Wana JF naombeni nafasi nami nipande jukwaani,
Kutokana na chanzo changu cha habari kilichopo jijini dar es salaam kilichokuwa kikidodosa dodosa kuhusu kucheleweshwa kutolewa majina ya walioomba mkopo kupitia HESLB chanzo kinaeleza kwamba mpaka ijumaa mambo yalikuwa yapo tayari kabisa na ruhusa ilikuwa imetolewa kwamba majina hayo yatolewe na watu wajionee ila sababu inayopelekea mpaka sasa majina hayo yasiwepo wazi ni kwamba kuna idadi kubwa ya wanafunzi wamekosa mikopo hiyo ya elimu ya juu na iwapo bodi itatoa majina hayo mapema basi watakabiliwa na vurugu kubwa itakayotokea eneo lile la ofisi za bodi. Mwanadodoso hakuishia hapo alipotaka kujua zaidi kwa nini wanafunzi wengi wakose mikopo majibu yaliyotoka pale ni kwamba : KAMA WAHADHIRI HADI LEO HAWAJAPATA MISHAHARA YAO SEMBUSE WEWE MWANAFUNZI?, TULIA HADI HAPO UTAKAPOONA MAJINA KWENYE WEBSITE MAMBO MENGINE NI YAKIOFISI ZAIDI....mwanadodoso mwenzangu aliishia hapo kwa hiyo tuwe wavumilivu tutaendelea kuwajuza yanayojiri maeneo hayo ya HESLB.
Mjumbe hafungwi. asanteni