Kauli ya First Lady wa Dk. Slaa, Josephine

Zion, nakuunga mkono kwa asilimia 100,kwa sababu ukimwi siyo ugonjwa bali ni upungufu wa kinga mwilini ambapo mwathirika anaweza akaishi zaidi ya miaka 20 huku akiendelea kufanya shughuri zake kama kawaida iwapo atazingatia masharti ya matumizi ya dawa za kuongeza kinga mwilini. Je? tumewaona watanzania wangapi wanafanya kazi na wanatumia dawa kila siku kulingana na magojwa waliyonayo huku utendaji wao ukiwa mzuri na wa kuigwa.

Huyu wa kwenu utendaji wake ni washaka kwani:-

1. Anaonekana kuwa msahaulifu. mfano anatoa ahadi alafu atekelezi na kabla ajatekeleza za mwanzo anatoa nyingine mpya.

2. Sio mkakamavu ananguka jukwaani kama Mzee wa miaka 80 (Bob makani)

3. Anasahau kauli zake. Mfano alisema waziwazi kuwa hataki kura za wafanyakazi leo anabisha kuwa hakusema hivyo.

4. Inaelekea anashindwa kutofautisha KERO na MAENDELEO. mfano wakati wakazi wa dar wanalalamika miundombinu ya barabara ni michache ndio insababisha foleni yeye anasema foleni ndio dalili ya maendele. Jiji la dar lina njia Tatu tu za kuingilia mjini ukiondoa pantoni ya nne.

5.' ......

6. .......
 
Josephine kesha sema ni kweli alikuwa ameolewa na hawajawasiliana na mmewe kwa miaka mitatu. Saafi sana jose kwa ukweli na uwazi. Sasa mafisadi waliokwapua pesa zetu katika account ya EPA nao watakubali kujitokeza hadharani na kusema ni kweli tuliziiba na tumezirejesha? Na yule aliyezipokea akiri kuwa ni kweli nimepokea kiasi fulani kutoka kwa mwizi fulani na zipo account NO fulani? Ama wataendelea na jitihada zao za kufadhili siasa za maji taka wakifikiri watanzania wa sasa ni limbukeni wa kudanganyiwa peremende kwenye lulu yao?
SAA IMEFIKA AMBAPO KILA ANAEJIJUA NI FISADI ASAHAU KABISA KURA ZA WANANCHI.
 
attachment.php
 
Binti Zion
Ndio maana siasa za maisha binafsi zinatakiwa kukemewa kwa nguvu zote maana zina madhara sana. Na madhara yanakwenda si kwa wanaorushiana maneno bali kwa watu wao wa karibu hasa familia. Hili suala la "umechukua mke wa mtu" basi na "wewe una VVU" ni mambo binafsi, ila kwa kuwa mambo ni mwaga ugali, nami nimwage mboga siasa zinasonga ndo tumefika hapa

Kama hali ndiyo hiyo ndugu yangu,je,watanzania tunaelekea wapi? tunawajengea watoto wetu misingi ipi ya siasa za ushindani (vyama vingi)? kwamba lugha chafu zilizojaa kejeri,matusi, kashfya na udharalishaji ndizo mbinu sahihi katika siasa za ushindani?. Je ? hapo tunajenga au tunabomoa jamii iliyojengwa na wazee wetu katika misingi bora na imara .Tabia na mienendo ya kisiasa zinazoendelea hivi sasa lazima zikemewe na watanzania wote wenye kuitakia mema nchi yetu.
 
...
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Hatutaki hata kuzungumzia ‘status’ ya ukimwi kwa baadhi ya wagombea, ana wake wangapi, ana vimada wangapi...nani anakwenda nje kubadilisha damu kila miezi sita, hatutazungumzia siasa za chumbani kama wanavyotaka tufanye, kwa sababu hayatatatua matatizo tuliyonayo,” alisema.[/FONT]

...kwanini wananchi wasielezwe wazi afya ya kiongozi wanayetaka kumchagua? Huo ndio ujumbe wangu kwanini tufiche ugonjwa.




kwa sababu hayatatatua matatizo tuliyonayo.
 
hivi mwenye ukimwi sheria inamkataza kuwa kiongozi wa juu wa nchi?
 
