Kauli ya Jahazi asilia – Dola ya Zanzibar irudishwe

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Written by administrator // 20/05/2011 // Habari // 8 Comments

Waheshimiwa Wazanzibari
Asalam Aleikum,


Kwa heshima nakuleteeni hapa kauli ya Jahazi Asilia kuhusu “Shirikisho la Afrika Mashariki (East Arican Federation) na Muungano”.
Siku ya Alkhamis, tarehe 07.05.2011 Jahazi Asilia tulipata kufanya mazungumzo na redio “Bomba FM” na kujibu masuala ya wasikilizaji juu ya suala hili. Ijumaa ya tarehe 08.05.2011 tulitoa vipeperushi sehemu zote za Zanzibar kuhusiana na suala hili.
Ijumaa hii hii ulifanyika mkutano huko Bwawani kuhusiana na maoni ya Wazanzibari juu ya marekebisho ya katiba ya Tanzania. Msimamo wa Wazanzibari wote kwa jumla ulikuwa kauli moja tangu mwanzo mpaka mwisho, Wazanzibari walisimama kuonesha kutoridhia kwao na huu muungano na kuukataa kwa kauli moja. Wote walitaka ujumbe huu ufikishwe huko Bara.
Mtumweni Jabir
Naibu Katibu Mkuu
Jahazi Asilia
18 Mei, 2011
KAULI YA JAHAZI ASILIA
KUHUSU SHIRIKISHO LA AFRIKA YA MASHARIKI
(EAST AFRICAN FEDERATION) NA MUUNGANO
1. Katiba ya Chama Cha Jahazi Asilia
Katiba ya Chama Cha Jahazi Asilia imejengeka kuwepo kwa mfumo wa Sirikali tatu, Sirikali ya Zanzibar, Sirikali ya Tanganyika na Sirikali ya Muungano.
2. Shirikisho la Afrika Mashariki (East African Federation)
Mnamo miaka ya sitini, 1960s, viongozi wa sirikali za wakati huo, ambazo zilikwishapata uhuru wa nchi zao, wakati ambapo Zanzibar haijapata uhuru wake, uhuru wa Zanzibar uliopatikana Disemba, 1963. Viongozi hao, wakiwa ni Mwalimu Julius Nyerere wa Tanganyika, Mzee Jomo Kenyata wa Kenya, Bwana Melton Obote wa Uganda. Viongozi hawa kwa umoja wao walikubaliana kwamba baada ya uchaguzi wa Zanzibar wa 1963, na Zanzibar kupata uhuru wake, Zanzibar iwekewe sehemu yake ya kushiriki katika mazungumzo na mipango ya kuasisi “Shirikisho la Afrika Mashariki” (East African Federation), lenye wanachama wa nchi huru nne, nazo ni, Uganda, Kenya, Tanganyika na Zanzibar. Nchi zote hizi zitaendelea kuwa Nchi Huru Kamili, “Soveireign States”; na kuendelea kuwa na uwanachama wao kamili katika Umoja wa Mataifa, (United Nations) na pia kwenye Umoja wa Jumuia ya Madola, (Commonweath).
3. Chama Cha Jahazi Asilia kinataka, kulingana na Katiba yake kuwepo kwa Srikali tatu, Sirikali ya Zanzibar, Sirikali ya Tanganyika na Sirikali ya Muungano. Kwahivyo, Chama cha Jahazi Asili; kinadai kurejea Dola ya Zanzibar kama pale ilipojiunga na Umoja wa Mataifa, Disemba 1963, na kuwa mwanacha wa 112 katika Umoja huo.
4. Chama Cha Jahazi Asilia kinadai kurejea Dola ya zanzibar bila ya shuruti lolote. Chama Cha Jahazi Asilia, kinakataa kabisa mpango wowote ule wa kuleta kura ya maoni kuhusiana na suala la kurejea Dola ya Zanzibar; kwa sababu, kurejea Dola ya Zanzibar ni haki ya kimsingi ya Dola ya Zanzibar sawa na Dola yoyote ile ulimwenguni.
5. Tunawataka Wazanzibari tuungane pamoja tuendelee kudai Nchi yetu.. Tudai Nchi yetu kwa busara, utulivu, kushirikiana na viongozi wa sirikali yetu ya Zanzibar; bila ya fujo, maandamano, marumbano au mwenendo wowote utaovunja salama na utulivu tulionao nchi mwetu Zanzibar iliopatikana kutokana na maridhiano ya Wazanzibari yalioletwa na Rais Abeid Aman Karume na Maalim Seif Sharif Hamadi
Mwenyezi Mungu atuzidishie kila mafanikio na atudumishie mapenzi baina yetu, kushirikiana daima na kuwaombea siha njema viongozi wetu pamoja na kuendelea kuingoza nchi yetu katika kila kheri, Amin.
Mwenyekiti, Jahazi Asilia. April 08, 2011
Tafadhali ifikishe kwa mwenzio baada ya kuisoma.
 
