Easyway
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 2,606
- 3,702
Kwenye ripoti ya kamati ya waziri Nchimbi , Mukama alitoa pendekezo lifuatalo,ninanukuu "Katibu mkuu wa CCM Wilson Mukama,alishauri kufanyiwa marekebisho kwenye sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 itakayoweka wazi shughuli ya vyama vya siasa baada ya uchaguzi mkuu. Akisisitiza kuwa shughuli ya za siasa baada ya uchaguzi mkuu zihamie bungeni kwa wanasiasa kuhoji mipango ya maendeleo ya Serikali na matumizi ya rasilimali za nachi na wananchi waachwe wachape kazi zao za maendeleo" mwisho wa kunukuu.
Nina maoni yafuatayo kwa Mukama:
Kazi mojawapo ya vyama vya siasa ni kufanya siasa muda wote bila kujali kama kuna uchaguzi mkuu au hakuna ili visiitwe vyama vya msimu na lengo la kufanya hivyo ni kujitangaza kwa kueneza sera zao na mikakati yao ili kujiandaa kwa uchaguzi mkuu unaofuata na uchaguzi wa serikali za mitaa kama uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014.
Hakuna mwananchi anayelazimishwa kushiriki kwenye shughuli za siasa hivyo si kweli kwamba shughuli za siasa zinasababisha wananchi wasichape kazi zao za maendeleo.
Je,kwa vyama ambavyo vilishiriki kwenye uchaguzi mkuu na havikupata mbunge/wabunge wao watahamishiaje shughuli za siasa bungeni? tusitunge sheria kwa sababu ya kukizuia chama fulani kufanya kazi zake za kujenga chama tuache wananchi wenyewe waamue kama waende kwenye mikutano ya vyama vya siasa au la.