Kama hali ndiyo hiyo ndugu yangu,je,watanzania tunaelekea wapi? tunawajengea watoto wetu misingi ipi ya siasa za ushindani (vyama vingi)? kwamba lugha chafu zilizojaa kejeri,matusi, kashfya na udharalishaji ndizo mbinu sahihi katika siasa za ushindani?. Je ? hapo tunajenga au tunabomoa jamii iliyojengwa na wazee wetu katika misingi bora na imara .Tabia na mienendo ya kisiasa zinazoendelea hivi sasa lazima zikemewe na watanzania wote wenye kuitakia mema nchi yetu.
Leo ndio umeyakumbuka maneno ya busara baada ya Lissu kusema hili.
 
Jamani acheni hasira za kupitliza... suala la UKIMWI ni confidential na waathirika wanahaki zote za kufanya kazi na kuwa viongozi. tuache unyanyapaa. pengine hata wewe una UKIMWi umepima wewe? au hata dawa unatumia
 
Huu ni upuuzi na ni dalili mbaya sana kwa nchi yetu. Yaani CCM wanajaribu kujenga chuki kwenye jamii badala ya kuuchukulia uchaguzi kama mchakato tu wa kuomba ridhaa ya Watanzania. Na laiti wangejua kuwa Watanzania hata hawana muda wa kusikiliza hadithi zao chafu. Sijawahi kusikia kiongozi hata mmoja akisulubiwa na umma kwa ajili ya ukware. Mifano iko mingi ukianzia na watu kama Marehemu Ditto. Kwa maana hiyo sina hakika CCM wana malengo gani. Kama ni ukware naamini CCM ndo nyumbani kwake. Watazania wengi ni wakware na kwa hiyo habari kama hizi siyo issue kubwa. Labda walidhani kuwa hii issue inaweza kubalance madudu yao ya ufisadi. These guys made a grave miscalculation and they better rethink twice!
 
Mkuu huchoki???????? You would have been making a point lakini I see in ur mind unafikiri Dr. Slaa anazuia Lipumba kuchagulika which is non sense, this is democracy live with it. Na kinachoendelea kwenye hii ishu ni sehemu ya siasa. Kwa hiyo kama wewe unaona dr. slaa hafai kwa sababu ya hii issue ni sawa and you have tht right lakini siyo kulalamika weeeeeeeeeeeeee kwenye kila thread. Lipumba will be a distant third this yr, na ndiyo mwisho wake kisiasa. Mark my words. That is a fact, na ni sehemu ya siasa pia.[/QUOTE]

Kwenye bold huo ndio ukweli wenyewe hata kama wengine hawatapenda kuusikia.
 
Jamani acheni hasira za kupitliza... suala la UKIMWI ni confidential na waathirika wanahaki zote za kufanya kazi na kuwa viongozi. tuache unyanyapaa. pengine hata wewe una UKIMWi umepima wewe? au hata dawa unatumia
Suala la Ukimwi ni confidential ila la chumbani ni public, is that you are trying to advocate!
 
Kuna mmoja kati ya wagombea urais aliwahi kupima katika kuhamasisha kampeni za upimaji wa hiari pale mnazi mmoja,sijui alitoa majibu?Mwenye data atujuze.
 
Haya mambo ya ukimwi kwa wagombea, unafikiri wapiga kura hali zao zikoje? asijekuwa anapunguza kura zake kwa kuropoka hovyo akidhani anasaidia kampeni. Kwa taarifa yenu wenye ukimwi tuko wengi na wale wazima wanauguliwa au hata pengine kufiwa na watu wao wa karibu, tuache mambo ya UNYANYAPAA!

Huyu Tundu Lisu mara nyingine huwa controversial, si ajabu amegombea ubunge hii mara ya 3 na katika majimbo tofauti na hatutashangaa mwaka huu akabwaga tena!
 
Jamani acheni hasira za kupitliza... suala la UKIMWI ni confidential na waathirika wanahaki zote za kufanya kazi na kuwa viongozi. tuache unyanyapaa. pengine hata wewe una UKIMWi umepima wewe? au hata dawa unatumia


Wanaoambukiza ukimwi siku zahesabika-Kikwete



Jakaya Kikwete, amesema watu wote wanaojijua kuwa wameathirika na Ukimwi na kuwasambazia wengine kwa makusudi siku zao zinahesabika.

