwazia itakuwaje kama ndege itatekwa!

Itikadi ya hofu inahitaji watu wa kuieneza; Osama alikuwa mtu pekee mwenye uwezo huo. Alikuwa na vitu ambavyo vilimpatia credibility kubwa kati ya mashabiki wake wengi kuliko mtu mwingine yoyote. Alikuwa ni mtu anayetoka kwenye familia ya matajiri, msomi na ambaye kwa kila kipimo angeweza kuishi maisha ya raha mustarehe kama matajiri wengine katika nchi za Kiarabu. Aliacha hayo yote na kujiunga na mujahidin na baadaye kuwa radical zaidi na kuona kuwa yeye ni mjumbe wa aina yake kwa nchi za Magharibi. Mvuto huu ulimtengenezea mashabiki wengi na wafuasi wengi ambao wengine sio wale waliobeba silaha au kujivika mabovu.

Baadhi yao ni watu ambao wanaishi katika maisha ya kawaida pote duniani ambao wanaamini mioyoni mwao kabisa kuwa Marekani ni adui yao - kama mtu mmoja mmoja au kama jamii. Watu ambao wanaamini kuwa nchi za Kimagharibi (Za Kikristu) ni kizuizi cha maendeleo na mafaniko ya jamii za Kiislamu ambazo ziliwahi kupiga hatua kubwa sana ya maendeleo ya sayansi na tamaduni wakati Magharibi wakiwa katika giza la zama za giza. Watu hawa wenye kuunga mkono mawazo hayo ni wasomi, watendaji wa taasisi mbalimbali, na wengine wanashikilia nafasi mbalimbali kama tulivyoona yule Daktari aliyeenda kuwaua wenzake akiwa yeye mwenyewe ni afisa wa juu wa jeshi la Marekani!

Kumbe kwa upande mmoja kama ilivyosemwa na wengine kuuawa kwa Osama kunaondoa tatizo la mtu wa kuamsha hisia za watu na kuwafanya watu waunganike nyuma yake lakini hauondoi hisia za uchungu au kuona watu wameonewa kuuawa shujaa wao. Msemaji wa ikulu ya Marekani mchana huu amesema kitu ambacho wengine tunakubaliana nacho - Osama hakuwa kiongozi wa Waislamu alikuwa ni Muuaji tu - ambaye alifurahia kuua mamia watu pote duniani. Alikuwa ni adui wa dunia. Ni wazi kuwa operesheni ya kuwaondoa hawa wenye hii itikadi ya chuki haitokoma kwa kifo cha Osama bali wengine kama kina Zawahri na wenzake watakuwa wakihama nyumba na vyumba wakitafuta mahali pa kujificha.

Njia pekee ya wao kuepukwa na yaliyomkuta kiongozi wao ni wao wenyewe kunyosha mikono juu na kwenda kujisalimisha kwa vyombo vya usalama wakikana kuhusika na vitendo vya ughaidi na hivyo waweze kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka mbalimbali dhidi yao. Mpaka watakapofanya hivyo tai mwenye kucha ndefu ataendelea kuzunguka juu yao na nafasi ikipatikana atashuka juu na kuwakwapua. Lazima ifike wote tuingie katika ulimwengu mambo leo wa ushirikiano baina ya jamii za binadamu bila kuwaacha wengine wakiendeleza vinyongo vya mababu!

Waarabu wameshaamka na kuchukuau nafasi yao na kuanza kutengeneza hatima yao mpya. Hawa kina Osama na wenzake hawana nafasi katika dunia mamboleo.
 
maishani tunajifunza mengi...pengine tutajifunza dawa sio kujivua gamba ni kufanya mambo yanayotakiwa kufanyika na kuacha hadithi
 
The American government has admitted that the mission was to kill him, not to capture him!. had they wanted to capture him alive they would!, i believe the SEALS have this training too! and all those possibilities of bombs had been taken into consideration in mapping this mission.
but it seems the mission had already been decided, KILL HIM EVEN IF HE OFFERS NO RESISTANCE!, and this is what makes us believe Justice at the rule of law has been denied to him. may be he would be proved not guilty how do you know otherwise?.

