Kauli ya chadema kuhusu Hotuba ya Kikwete na Maadhimisho ya CCM

luckman

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,211
371
Utangulizi:
Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imefuatilia matukio na maneno mbalimbali yaliyotolewa na CCM na viongozi wake wakuu akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho katika ‘sherehe’ za kuzaliwa tarehe 5 Februari 2012 .

Katika ‘sherehe’ hizo CCM imeshindwa kuonyesha kwa umma namna ambavyo chama hicho kimejipanga kushughulikia changamoto za msingi za kisiasa, kiuchumi na kijamii zinazolikabili taifa kama zilivyoelezwa katika tamko la CHADEMA kuhusu mwelekeo wa taifa mwaka 2012 lilitolewa na Katibu Mkuu Dr Wilbrod Slaa.

Aidha, ilitarajiwa kwamba Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete angetumia fursa hiyo kueleza hatua ambazo chama hicho kimechukua kushughulikia masuala ambayo aliyatolea kauli katika hotuba yake kama hiyo tarehe 5 Februari 2011 kuhusu kujivua gamba, utekelezaji wa ilani ya CCM na malipo ya tozo ya fidia kwa kampuni ya Dowans.

Badala yake CCM imetumia ‘sherehe’ hizo kuthibitisha namna chama hicho kilivyo chama dola kinachotumia rasilimali za umma katika kazi zake cha chama, kinavyofanya matumizi ya anasa ikiwemo kuvutia watu kwa ahadi za kuwapa chakula wakati serikali inaoongozwa na chama hicho ikiwa katika hali mbaya ya kifedha na kushindwa kutimiza madai ya msingi ya madaktari, wanafunzi wa vyuo vikuu, makundi muhimu katika jamii na kusuasua kwa miradi ya maendeleo kwa ujumla.

CCM imerudia tena kilichofanywa na serikali inayoongozwa na chama hicho ambayo ilifanya matumizi ya anasa ya zaidi ya bilioni 50 kwenye ‘sherehe’ za kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika wakati taifa likiwa katika changamoto mbalimbali.
Ikumbukwe kwamba katika hotuba yake kwa taifa ya tarehe 9 Disemba 2011 Rais Jakaya Kikwete aliahidi kwamba angetafuta siku ya kuzungumza kwa kina kuhusu hali ya taifa; zaidi ya miezi miwili baadaye Rais Kikwete amerudia tena kuahidi kwamba atatafuta siku ya kuzungumza masuala ya msingi yanayolikabili taifa hali ambayo inaashiria kuwa CCM na Mwenyekiti wake hawana majibu juu ya matatizo yanayolikabili taifa kwa sasa.

Kuhusu Siasa:

Kauli ya Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete ya kuendelea kusema kuna viongozi ndani ya chama hicho wanaotuhumiwa kwa mambo ya ovyo na kurudia kauli ya kuwataka wajitafakari sambamba na kutoa mwito kwa wanachama wa chama chake inaashiria kwamba CCM imeshindwa kuchukua hatua dhidi ya mafisadi katika chama hicho. Ilitarajiwa baada ya vikao vya chama hicho chini ya uenyekiti wake mwezi Aprili na Novemba 2011, CCM ingekutumia ‘sherehe’ yake hiyo kudhihirisha kwa umma hatua ambazo imechukua kwa mafisadi ndani ya chama hicho na serikali.

CCM izingatie kauli ya CHADEMA kwamba umma haujaridhika na uwajibikaji katika serikali na chama hicho ikiwa miaka minne imepita tangu kutolewa hadharani kwa Orodha ya Mafisadi (List of Shame) Septemba 15 mwaka 2007.
CHADEMA inaitaka CCM na serikali inayoongozwa na chama hicho kuhakikisha kwamba uchunguzi na uchukuaji wa hatua dhidi ya wahusika katika kashfa mbalimbali ili kurejesha utamaduni wa uwajibikaji unakamilishwa badala kuahirisha kuchukua hatua kamili serikalini, bungeni na hata ndani ya chama chenyewe.

CHADEMA ingependa umma uzingatie kuwa katika kipindi cha mwaka 2011 pamejitokeza tena ufisadi mwingine katika ngazi mbalimbali na utamaduni umekuwa ni ule ule wa maazimio kupitishwa ikiwemo na bunge bila utekelezaji wa haraka wa serikali na hatua stahiki za kinidhamu na kisheria kuchukuliwa kwa wahusika.

Hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete na viongozi wengine katika mkutano huo zimedhihirisha kuwa imeelemewa na ufisadi na wameshindwa kuchukua hatua kwa kuwa ufisadi umejikita katika mfumo mzima unaowagusa pia viongozi waandamizi katika chama na serikali hivyo namna pekee ya kusimamia uwajibikaji ni kwa kuunganisha nguvu za wananchi katika kutetea rasilimali za taifa.

Kuhusu Uchumi:

Pamoja na matatizo ya kiuchumi yanayolikabili taifa kwa sasa, CCM imekwepa katika ‘sherehe’ zake kuzungumzia namna ambavyo chama hicho kinachukua hatua za haraka za kutoa mwelekeo kwa serikali kukabiliana na hali hiyo.
Ukimya wa CCM kuhusu hali mbaya ya kiuchumi na kifedha ndani ya serikali ni ishara ya chama hicho kukosa majibu ya msingi kwa maswali ya msingi na pia kukosa maelezo juu ya utekelezaji wa ahadi ya chama hicho na Mwenyekiti wake Rais Kikwete ya kuhakikisha maisha bora kwa kila mtanzania.

CHADEMA inarudia tena kuitaka CCM na Serikali kutoa maelezo ya kina kuhusu hali tete na mwelekeo mbovu wa uchumi wa nchi yetu na kupanda kwa gharama ya maisha kwa wananchi kunakoendelea kusababishwa na pamoja na mambo mengine mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya shilingi.

CHADEMA inaitahadharisha CCM dhidi ya mikakati inayoendelea kutekelezwa na serikali inayoongozwa na chama hicho ya kuongeza malipo ya posho za vikao kwa baadhi ya viongozi waandamizi kama wabunge kukabiliana na ugumu wa maisha huku yenyewe serikali ikiikabili hali hiyo kwa kupandisha bei ya huduma za msingi zinazotolewa na taasisi zake huku ukimuacha mwananchi kwenye mazingira ya kipato kile kile wakati sekta ya umma ikiungana na sekta binafsi kupandisha bei za bidhaa na huduma. Hali hii ikiaachwa iendelee itakuza pengo la wenye nacho na wasionacho katika taifa na wakati huo huo itaongeza zaidi gharama za maisha kwa wananchi hususani wa kipato cha chini tofauti na ahadi ya Rais Kikwete na CCM ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.

CHADEMA inarudia kuitaka CCM na serikali inayoongozwa na chama hicho kuzingatia kwamba kipaumbele cha kikuu cha taifa na chama kiuchumi kiwe ni kunusuru uchumi wa nchi na kupunguza ongezeko la kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi.
Tunatarajia kwamba serikali inayoongozwa na CCM itazingatia mwito huu na kuwasilisha mpango maalum katika mkutano wa sita wa Bunge unaoendelea hivi sasa na kama sehemu ya utekelezaji wa mpango huo utafanya mapitio ya bajeti za Wizara zote za Serikali kwa kuzingatia maoni yaliyotolewa na Kambi ya Upinzani Bungeni. Pia, tunatarajia serikali kama ilivyofanya kwa suala la katiba mpya itazingatia hoja toka kwenye ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010 kuhusu hatua ambazo serikali inapaswa kuchukua katika kuinua uchumi wa nchi na kupunguza gharama za maisha kwa wananchi kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Kuhusu Jamii:

CCM na Mwenyekiti wake Rais Kikwete wamekwepa kuzungumza namna ambavyo chama hicho kimejipanga kisera na kiutendaji kuisimamia serikali kuboresha huduma za msingi za kijamii hususani elimu, afya, maji na nyinginezo kwa kuzingatia kwamba hali katika huduma hizo haulingani na umri wa taifa na rasilimali ambazo nchi inazo.

Katika hotuba hiyo ameeleza kwamba masuala mengine ya migogoro mathalani ya madaktari atayazungumza siku chache zijazo; na kwa upande wa mgogoro kati ya Serikali na wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga badala ya Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete kueleza namna chama chake kimejipanga kitaifa kisera na kimkakati kushughulikia matatizo yao ameishia na kuahidi kukutana na kikundi kimoja cha wamachinga. CHADEMA inatambua kwamba Serikali inayoongozwa na CCM imekuwa ikitumia wakuu wa mikoa na vyombo vya dola katika kuwanyanyasha wafanyabiashara ndogo ndogo katika maeneo mbalimbali nchini badala ya kutekeleza ahadi za Rais Kikwete kuhusu ‘wamachinga’ ambazo amezitoa kwa nyakati mbalimbali toka aingie katika urais mwaka 2005.

CHADEMA imekuwa mstari wa mbele kuwatetea wafanyabiashara hao nyakati zote ambapo CCM kimekuwa na kawaida ya kuwatumia nyakati za uchaguzi na kuwanyanyasa mara baada ya chaguzi.
CHADEMA inatambua kwamba kuna ongezeko la migogoro ya kijamii katika taifa ambayo serikali badala ya kushughulikia vyanzo vya migogoro hiyo inashughulikia matokeo na hivyo kuendeleza migogoro zaidi.

CHADEMA imebaini kwamba mtizamo wa Serikali katika kushughulikia migogoro katika mwaka 2011 umesukumwa na maelezo ya Rais Kikwete ya mwishoni mwa mwaka 2010 kwamba: “Najua wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa ambavyo vimepanga mikakati ya kuendeleza malumbano ya uchaguzi na kutaka Watanzania waishi kama vile nchi ipo kwenye kampeni za uchaguzi.Wamepanga wakati wote kutafuta jambo au hata kuzua jambo ili kuwachochea wananchi waichukie Serikali. Wamepanga kuchochea migomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwa mara.”

Na Mwenyekiti huyo wa CCM akasisitiza msimamo huo wa chama chake kwenye Hotuba yake ya tarehe 5 Februari 2011 kwamba “Hivi sasa wanakula njama za kutaka wapate kile walichokosa kwenye kura za wananchi kwa njia ya maandamano, migomo na kuchochea ghasia. Nalo wanajidanganya, kamwe hawatafanikiwa. Napenda kuwahakikishia wana-CCM na wananchi wenzangu wote pamoja na hao wanaohangaika usiku na mchana kupanga njama ovu na hujuma dhidi yangu na Chama cha Mapinduzi kuwa hawatafanikiwa ng’o. Wananchi wengi wa Tanzania ni werevu na wanajua kupambanua ukweli na uongo na zuri na baya. Hawatawafuata watu hasidi na wasioiombea mema nchi yetu na watu wake. Nawasihi msiwasikilize na msiwafuate watu ambao hawajali mateso watakayopata watu wengine ili mradi tu maslahi yao binafsi yanaendelezwa”

Katika hali hii madai ya haki za kisiasa, kiuchumi na kijamii za raia na makundi mbalimbali ya kijamii yamekuwa yakishughulikiwa na Serikali na mara nyingine kwa maelekezo ya CCM kama vile ni msukumo wa CHADEMA na viongozi wake na hatimaye badala ya serikali kushughulikia madai ya msingi imekuwa ikiwashughulikia wanaotoa madai hayo au matokeo ya madai hayo badala vyanzo vya madai hayo.

CHADEMA kinaitaka CCM na serikali kuweka mkazo katika kushughulikia migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, serikali na umma, na wananchi na wawekezaji katika maeneo mbalimbali yenye rasilimali za kilimo, misitu, madini na nyinginezo. CHADEMA kinaitaka CCM na Serikali kuzingatia kwamba kipaumbele kikuu cha kijamii iwe ni kushughulikia vyanzo vya migogoro katika maeneo mbalimbali badala ya kukabiliana na matokeo.

Hitimisho:

CHADEMA inarudia kutoa rai kwa umma watanzania na wanachama kutambua kwamba katika kusimamia vipaumbele vya kisiasa, kiuchumi na kijamii vya taifa na chama; CHADEMA kimejipanga kutimiza wajibu wa chama mbadala na chama kikuu cha upinzani nchini katika mwaka 2012 kwenye vyombo vya uwakilishi ambavyo tuna wajumbe wa kuchaguliwa na katika ngazi mbalimbali za chama.

Aidha, pamoja na kutumia mikutano ya maamuzi ya kiserikali na kichama CHADEMA kitaendelea kutumia pia njia nyingine zote za kidemokrasia ili kuunganisha umma katika kuiwajibisha CCM na serikali kutimiza wajibu wake katika kipindi cha sasa na kuwaongoza watanzania katika kufanya mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiuongozi katika taifa kupitia chaguzi zijazo .
CHADEMA kinatoa mwito kwa umma kupuuza kejeli zilizotolewa na CCM na viongozi wake katika maeneo mbalimbali ya nchi katika ‘sherehe’ za chama hicho zilizoanza tarehe 1 Februari mpaka 5 Februari 2012. Wanachama na wananchi kwa ujumla wazingatie kwamba CHADEMA itaendelea na ziara zake katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili kutimiza dhima yake ya kuhakikisha uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni dhabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania; kazi ambayo CCM wameishindwa miaka 35 tangu kuanzishwa kwa chama hicho.

John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
 
Nitarudi kusoma baadae kidogo maana imekuwa ndefu na hapa kuna mteja wa kumhudumia
 
Pamoja na kwamba upo ukweli katika hiyo kauli, lakini ni lini mataachana na mtindo
wa REACTION POLITICS na kujielekeza zaidi katika proactive measures??!!
Ninamaanisha kuwa kauli kama hii CCM waliitarajia kutoka kwenu, mngekuwa mmetarajia watakayoyasema
kwenye sherehe zao mngeweza kuwa pre-empty mapema...ni matarajio yetu kuwa kazi yenu ni kuongoza
njia ambayo hata wao wapende wasipende wataifuata, ndipo sisi wananchi tutakapo watofautisha nao...
Tumieni muda wenu kufanya utafiti wa kweli kuhusu matatizo yetu, bila kujali kama majibu yatawaathiri
au la...mfano kwa sasa wabunge ni watu wasioaminiwa kabisa hapa nchini(Mnyika ukiwamo), mmefanya nini
kutufanya tuwaamini???
 
chadema mpo juu!endeleeni kutafuta kila kona yale yanayotudidimiza watanzania na kutufanya tusisonge mbele kwa spidi kisha tuweekeni hadharani,ila wabunge wasijisahau kutembelea majimboni mara kwa mara na kusikiliza kero zetu na kuzitafutia ufumbuzi kwa kufanya hivyo uhakika wa kubaki kwenye majimbo utakuwepo pamoja na kuongeza mengine kwani kwasasa wananchi tunahitaji vitendo zaidi!kingine msiisahau igunga wapenzi wa chadema ni wengine hivyo muwe mnawatembelea na kuwatia nguvu hasa viongozi wa kitaifa wa cham ili wasibadili mawazo najua na wengine watafuata 2015 jimbo la chadema hilo,asante chadema oyeeeeeeee!
 
Pamoja na kwamba upo ukweli katika hiyo kauli, lakini ni lini mataachana na mtindo
wa REACTION POLITICS na kujielekeza zaidi katika proactive measures??!!
Ninamaanisha kuwa kauli kama hii CCM waliitarajia kutoka kwenu, mngekuwa mmetarajia watakayoyasema
kwenye sherehe zao mngeweza kuwa pre-empty mapema...ni matarajio yetu kuwa kazi yenu ni kuongoza
njia ambayo hata wao wapende wasipende wataifuata, ndipo sisi wananchi tutakapo watofautisha nao...
Tumieni muda wenu kufanya utafiti wa kweli kuhusu matatizo yetu, bila kujali kama majibu yatawaathiri
au la...mfano kwa sasa wabunge ni watu wasioaminiwa kabisa hapa nchini(Mnyika ukiwamo), mmefanya nini
kutufanya tuwaamini???

Jina lako ni moshi nyingi
 
taarifa nzima ya chadema inaongea kuhusu ccm2, maana yake nn,, mmekosa taarifa ya kuwaeleza watanzania? ,, mbona wao hawaongei ya kwenu? Hapo ndipo ninapogundua kuwa ya ccm ni mazuri kuliko ya cdm. Pilipili usoila yakuwashia nn?. Mtaiga sana ya ccm maana ni chama makini mkubali msikubali mtajifunza kutoka ccm.
 
Natanguliza pongezi kwa ufafanuzi na msimamo wenu (CHADEMA). Hongera Mheshimiwa Mnyika kwa ufafanuzi wa yale yaliojiri jana katika maadhimisho ya CCM. Mimi binafsi Sikuona tofauti ya sikukuu za kitaifa kwa maana ya za kiserikali na ile ya CCM. Nadiriki kusema katika maisha yangu sherehe ambazo watu walikula chakula katika maadhimisho kama hayo ilikuwa ni sherehe za saba saba miaka ya sabini! Nyati waliwindwa na kuwa kitoweo kwa wanafunzi waliokusanyika kucheza ngoma katika sherehe na wazazi wao pia. Niliposikia tangazo la watu kupata mlo ile siku nilijiuliza, Mafungu ya kulisha maelfu ya wale watu yanagharimiiwa na nani? Umuhimu wake ni nini? Je ile pesa ya kuwapa chakula wale maelfu isingetosha angalau kupunguza ahadi za Mheshimiwa Rais wetu alizotuahidi?
 
Nice press release! Kweli CHADEMA ni chama makini, andiko limeenda shule
 
taarifa nzima ya chadema inaongea kuhusu ccm2, maana yake nn,, mmekosa taarifa ya kuwaeleza watanzania? ,, mbona wao hawaongei ya kwenu? Hapo ndipo ninapogundua kuwa ya ccm ni mazuri kuliko ya cdm. Pilipili usoila yakuwashia nn?. Mtaiga sana ya ccm maana ni chama makini mkubali msikubali mtajifunza kutoka ccm.

hata kichwa cha habari husom! kwel wew na wao kam pipa na mfuniko
 
Pamoja na kwamba upo ukweli katika hiyo kauli, lakini ni lini mataachana na mtindo
wa REACTION POLITICS na kujielekeza zaidi katika proactive measures??!!
Ninamaanisha kuwa kauli kama hii CCM waliitarajia kutoka kwenu, mngekuwa mmetarajia watakayoyasema
kwenye sherehe zao mngeweza kuwa pre-empty mapema...ni matarajio yetu kuwa kazi yenu ni kuongoza
njia ambayo hata wao wapende wasipende wataifuata, ndipo sisi wananchi tutakapo watofautisha nao...
Tumieni muda wenu kufanya utafiti wa kweli kuhusu matatizo yetu, bila kujali kama majibu yatawaathiri
au la...mfano kwa sasa wabunge ni watu wasioaminiwa kabisa hapa nchini(Mnyika ukiwamo), mmefanya nini
kutufanya tuwaamini???
Mkuu, umesoma hiyo post? au unajibia experience na ulichojiaminisha kichwani mwako?