Na Jackson Kalindimya, Tabora
Rais Jakaya Kikwete, amesema watu wote wanaojijua kuwa wameathirika na Ukimwi na kuwasambazia wengine kwa makusudi siku zao zinahesabika.
Rais Kikwete pia ametangaza hadharani majibu ya vipimo vyake vya VVU kuwa yanaonyesha hajaathirika.
Amesema kuna watu wanajijua kuwa wanaishi na VVU lakini wamekuwa wakitumia vishawishi au njia nyingine zozote zile, kuwaambukiza wengine.

Akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika mjini hapa kitaifa jana, Rais Kikwete alisema sheria mpya ya Ukimwi itakapopitishwa na Bunge Februari mwakani, itawabana watu hao na kuwalinda watu wasiambukizwe Ukimwi kwa nguvu na watu wanaojijua kuwa wameathirika.
``Mtu huyo akitajwa kuwa ni mwathirika wa Ukimwi na anatumia hila mbalimbali zikiwemo fedha, mali au njia nyingine kuwaambukiza watu wengine atakamatwa na kupimwa kisha akibainika kuwa�anao�sheria itachukua mkondo wake``, alisisitiza.
Rais Kikwete alisema, licha ya sheria hiyo kuwabana watu hao, pia watu wote wanaowanyanyapaa na kuwatenga watu wenye virusi vya Ukimwi, ikiwa pamoja na kuwanyima haki zao za msingi nao hawatavumiliwa.
Akizungumzia mkakati wa upimaji kwa hiari, alisema anapenda kuona Tanzania inasifika kwa uhodari wa kuzuia watu wapya wasiambukizwe zaidi, badala ya uhodari tu wa kuwahudumia watu walioambukizwa Ukimwi.

�Rais Kikwete alisema taifa linajiandaa kuwahudumia waathirika wa Ukimwi na kati ya watu 220,000 waliothibitika kuwa wanaishi na virusi vya Ukimwi, kati yao 120,000 tayari wanahudumiwa na waliobaki taratibu za kuwahudumia zinakamilishwa.
``Tunataka waathirika wa Ukimwi wahudumiwe ili waweze kuishi maisha ya kawaida na kusogeza siku zao za kuishi`` aliuambia umati uliojitokeza kuhudhuria maadhimisho hayo.
Rais akigusia changamoto ya kupokea majibu baada ya kupima, alisema kuwa, wakati alipopima Ukimwi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, kuzindua kampeni ya upimaji kwa hiari, alikuwa na changamoto kubwa ya kuyasubiri majibu yake, lakini kwa kuwa anajiamini, anashukuru Mungu kuwa majibu yalionyesha kuwa yuko salama.
``Nilikuwa chumbani na Profesa Mwakyusa, ambaye yawezekana alikuwa na hofu kubwa zaidi kuhusu majibu ya Rais, yakiwa mabaya itakuwaje?�lakini majibu yakatoka ni salama.
Nawahimiza wananchi wote wakabili changamoto za kupima na kupokea majibu`` aliasa.
Kuhusu mwenendo wa zoezi la upimaji kwa hiari, alisema kuwa, zoezi hilo linakwenda vizuri na analifuatilia kwa karibu sana ili kuhakikisha kuwa linatoa matokeo yanayotarajiwa kwa manufaa ya taifa.
``Changamoto kubwa ni upya au ugeni wa zoezi hili. Kuna hofu na changamoto mbalimbali zikiwemo za walengwa, usafirishaji wa vifaa vya kupimia na posho za wapimaji ambazo zinashughulikiwa `` alisema.
Kikwete pia alisema serikali imeweka mipango endelevu ya miaka mitano 2008- 2012 kupambana na ukimwi, ikiwa pamoja na kuboresha huduma za uzuiaji na�upimaji, kinga na tiba.

