Kauli hizi si-nzuri, binafsi sizipendi.......

Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
3,197
3,930
Kauli hizi kwa hakika zinanikera....
I. Wakulima kuzuiwa kuuza mazao yao eti kisa huenda kukawa na uhaba mkubwa sana wa chakula baadaye! kauli hii huwa inatolewa na viongozi katika namna ya kuonyesha Mkulima anahurumiwa!

II. Huyu fulani (wanataja jina) anasema nini sasa? wakati yeye aliwahi kuwa Kiongozi, kwenye Serikali ya awamu fulani?

Ninakerwa kwasababu,

Kauli ya I: Mbona wafanyakazi waajiriwa Serikalini au kwenye sekta binafsi hawapewi mishahara yao kidogo kidogo, wakati twafahamu wengine ni walevi, wazinzi n.k.? Kwanini nao wasitendewe kama atendewavyo mkulima?

Kauli ya II: Hivi ni kosa kwa Mtanzania yeyote kuukosoa utawala uliopo madarakani sasa eti kisa tu aliwahi kuwa DC, RC, etc etc kwenye Serikali ya awamu fulani?

Ni kwanini lakini? I stand to be corrected!
 
Kwenye chakula napinga

na na wewe kwani serikali inapaswa kuwa makini kwa maslahi ya watanzania wote kikubwa ipandishe bei za mazao ili wakulima wanufaiki. Pili, unapokosoa jambo lazima tuone vitendo na sio maneno matupu. Kama mtu alikuwa dc, rc au waziri halafu hakutenda kile anacho hubiri baada ya kustaafu huyo ni mnafiki.
 
Kwenye chakula napinga na na wewe kwani serikali inapaswa kuwa makini kwa maslahi ya watanzania wote kikubwa ipandishe bei za mazao ili wakulima wanufaiki. Pili, unapokosoa jambo lazima tuone vitendo na sio maneno matupu. Kama mtu alikuwa dc, rc au waziri halafu hakutenda kile anacho hubiri baada ya kustaafu huyo ni mnafiki.

Mkuu,
Shida ni kuwa bei ya mazao kwa mkulima ipo chini, na mfumuko wa bei ni mkubwa mno kumbuka, mkulima anapata mahitaji yake yote kupitia mazao yake. Akili ya kujua mbele kuna nini, kwa maana ya njaa hata yeye(mkulima anayo).

Kuhusu viongozi, nadhani walitenda vile kwa kutumia ilani ya chama kilichowapa mamlaka hayo kwa wakati huo. Je, vipi kama aliamua kuachia nafasi hiyo baada ya kugundua kuwa(ilani ) haikuwa ikitenda vyema? naye hapaswi kusema?
 
Mimi nitasema kidogo kuhusu chakula hayo ya viongozi tunawaachia wenyewe viongozi, Wakulima siku zote wamekuwa ni watu wa daraja la chini lakini ndo wazalishaji wakubwa wa mazao yote ya biashara na chakula na miaka ya hivi karibuni mfano kanda ya ziwa kwa sehemu wanazolima pamba wamepunguza kwa kiasi kikubwa kulima pamba na wamejikita zaidi kwenye kulima mahindi, kwa hiyo zao la mahindi kwa sasa limekuwa ni kwa ajili ya chakula lakini pia linawapatia pesa kwa ajili ya mahitaji ya kila siku kama vile kulipa ada, kununua mboga, mafuta ya taa, chumvi, sukari, nguo, matibabu, kununua vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kujenga nyumba angalau ya bati na mahitaji mengine mengi ya kila siku. Sasa unapowazuia kuuza kwa kisingizio eti kuna upungufu wa chakula mimi naona ni kuwaonea, labda serikali ingefanya kitu kimoja kuhakikisha kwamba wakulima wanapata mahitaji yao na chakula hakitoki nje ya nchi ambacho ni serikali yenyewe kuwa wanunuzi wakuu wa mazao ya chakula pale ambapo mkulima atataka kuuza kwa ajili ya kujikimu.
 
mkuu tatizo ni moja kwenye swala zima la mazao unakuta ukipeleka mazao nje ni rahisi kuliko kusambaza nchini kwa mfno mtu wa rukwa anaona rahisi kuuza mahindi congo kwani wanamfuata wanunuzi kuliko hapa anaekufuata ni dalali afu malalamiko kibao kwa hiyo ni bora mtu auze nje kuliko hapa..
 