There are circumstances of some who are alleged terrorists have been acquitted, even though they had suffered years in Guantanamo
.
Osama was not on FBI wanted list for September 11, with the admission of FBI itself that it had no enough evidence to implicate him on those attacks, but yet many charges have been made on him with American politicians, why dont you ask yourself this question?

He was the most wanted person in the planet with a bounty of 25 millions dollars on his head.
I don't understand why you think Osama has been denied justice, a person who has committed atrocities in our modern history.
Osama could not come up and make his case openly; instead he planned and executed murders to thousands of his brother and sisters in his own region. He never took to justice those alleged to violate his principles.
What is so special to Osama when comes a question of justice, while we know thousands have been denied the same!
Justice should be applied across the board and not to a single monster.
 
Ni kweli kabisa, hata kama angekuwepo hilo lipo siku zote vichwani vya magaidi. Jambo moja la muhimu ni kuwa yule kiongozi aliye wa 'inspire' sasa hayupo, kama atatokea mwengine the time will tell. Ujumbe umefika kuwa hata atakayejificha chini ya godoro atafikiwa tu.

Ughaidi umeanza zamani hata kabla ya Osama hajapanda chati. Hapo utaona hao maghaidi wa zamani hawakuhamasishwa na Osama. Osama kapanda chati kuanzia 1998. Hivyo basi kifo chake (kama kweli kafa) kitahamasisha wengine zaidi kutaka kuifanyia mabaya Marekani.

Lakini elewa kuwa si mashambulizi kwa marekani tu, Ubalozi ulipolipuliwa hapa Dar hakufa mmarekani hata mmoja, ni wale masikini walinzi na watafuta riziki wa kitanzania na kikenya. Iligusa jamii yetu na sijui unaweza kuwaambia nini wafiwa.
Wao hulenga maslahi ya Marekani kwa hiyo wengine mkikumbwa ni bahati mbaya tu.

Ndege zinapolipuliwa hujui nani atakuwemo ndani, majengo na treni zikilipuliwa hujui utakuwa wapi na nani atakuwepo humo ndani. Sep 11 watu waliokufa katika WTO wengi ni foreigners na utashangaa uingereza ilipoteza watu wengi zaidi.
Kwa bahati mbaya hilo ni kama limesahaulika vile kwa sababu leo hii hata viongozi wa Marekani bado husema eti Waamerika 3,000 na kitu ndo waliouwawa siku ile ya 9/11.

Mwanahabari Mohamed Amin alifanya kazi katika sehemu za hatari, kwa babhati mbaya akiwa ndani ya ndege ya Ethiopian airline iliyotekwa akawa mhanga wa ugaidi bila kutarajia.
Dhana ya kushangilia kuwa wamarekani watashambuliwa ina mapungufu sana kwasababu hakika katika ugaidi hakuna aliye salama.
Wapende wasipende Wamarekani inabidi wajiangalie na kujifanyia tathmini pia. Kwa nini Waarabu wawachukie hivyo? Lazima kuna sababu za msingi. Ila habari ndo hiyo, Marekani haitakuwa salama kwa muda mrefu sana na kwa bahati mbaya na sisi wengine tutajikuta tumo kwenye mix ya ugomvi ambao hata hautuhusu.

Na maghaidi nao wakae mkao wa tahadhari wakijua kwamba Marekani haitachoka kuwashikisha adabu. Hapo chacha ndo ngoma inogile. Sijui nani atasalimu amri kwa mwenzake
 
Ughaidi umeanza zamani hata kabla ya Osama hajapanda chati. Hapo utaona hao maghaidi wa zamani hawakuhamasishwa na Osama. Osama kapanda chati kuanzia 1998. Hivyo basi kifo chake (kama kweli kafa) kitahamasisha wengine zaidi kutaka kuifanyia mabaya Marekani.

Wao hulenga maslahi ya Marekani kwa hiyo wengine mkikumbwa ni bahati mbaya tu.

Kwa bahati mbaya hilo ni kama limesahaulika vile kwa sababu leo hii hata viongozi wa Marekani bado husema eti Waamerika 3,000 na kitu ndo waliouwawa siku ile ya 9/11.

Wapende wasipende Wamarekani inabidi wajiangalie na kujifanyia tathmini pia. Kwa nini Waarabu wawachukie hivyo? Lazima kuna sababu za msingi. Ila habari ndo hiyo, Marekani haitakuwa salama kwa muda mrefu sana na kwa bahati mbaya na sisi wengine tutajikuta tumo kwenye mix ya ugomvi ambao hata hautuhusu.