Sijawaelewa... Jahazi Asilia ndio Wasemaji wa Watanzania Visiwani? Walipiga kura za Kutouunga muungano?
 
tarehe 7/5 ilikuwa jmosi. 8/may ilikuwa j2 humu inaelezwa kuwa ni alhamisi na ijmaa. ni ishara kwamba thread nzima ni ya kizushi?majungu?
 
Hivi hiki Chama kiko Tanzania pia???!!!!!. Wenzenu walipindua nyie mnataka mrejeshewe dola ya Zanzibar on silver plate. Mnafikiri kila kitu mdebwedo hee!. Subirini tu na hizo suluani zenu vipisi kama mtapata dola yenu au hamjui maana ya serikali ya Mapinduzi.
 
Hivi hiki Chama kiko Tanzania pia???!!!!!. Wenzenu walipindua nyie mnataka mrejeshewe dola ya Zanzibar on silver plate. Mnafikiri kila kitu mdebwedo hee!. Subirini tu na hizo suluani zenu vipisi kama mtapata dola yenu au hamjui maana ya serikali ya Mapinduzi.

Hishi chama kiko Zanzibar na viongozi wake ni wasisi wakubwa wa ccm Zanzibar akiwemo Dr Salmini Amour na Dr Bilali Haribu, kwa hio kuskia kuwa Jahadi asilia nayo inataka Dola ya Zanzibar irudi nifaraja kubwa kwa sisi Wazanzibar.

Sasa nyiyi Watanganyika mujitao Watanzania wivu wenu nini? Walio Jahadi asilia ni chama kiko Zanzibar na kinaongozwa na Wazanzibar hamuna Mtanganyika na kama munaumwa na nyiyi daini Tanganyika yenu munayo ipenda.

Kifo cha Muungano hakiko mbali ni Baraza la Uwakilishi au kura ya maoni ya Wazanzibar kusema Muungano basi.

Jee mutabaki na jina la Tanzania au mutabaki na Jina la Kutangatanga ktika mbuga ya nyika?
 
Hishi chama kiko Zanzibar na viongozi wake ni wasisi wakubwa wa ccm Zanzibar akiwemo Dr Salmini Amour na Dr Bilali Haribu, kwa hio kuskia kuwa Jahadi asilia nayo inataka Dola ya Zanzibar irudi nifaraja kubwa kwa sisi Wazanzibar.

Sasa nyiyi Watanganyika mujitao Watanzania wivu wenu nini? Walio Jahadi asilia ni chama kiko Zanzibar na kinaongozwa na Wazanzibar hamuna Mtanganyika na kama munaumwa na nyiyi daini Tanganyika yenu munayo ipenda.

Kifo cha Muungano hakiko mbali ni Baraza la Uwakilishi au kura ya maoni ya Wazanzibar kusema Muungano basi.

Jee mutabaki na jina la Tanzania au mutabaki na Jina la Kutangatanga ktika mbuga ya nyika?

Sawa mheshimiwa nashukuru pia, kwa kunitajia hao wanachama. Kuhusu jina la nchi yetu baada ya muungano kufa hilo halina shaka, jina tu!, tutachagua lolote tunalotaka. Tunaweza kujiita hata Makunduchi au Mchamba wima, yote ni majina tu. Hata tukibaki na Tanzania itakuwa poa tu, kwani bado litakuwa halina hati miliki baada ya kufa muungano. By the way mnasuburi nini kama uwezo mnao, si waiteni tu ndugu zetu wanang'ang'ania posho za serikali ya Muungano warudi harafu tangazeni nchi yenu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom