Kauli ya "Afande Sele" kuhusu gas Mtwara

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,697
8,843
JUMAMOSI NILIKUA MTWARA KWENYE KONGAMANO LA WANANCHI WA KUSINI NA SAKATA ZIMA LA GESI;

Kilichonifurahisha kwenye ule mkutano wa wazi ni kutoona bendera ya chama chochote, na kauli mbiu yao ya "GESI KWANZA VYAMA BAADAE" inaonyesha ukomavu wao kifikra, bila kujali tofauti zao wamesimama kwa pamoja kudai haki yao. (nitaziposti zile picha mjionee).

Siku zote anaeivuruga Nchi na kuichana vipandevipande ni viongozi wa Dola wanaondeleza dhuluma na kutokua na uwiano sawa katika kutumia/kufaidika na Rasilimali za Taifa, sio raia anaesimama na kuteteta haki yake inayodhulumiwa kwa miaka na kikundi kichache cha watu waliopo kwenye dola na mabwana zao (their lords) wawekezaji.

Huu ndio msingi wa madai ya Watu wa kusini (Lindi na Mtwara) na sio Mtwara pekee; Na kwamba si kuwa hawataki Gesi itumiwe kwa faida ya mikoa ingine ya Tanzania, bali wanataka mitambo ya kuzalisha huo umeme iwe palepale Mtwara ndipo umeme usambazwe kwa Mikoa mingine.

Ili kiinue Maisha na uchumi wa Mikoa ya Kusini ili nayo iwe na maendeleo kama miko mingine, ili nao waweze kupata ajira (Lindi hamna kiwanda hata kimoja), elimu (manispaa ya Lindi ina shule ya kidoto cha 5 na 6 moja, Lindi na Mtwara wana chuo Kikuu kimoja tu nacho ni cha Taasisi ya Dini, Roma na Chuo cha Serikali chenye kutoa kozi nyingi ni cha Utumishi wa Uma tu), miundombinu (miaka 51 toka tupate uhuru barabara kuu inayounganisha mikoa ya kusini na Dsm haijakamilika ujenzi wake), Huduma Bora za Afya (Lindi na Mtwara hawana Hospitali ya Rufaa wanategemea Muhimbili, barabara hawana tafakari masika atafikaje Dsm?) n.k, kwa kupata vitu hivyo watatulia makwao baadala ya sasa kila kitu kipo Dsm, ndio inachangia Dsm kuwa na Ongezeko kubwa la watu kila mwaka, na vijana kukosa ajira kiasi cha kuhatarisha amani na usalama wa Taifa,

Sasa kama bado kuna Mtanzania bado haoni\haungi mkono madai ya wana wa Kusini basi Taifa lipo mashakani,kwa kuwa Amani bila Haki haitadumu kila mwaka.Ole wao wale waoga wasiotaka kufikiri,"Bora uzee kuliko uzembe" Na woga wako katika kudai haki yako ndio umaskini wako,mzigo wa upumbavu ni zaidi ya gunia la mchanga mbichi.

Tusiwe kama manyumbu, simba mmoja au wawili wanamchukua mwenzao wakati wao wapo 200 wanaangalia.

Mungu ibariki Tanzania.



 
Waliomchakuwa kuwa Mfalme wa rhymes hawakukosea. Maana huwa ni mchambuzi wa vijimambo angalau, si kuweka mistari tu. Nilishawahi msoma pia akiandika kuhusu kwanini wamachinga wanaongezeka Dar, kwakweli aligusa mambo muhimu. Kama serikali haitachukuwa mawazo ya wasanii kama neutral ground inayowawakilisha wananchi basi watakuwa wanafanya makosa makubwa ambayo yatawagharimu sana. Swala la gesi kusini tusilipigie propaganda, tuliweke sawa na kukubaliana na wananchi.
 
Wana haki kudai maendeleo baada ya miaka 50 ya uhuru hawana lami ya uhakika, elimu duni, dawa za hospitali ni msamiati kwao.
 
namkubali sana huyu ndugu, alichoongea ni sehemu ya mistari yeke....tatizo bangi mno.!
 
Utadhani katoka chumba cha maiti..... anahema huku ana mashaka.

Ni kama alitaka kuwa na point lakini haeleweki kwa sababu alikuwa anawahi kuwa mtu wa kwanza ku- post JF
 
Meikumbuka ile show alovua nguo jukwaani,kumbe anapoint sometimes?nambiwa ndo mgombea ubunge wa moro kupitia CUF.
 
namkubali sana huyu ndugu, alichoongea ni sehemu ya mistari yeke....tatizo bangi mno.!

Nadhani ameacha na kwa sasa anajiandaa Kutafuta UBUNGE, SUGU kawa stua wasanii wengi sana kuwa inawezekana, nadhani itakuwa kwa Tiketi ya CUF.
 
Back
Top Bottom