Sasa unapowazuia kuuza kwa kisingizio eti kuna upungufu wa chakula mimi naona ni kuwaonea, labda serikali ingefanya kitu kimoja kuhakikisha kwamba wakulima wanapata mahitaji yao na chakula hakitoki nje ya nchi ambacho ni serikali yenyewe kuwa wanunuzi wakuu wa mazao ya chakula pale ambapo mkulima atataka kuuza kwa ajili ya kujikimu.

....tena kwa bei nzuri.
 
Kauli hizi kwa hakika zinanikera....
I. Wakulima kuzuiwa kuuza mazao yao eti kisa huenda kukawa na uhaba mkubwa sana wa chakula baadaye! kauli hii huwa inatolewa na viongozi katika namna ya kuonyesha Mkulima anahurumiwa!

II. Huyu fulani (wanataja jina) anasema nini sasa? wakati yeye aliwahi kuwa Kiongozi, kwenye Serikali ya awamu fulani?

Ninakerwa kwasababu,

Kauli ya I: Mbona wafanyakazi waajiriwa Serikalini au kwenye sekta binafsi hawapewi mishahara yao kidogo kidogo, wakati twafahamu wengine ni walevi, wazinzi n.k.? Kwanini nao wasitendewe kama atendewavyo mkulima?

Kauli ya II: Hivi ni kosa kwa Mtanzania yeyote kuukosoa utawala uliopo madarakani sasa eti kisa tu aliwahi kuwa DC, RC, etc etc kwenye Serikali ya awamu fulani?

Ni kwanini lakini? I stand to be corrected!

Nyingine umesahau kali kuliko zote

"Anatafuta/unatafuta umaarufu"
 
Kwenye chakula napinga

na na wewe kwani serikali inapaswa kuwa makini kwa maslahi ya watanzania wote kikubwa ipandishe bei za mazao ili wakulima wanufaiki. Pili, unapokosoa jambo lazima tuone vitendo na sio maneno matupu. Kama mtu alikuwa dc, rc au waziri halafu hakutenda kile anacho hubiri baada ya kustaafu huyo ni mnafiki.
mkuu inawezekana wewe haujalima na kujua tabu ya kilimo cha bongo, ungejua hilo basi serikali ingemruhusu mkulima kuuza chakula kokote apendako na kama unahitaji kwa ajili ya nchi basi nunua na kuifadhi ili kumfanya mkulima aweze kupata mahitaji yake na kuinua maisha yake, kuliko kumuua masikini wakutupwa na hata hatukubali utendaji wao. yaani MKULIMA NAKUWA KAMA BEKI HASIFIWI HATA SIKU MOJA!
 
....tena kwa bei nzuri.
Sure, kama leo nilitune TBC1 nikamwona mkulima mmoja wa Mbozi anasema wakiuza mahindi kwenye masoko ya wananchi wanapata kama elfu nne kwa debe ambayo ni elfu 24 kwa gunia, lakini akasema wakiuza kwenye masoko ya serikali wanapata sh 320 kwa kilo kwa gunia lenye kilo kama 110 kutokana na maelezo ya yule mtu ni kama elfu 35, nikaona ni kitu kizuri lakini kama kutakuwa na ushindani na wafanyabiashara wa nje lazima bei ingekuwa zaidi ya hapo, mfano kwa mikoa ya Mwanza, Mara na Shinyanga debe moja sio chini ya elfu 8.
 
1. Amepotoshwa na washauri wake.
2. Nilipwe posho kwani mie manamba? (Shibuda)- kwani manamba si watu ?
 
Back
Top Bottom