Na maghaidi nao wakae mkao wa tahadhari wakijua kwamba Marekani haitachoka kuwashikisha adabu. Hapo chacha ndo ngoma inogile. Sijui nani atasalimu amri kwa mwenzake

Mzee njia pekee ya Marekani kuwatuliza hao maghaidi ni ile ya kukubali kutokuwa Marekani. Yaani, lazima ikubali kubadilika na kuachana na tunu ambazo zimeifanya iwe Marekani. Yaani, kukubali kucompromise mbele ya terror. Hicho ndicho Osama alikitaka na hata hao wengine waliosalia wanakitaka. Lakini, kama maghaidi wanaweza kuitishia Marekani hadi ikabadilika na kuwa isivyo ni nchi gani inaweza kusalimika? Ukiangalia sana utaona kuwa malalamiko ya hao maghaidi yamejibiwa na Waarabu walioamka Tahrir Square na Tunisia, Saudia na Yemen, Oman na Syria.

Hao wananchi wametambua kuwa adui zao siyo Wamarekani wala nchi za Maghabiri bali viongozi wao wenyewe waliolelewa wakati mwingine na Wamarekani lakini ambao wanaweza kuwajibishwa na wananchi wenyewe. Ndio maana Marekani haikuweza kumuokoa Hosni Mubarak dhidi ya hasira ya watu wake wala Saleh. Hatuwezikusema Bashar ni zao la Marekani lakini naye amekataliwa na watu wake; hatuwezi kuilaumu Marekani kwa Ahmedinajad.

Maghaidi kama walivyo wahalifu wengine hawatahiji kukaa chini nao na kujadiliana nao. Ndio maana wengine tuliona ni mambo ya ajabu sana kuona serikali yetu eti inafanya vikao na mafisadi jinsi ya kurudisha fedha zetu ili nchi isilipuliwe. Ukikubali kutishiwa kiasi cha kukubali kubadili maisha yako sababu ya hofu unapoteza siyo uhuru wako tu bali hata utu wako. Wamarekani wamekataa kupigishwa magoti na Osama. Ni wazi kuwa na wenye kukumbatia itikadi ya chuki dhidi ya Marekani nao wameongezewa chuki hiyo baada ya kifo cha Osama. Hili halina shaka. Lakini, ukweli ni kwamba hawana ujasiri wa kuja nje na kudai madai yao mahakamani au kwa maandamano kama walivyofanya kina Khaled.

Kina Khaled waliweza kufanya kwa wiki mbili na kubadilisha kabisa sura ya Mashariki ya Kati kile ambacho Osama na vikaragosi wake walishindwa kukifanya kwa miaka ishirini hivi! Ukiniambia mimi kifo cha Osama kinafanya hoja za kina Khaled na kizazi kipya cha Waarabu kutambua zaidi kuwa ughaidi siyo njia ya kufikia mabadiliko ya kisiasa. Kama kutakuwa na rapid taking down ya hawa waliosalia utakuwa ni mwisho wa ughaidi wa aina ya Osama kwa muda mrefu. Kutakuwepo na majaribio (labda mengine yatafanikiwa) dhidi ya Marekani. Hiyo yote haiondoi ukweli kwamba ughaidi kama ufisadi havihitaji kuvumiliwa. Vinahitaji kuwa confronted na kuwa defeated.
 
Hivi mtu yeyote yule anayejificha kwa kuogopa kufa, ana haki gani ya kuwasababishia wengine kifo ? Nafikiri hapa Wamarekani wametoa onyo tosha kwa wote wenye nia ya kufuata nyayo za Osama kuwa ukipatikana ni risasi tu na mwili kutupwa baharini, full stop. Sijui ingekuwaje kama sisi hapa ndio tungemkamata, bila shaka majadiliano yangekuwa yanaendela kuhusu dau ! Labda Nape Nnauye angepewa jukumu hilo, masikini dogo !
 