Alisisitiza kuwa hali ya maambukizi bado ni ya kutisha na kwamba kila mmoja� ana wajibu wa�kutilia mkazo� jitihada kubwa za kuzuia ongezeko la wanaoathirika na� jamii kushirikiana na serikali katika uzuiaji maambukizi mapya kwa kuwa waaminifu katika mahusiano na kutumia kinga wanapofanya tendo la ndoa.
Aliwaonya pia watu wanaofuja mali zinazolengwa kwa waathirika wa Ukimwi na kujinufaisha wao kuwa hawatavumiliwa.

Waziri wa Afya, rofesa David Mwakyusa, akizungumza katika maadhimisho hayo ambayo kauli mbiu yake ni `Zuia Ukimwi,Timiza wajibu wako na Ongoza Mapambano`, alisema matokeo ya awali ya upimaji Ukimwi nchini, yanaonyesha kuwa watu milioni 2.5 sawa na asilimia 60.1 tayari wamepima. Lengo ni watu milioni 4.1 katika kipindi cha miezi sita tangu kuanza kwa zoezi hilo.
Aliitaja mikoa inayofanya vizuri zaidi kuwa ni Lindi iliyofikisha asilimia 115 na Kilimanjaro asilimia 96. Tabora ni ya 17 ambayo imefikisha asilimia 43.4. Wanawake ndio wanaoongoza kwa kujitokeza kupima.
Aliitaka mikoa yote kuendelea na upimaji wa hiari hata baada ya kupita kwa kipindi hicho, kwani zoezi la upimaji ni la kudumu na kuwataka wanaume nao kujitokeza kwa wingi kupima ili kujua hali ya afya zao.
Balozi wa Marekani nchini, Mark Green alimpongeza Rais Kikwete kwa namna alivyojitokeza kuongoza upimaji kwa hiari na kuwa mfano wa kuigwa.
Alisema binadamu sasa wanaishi katika kipindi cha misukosuko mikubwa katika historia ya maisha ya mwanadamu.

Balozi Green alisema katika nyakati zijazo,watoto na wajukuu zetu watapenda kujua kitu gani alichokifanya kila mmoja wetu katika vita dhidi ya Ukimwi na kujitoa kiasi gani katika kudhibiti maambukizi hayo.
Miongoni mwa waliohudhuria maadhimisho hayo ni Spika wa Bunge, Samwel Sitta, Waziri anayeshughulikia masuala ya Bunge, Dk. Batilda Buriani, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Abeid Mwinyimusa, Mwenyekiti wa TACAIDS, Dk. Fatuma Mrisho na viongozi wengine.

Source: Nipashe
 
Jamani eee Lissu hajataja mtu navojua kuna wagombea saba wa urais hata Mrema hagombei, alichosema baadhi inasemekana wana Ukimwi kwanini tunajihisi. Inavyo onyesha kumbe mnamjua kwanini sasa mnatetea kupeleka mzoga sorry mzigo ikulu?
 
Mara nyingi ugonjwa wa ukimwi unaathiri pia mfumo wa ubongo: mtu anaanza kuweweseka, kuongea mambo ya ajabuajabu, kusahau, kukosa mtiririko wa mawazo na mazungumzo, kufanya maamuzi yasiyotafakariwa kwa kina, nk. Ukimwi unapofikia hatua hii ni hatari sana kwa kiongozi kwani anaweza kutoa maamuzi yasiyo sahihi au yanayohatarisha usalama wa nchi na wananchi. Kwa mawazo yangu nadhani shida kubwa ya mwenye ukimwi na akiwa kiongozi iko hasa hapo. Mambo mengine yanaweza kuvumiliwa, lakini hili la akili nzima/timamu ni shida kubwa si ya kupuuzia.
 
Kumbe ndio maana Mtu mzima alipotolewa kwenye ze Utamu alituma majeshi yakamsake mwenye the Utamu kwa vile alijua oko mambo yangu yako karibu kubumbuluka nisipokaa tayari... Nitaanikwa zaidi...

Inabidi tuombe the utamu irudi tena kuja kutuletea habari maana inajua mengi mpaka kupata picha za kinamna.. sasa ni wakati wa watanzania kufumbua macho kuhusu afya zote za wagombea wetu ili tujue ni yupim tuko tayari kumgharimia kwa kodi au kwa insurance yake binafsi akiwa ofisini...
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom