Kauli inayomgharimu Hadji Mponda dhidi ya Madaktari

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Kuna watu wengi wamekuwa wakihoji kwa nini Waziri wa Afya ajiuzulu? Hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda nae alihoji swali hili wakati akizungumza na Waandishi wa habari hivi majuzi na akaenda mbali kwa kusema Waziri Mponda ni mgeni pale Wizarani na hadly ana kama mwaka mmoja ofisini. Kwa wale ambao hamjui kiini cha Madaktari kumchukia huyu Waziri napenda tu niwaambie kauli yake moja aliyoitoa wakati akihojiwa na waandishi wa habari kabla ya ule mgomo wa kwanza. Alisema hivi: Nanukuu

Mimi nawajibika kwa Wakulima na Wafugaji wa Jimbo la Ulanga Magharibi. Madaktari hawanihusu!

Mwisho wa kunukuu!
 
Alishasahau, wamkumbushe tena na tena!! Kiongozi mkubwa kama yeye tena Dr anashindwa ku-control kauli zake. Madaktari wakati mwingine walihitaji kitu kidogo, lakini kwa kauli kama hizo, inawafanya watu wawe discouraged!
 
Huyu anatakiwa afukuzwe na mapanga asionekane wala kusikika harufu yake hapa Tanzania. Akafie mbali na wala mait yake isirudishwe hapa Tz.
 
Kuna watu wengi wamekuwa wakihoji kwa nini Waziri wa Afya ajiuzulu? Hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda nae alihoji swali hili wakati akizungumza na Waandishi wa habari hivi majuzi na akaenda mbali kwa kusema Waziri Mponda ni mgeni pale Wizarani na hadly ana kama mwaka mmoja ofisini. Kwa wale ambao hamjui kiini cha Madaktari kumchukia huyu Waziri napenda tu niwaambie kauli yake moja aliyoitoa wakati akihojiwa na waandishi wa habari kabla ya ule mgomo wa kwanza. Alisema hivi: Nanukuu

Mwisho wa kunukuu!

Acha upuuzi wewe hiyo kauli ndiyo iwe sababu hao madaktari ni makanjanja tu, huwezi kumpa Rais masharti.
 
Ni wakati wa kuanza kuwawajibisha viongozi kwa kauli zao za dharau. He should go. Ngojea tukaichapishe hiyo kauli tumbandikie mlangoni kwa ofisi yake. Anafikiri kuongoza wizara ya afya ni kuidhinisha hela za kupeleka vigogo nje tu, aangalie sasa wizara yake imefilisika, hamna vifaa mahospitalini, wanafunzi muhimbili hawana chakula ( hivi ukimnyima mtu chakula kwa siku saba weye si muuaji?)
 
Acha upuuzi wewe hiyo kauli ndiyo iwe sababu hao madaktari ni makanjanja tu, huwezi kumpa Rais masharti.
kwani raisi ni nani? Km waziri wa wizara husika anatamka waziwazi kuwa wafanyakazi chini ya wizara yake hawamuhusu wanaomuhusu ni wapigakura wake, anabaki kuwa waziri wa kumwongoza na kusikiliza matatizo ya nani?? Kukiwa na tatizo lolote kwa madaktari watamfata nani? Nenda kaswaki unywe na chai ndo urudi kuchangia.
 
Madaktari ni makanjanja tu. Sasa itakuwa mchezo kila idara ya serikali iwe inampa rais masharti huo ni upuuzi
na kama rais atafanya kazi kwa umakini na umahiri hawezi pelekeshwa,hii yote inatokana na kuongozwa na rais asiyejitambua.
 
kwani raisi ni nani? Km waziri wa wizara husika anatamka waziwazi kuwa wafanyakazi chini ya wizara yake hawamuhusu wanaomuhusu ni wapigakura wake, anabaki kuwa waziri wa kumwongoza na kusikiliza matatizo ya nani?? Kukiwa na tatizo lolote kwa madaktari watamfata nani? Nenda kaswaki unywe na chai ndo urudi kuchangia.

Unauliza rais ni nani kweli wewe chai ya rangi. Wakifukuzwa hao mawaziri ndiyo matatizo ya madaktari yataisha au wakija mawaziri wapya watakuja na pesa za kutoka mfukoni mwao kuwapa hao madaktari makajanja wakati bunge la bajeti limeishapita.? Punguza gongo wewe.
 
Back
Top Bottom