Al Qaeda member surrenders, Saudi Arabia says

By Laura Rozen
In the wake of Osama bin Laden's demise, is al Qaeda falling apart?
The Saudi Interior Ministry said today that a senior al Qaeda member on Riyadh's most-wanted list named Khaled al-Qahtani called from abroad and turned himself in.
"Interior Ministry's spokesman Maj. Gen. Mansour Al-Turki said in a statement Wednesday that Khaled Hathal Abdullah al-Atifi al-Qahtani contacted the security authorities from an undisclosed country and expressed his wish to come home," the Associated Press reports.
"Al-Qahtani was reunited with his family and his surrender will be taken into consideration while looking into his case, Al-Turki said."
Mohammed_al_Quahtani.jpg
The Saudi Interior Ministry spokesman did not indicate when Khaled al-Qahtani gave himself up, but many members of the group's Yemeni wing, al Qaeda in the Arabian Peninsula (AQAP), have recently fled from Yemen, the AP writes.
It wasn't immediately possible to ascertain whether Khaled Al-Qahtani is the brother or relative of Mohammed al-Qahtani (pictured at right), a Saudi-born al Qaeda militant detained at the U.S. military detention facility at Guantanamo Bay, Cuba. Mohammed al-Qahtani, now 32, had been picked up in the battle of Tora Bora in Afghanistan from which bin Laden is believed to have escaped. While at Guantanamo, Mohammed al-Qahtani, 32, was reportedly subjected to severe U.S. torture, the senior official in charge of the U.S. office of military commissions told the Washington Post's Bob Woodward.
Mohammed al-Qahtani flew to Orlando, Fla., from Dubai in August 2001, a month before the Sept. 11 terrorist attacks, but was sent back to Dubai by U.S. immigration authorities suspicious he planned to remain in the country illegally. U.S. interrogators later said they found airport video surveillance showing the car of lead 9/11 hijacker Mohammed Atta waiting to pick al-Qahtani up at the Orlando airport.
The United States dropped charges against Mohammed al-Qahtani in May 2008, for reasons it did not disclose, but presumably related to the inadmissability of evidence obtained under torture. Al-Qahtani is still detained at Gitmo, but his habeas corpus case was reinstated after a Supreme Court ruling in 2008.
(Photo: Wikipedia)

My Take:
Osama angefanya kama alivyofanya huyu wala pesa nyingi zisingetumika kumtafuta hadi kumpata kwa miaka kumi sasa. Labda na yeye kujisalimisha kwa hiari kungeangaliwa kwenye kesi yake. But we will never know that.
 
Kimsingi Wamarekani wameingia katika mtindo wa Israeli sasa kwamba maghaidi hawawezi tena kujificha wakitegemea kuwa wakikamatwa watatiwa pingu na kusomewa miranda! Kumbuka SEALs hawafanyi kazi chini ya taratibu za kawaida za kisheria; wao siyo polisi! Jamani, miaka yote hii drones za CIA na jeshi zimekuwa zikiwapopoa watuhumiwa wa ughaidi kila kona kuanzia Afghanistan, Iraq, Pakistan yenyewe na hata Yemen bila kuwafikisha mahakamani au kutishia kuwatia pingu na hakuna watu waliolalamika kuwa kwanini hawakukamatwa! SEALs hawahawa ndio walioenda kuiokoa ile meli iliyochukuliwa mateka na maharamia na waliwapopoa maharamia kwa snipers na kumkamata yule bwana mdogo; watu hawakulalamika kuwa kwanini hawakuwakamata!

Lakini watu walitegemea Marekani iende imbembeleze Osama ajisalimishe, ageuke nyuma, atiwe pingu aambiwe "u have the right to remain silent"! Really? Nimeuliza kama Osama alikuwa hana hatia ya ughaidi dhidi ya Wamarekani na kuwa walikuwa wanamsingizia kwanini kwa mahela yote aliyokuwa nayo asiajiri mwanasheria makini na kujisalimisha miaka tisa iliyopita ili "asafishe jina lake" na kupewa siku mahakamani kujitetea na kuhoji ushahidi ulioko dhidi yake? Kama kweli Osama alikuwa anatafutwa bila kuhusika na vitendo vya ughaidi dhidi ya Wamarekani kwanini hakufunga safari toka pale Abbottabad na kwenda Islamabad na kujisalimisha kwenye Ubalozi wa Marekani ili wamtie pingu na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria? Hata Sadam Hussein alipokutwa kwenye "shimo la sungura" alipojisalimisha alitiwa pingu japo hatima yake ilishajulikana hata kabla hajakamatwa.

Khaled Sheikh Muhammed alikamatwa na kutiwa pingu
Zakaria Mousawi alikamatwa na kutiwa pingu

wote hawa walifanyiwa hivyo baada ya kujikuta hawawezi kukwepa sheria tena na kujisalimisha. Kwanini Osama hakujisalimisha kabla ya SEALs kuishukia nyumba yake kama mwewe? Ni wazi kuwa Osama angeweza tu kuepuka risasi kichwani kama angejisalimisha kabla lakini Navy SEALs waliposhuka walikuwa na ujumbe mmoja tu. Kumnyamazisha milele. Hili ndilo Waisraeli wamekuwa wakilifanya muda mrefu sana kwa maghaidi wao. Sasa Wamarekani nao wamekuwa wakilifanya hivyo kwa miaka hii kumi sasa nje ya sheria za kawaida zaidi ya sheria za vita.

Osama he was a dead man walking. Kama yeye na mashabiki wake waliongoza kukata hukumu ya kifo kwa maeflu ya watu bila kuwatajia makosa yao au kuwapa nafasi ya kujitetea miongoni mwao wakiwemo Watanzania 11 ni wazi kuwa alishajikatia na yeye mwenyewe hukumu. Tunashukuru Wamarekani wameenda kuitekeleza hukumu hiyo. Next time the next terrorist wannabe itabidi wafikirie tena. Angekuwa amejifunga mkanda wenye mabomu ya kujilipua kama mashabiki wake walivyofanya labda angekufa na ushujaa fulani. Kwa mtu ambaye amewaongoza watu wengine kufa na maadui zao yeye mwenyewe hata ardhi ya jengo lake alishindwa kupanda mabomu.

Cha kushangaza inadaiwa alikuwa amejifungia kiunoni fedha zaidi ili ikibidi kutoroka basi atoroke mara moja! Hakuwa tayari kufa, ila alikuwa tayari kutaka wengine wafe kwa ajili yake! Well.. it didn't work.
Kumbe nawe mzee mzima huwa unachemsha wakati mwingine, eeeh!
 
Nyani Ngabu;1932735]Ughaidi umeanza zamani hata kabla ya Osama.Hapo utaona hao maghaidi wa zamani hawakuhamasishwa na Osama. Osama kapanda chati kuanzia 1998
Usisahau kuwa ugaiidi wa siku za nyuma iulikuwa ni wa maslahi zaidi kuliko religious ideology. Osama ndiye ameingiza hili akitaka kuungwa mkono na kwa bahati mbaya tunaona mnavyomuunga mkono hata kwenye udhalimu usio na chembe za imani.

Wao hulenga maslahi ya Marekani kwa hiyo wengine mkikumbwa ni bahati mbaya tu
Kama aliyekumbwa ni baba au mama yako, kaka au dada usingetamka haya.
Mimi nimeona nikiwa kazini Aug 1998, nimesikia kishindo na nimebeba majeruhi ndani ya hospitali. Inaniwia vigumu na napata uchungu sana kwa maneno yako. Ungemuona yule bibi aliyekuja kuchukua maiti ya kijana wake au yule mama aliyeaachwa na watoto mayatima, neno bahati mbaya ungeliona tusi.

Kwa nini Waarabu wawachukie hivyo? Lazima kuna sababu za msingi. Ila habari ndo hiyo, Marekani haitakuwa salama kwa muda mrefu sana na kwa bahati mbaya na sisi wengine tutajikuta tumo kwenye mix ya ugomvi ambao hata hautuhusu
Si kweli, waarabu wanapenda sana marekani na nchi za magharibi. Vinginevyo tusingekuwa na waarabu wahamiaji haram marekani, Uingereza n.k, au tusingeona misururu ya kuomba visa kuja mareakani na nchi za magharibi.
Hebu jiulize, Tunisia, Libya, misri watu wote wamekimbilia Italy na sasa Shengen inafanyiwa marekebishokukidhi haja ya wahamiaji, sasa kwanini wasikimbilie Bahrain, Muscat, Saudi n.k.
 
Back
Top Bottom