Kumbuka kwamba, CHADEMA wanawakumbusha CCM kwamba, tuliwaambia hivi, and youi havent done anything and you dont seem to prioritize a damn serious thing!!!

Kimsingi, CCM wanakumbushwa waamke, kwani walishaambiwa................. mimi nafikiri CCM inatakiwa kushukuru sana kuwa na chama pinzani kinachowaambia mabo ya kufanya na kuwakumbusaha kila wanapoonekana kujisahau!
 
taarifa nzima ya chadema inaongea kuhusu ccm2, maana yake nn,, mmekosa taarifa ya kuwaeleza watanzania? ,, mbona wao hawaongei ya kwenu? Hapo ndipo ninapogundua kuwa ya ccm ni mazuri kuliko ya cdm. Pilipili usoila yakuwashia nn?. Mtaiga sana ya ccm maana ni chama makini mkubali msikubali mtajifunza kutoka ccm.
Mpelekee ujumbe huu mwenyekiti wa chama chako, yule anaye manufacture teachers.........
mwambie wananchi wake ndio hawa!!!

5235999.jpg
 
taarifa nzima ya chadema inaongea kuhusu ccm2, maana yake nn,, mmekosa taarifa ya kuwaeleza watanzania? ,, mbona wao hawaongei ya kwenu? Hapo ndipo ninapogundua kuwa ya ccm ni mazuri kuliko ya cdm. Pilipili usoila yakuwashia nn?. Mtaiga sana ya ccm maana ni chama makini mkubali msikubali mtajifunza kutoka ccm.


soma kwanza kichwa cha habari ndo uongee!
 
nilikuwepo mjini wakati ccm wanafanya iyo sherehe,its hopeless and stupid!!wasukuma kwa ubwabwa/nyama hamjambo:eyebrows:

mwanza kuna "MGAO WA UMEME" ingawa sijui taarifa yoyote kwanini umeme unakatika kila siku kuazia asubuhi adi jioni isipokua siku ya sherehe mch mzima umeme ulikuwepo walipomaliza sherehe umeme ukaenda kwao adi usiku sana,na maji ni almost hakuna kabisa kutokana na katizo ilo la umeme.yani adi unasikitika watu wanavoteseka kwa hizi shida.
ivi mwanza kuna engineer/meneja wa tanesco kweli???
huu mji haukutakiwa kuwa katika hali hii ya dhiki ilhali madini almost yote na samaki wanapatikana kanda ya ziwa ila umaskini umekithiri adi unashindwa elewa kwanini?!!

ebu nikasome ile thread kule "kwanini tanzania ni maskini" labda nitaelewa japo
 
taarifa nzima ya chadema inaongea kuhusu ccm2, maana yake nn,, mmekosa taarifa ya kuwaeleza watanzania? ,, mbona wao hawaongei ya kwenu? Hapo ndipo ninapogundua kuwa ya ccm ni mazuri kuliko ya cdm. Pilipili usoila yakuwashia nn?. Mtaiga sana ya ccm maana ni chama makini mkubali msikubali mtajifunza kutoka ccm.

umesoma kichwa cha habari we mbwira kabla hujachangia.. Au hauangalii unapokwenda utajigonga kwenye ukuta.. Funguka akili achana na maisha ya bora liende.. Wake up pambana na maisha na tafuta jinsi ya wote sisi tufanye nini ili tuikomboe tanzania yetu..km ccm wanakosea acha wasemwe ili waache kabisa..
 
Nakubaliana na CDM. Rais wetu alitakiwa kutolea majibu masuala makubwa ya kitaifa ambayo yanazungushwa tu bila kupata majibu...
 
hii ndio maana ya chama cha siasa kisichokuwa madarakani, yaani kila anachofanya mwenzako lazima unakifanyia kazi, sio kusubiri uchaguzi tu kama wengine tusio wasikia..... wamelala mpaka watakapopewa ruzuku tena 2014.....2015
 
Back
Top Bottom