Kauli ya JK itekelezwe kuwaokoa Wanawake

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
JANA ilikuwa ni Siku ya Wanawake Duniani. Viongozi wakuu wa nchi, wanaharakati wa masuala ya usawa wa kijinsia na wanawake walio mfano kwa wengine walikusanyika kutafakari hali ya kundi hilo lililo muhimu katika kila nyanja hapa nchini na duniani kwa ujumla wake.
Rais Jakaya Kikwete naye hakuwa kimya katika maadhimisho hayo ya kukumbuka na kuthamini pia kuangalia namna ya kulikwamua kundi hilo ambalo kwa ujumla wake limetupwa pembezoni kabisa na rasilimali za nchi.
Kutokana na hali halisi ya maisha ya wanawake hususan wale wa vijijini, tungependa kusema bila ya kumung’unya maneno kuwa amani ambayo Tanzania inajivunia tangu kupata uhuru, baadhi yao hawaitambui kutokana na ukandamizaji unaoendelea ndani ya jamii yetu na kutiwa baraka na mila na desturi zilizopo.
Katika kilele cha maazimishio ya siku hiyo ambayo kitaifa yalifanyika mkoani Tabora, Rais Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi aliahidi kuwa utawala wake (licha ya kubaki kipindi kidogo amalize awamu hii) kuwa itaendelea kuzifanyia marekebisho baadhi ya sheria zinazowakandamiza wanawake hapa nchini.
Tunamshukuru kiongozi huyo wa nchi si tu kwamba alikubali kuwa mgeni rasmi bali kwa kutambua kuwa katika utawala wake, kuna sheria kandamizi dhidi ya wanawake ambazo kwa namna moja ama nyinyine ni kikwazo kwa kundi hilo kutimiza ndoto za kimaendeleo.
Sisi, Tanzania Daima tunaongeza kuwa si sheria pekee ambazo zinamkandamiza mwanamke bali pia mila na desturi nazo zinamfanya mwanamke aishi kwa mashaka, kunyanyaswa na kushindwa kuamini iwapo taifa hili ni huru ama la.
Vyombo vya habari mara kwa mara vimekuwa vikiandika, kutangaza na tena kuonyesha matukio kadhaa ya unyanyasaji wa wanawake-matukio tunayoamini bila shaka yanatokana na kukomaa na pengine kuota mizizi kwa mfumo dume miongoni mwa jamii.
Mila na desturi hizo zimewafanya wanawake waonekane kuwa vyombo vya starehe hivyo vikishatumika, thamani haipo tena.
Katika takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa (UN) kupitia Idara ya Habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, ilibainika kwamba ukatili dhidi ya wanawake imezidi kuongezeka kwa kasi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kila mwaka, wanawake 5,000 huchinjwa kinyama duniani.
Katika takwmumu hizo za UN, kamwe Tanzania si kisiwa hata ijitoe katika mauaji ama hata manyanayaso ya kundi hilo muhimu katika jamiii. Hivyo inatupasa kuliangalia hilo na tujiulize kwa nini wanawake kama binadamu wasiishi kwa amani kama watu wengine?
Kama tulivyokwishaandika hapo juu kwa kumsifu rais kwa kukiri kuwa utawala wake unaongozwa na sheria ambazo moja kwa moja ni kikwazo ama zinamkandamiza mwanamke, ni dhahiri kuwa mabadiliko yanapaswa kuanzia katika hoja hii.
Kwa wanaharakati, vyombo vya habari, watunga sera na sheria (wabunge) wanapaswa kushiriki vema katika kuangalia ni sheria gani ambazo moja kwa moja ni kikwazo kwa kundi hilo na kujenga hoja ili zifike bungeni na kufanyiwa marekebisho.
Vyombo vya habari katika hilo, vinapaswa kufuatilia kwa karibu kumulika maeneo ya ukandamizaji wa mila na sheria mbalimbali-ambazo ni mbovu ili watunga sera na sheria waweze kuona na kutolea mifano kwa lengo moja tu; kushawishi mabadiliko yafanyike ili kuliokoa kundi hili ambalo ni uhai wa taifa lolote duniani.
Tunamshauri Rais Kikwete naye kuwa mstari wa mbele katika kuamsha fikra na mijadala kujadili sheria hizo kandamizi kwa wanawake ili kuweza kupata fikra pevu za kuwakomboa wanawake.
Aidha, tunamtaka rais mara aonapo miswada inayohusu uboreshwaji wa sheria hizo imetua mezani kwake, asiifumbie macho kuisaini kwa haraka.
Hii ni kwa kuwa amekwishalihakikishia taifa kuwa ana uwezo wa kuchukua hatamu na kuwaweka huru wanawake hapa nchini na hata kuwa mfano wa taifa lililopiga hatua kubwa ya kimaendeleo.
Kauli ya rais si ombi, kwa mamlaka aliyo nayo kutoka kwa umma, tunaamini kuwa alichosema ni amri ambayo inapaswa kutekelezwa mara moja.
My take:
Nitamuona Rais ni hero kama aliyoayaahidi kuhusu ukombozi wa mwanamke yatatekelezwa..Naamini this time,Rais anamaanisha anachokisema na sio changa la macho tena.
 
Back
Top Bottom