Kauli hii inanikera, nifanyeje?

Fikiria kesi ndogo kama hii;
Amechelewa kurudi nyumbani; anakukuta uko nje; unamuuliza mbona umechelewa hivi ulikuwa wapi?
Jibu; Eh! Baba fulani nisiongee ma marafiki zangu eti kisa nitaulizwa? kama ni hivyo ni bora nikupishe waje wengine wajaribu!

Utajisikiaje kwa jibu la namna hiyo??? Inakera!

Ninakuelewa, ikifikia hapo inabidi uwahusishe wakubwa wa pande zote, ni vitu vidogo dogo lakini vinaweza kuwa vina msukumo wa nje au ni kwa sababu ya kuweka vitu bila kuvijadili kwa muda mrefu na inazaa dharau.

Usiruhusu hasira ikutawale. We differ in interpretations, huenda haaminishi unavyomaanisha.
 
Katika muda ambao tumeishi wote sikuwahi kujadili mambo yangu ya ndani na m2 yeyote! Huwa sipendi kutangaza udhaifu wa mwenzangu - nami pia sipendi atangaze udhaifu wangu. Namaanisha hata wazazi (upande wangu) wanajua kuwa tunaishi kwa amani ya hali ya juu kwa kuwa hawakuwahi kusikia kuwa tumekwaruzana; nisijue upande wake kwa kuwa kipindi tukiwa kwenye mtafaruku sm kutoka kwao huwa ni nyingi sana.
 
Zaidi ya miaka 10 unafikiri sijawahi kuzungumza naye tukiwa wawili? Ila washwahili wanasema tabia haina dawa! Kumvumilia ni kumfanya atoe mapembe na kuendekeza dharau ya kunitishia mara kwa mara akijua wazi kuwa sina mpango wa kuwa na mwanamke mwingine hata kama ikitokea tukatengana kwa sababu yoyote ile.

Tatizo kubwa ni namna anavyodekezwa na ndugu zake + wazazi wake!
Kuna wazee wetu ambao wamekaa zaidi ya hiyo miaka kumi unayoisema na wamekuwa wakivumiliana,sasa wewe mwenyewe kumbe unaweza kujua tatizo ni ndugu zake,kuna njia za kupita na kutatua tatizo hilo nadhani kabla ya kuoa ulichumbia kwa kutumia washenga hivyo unaweza maliza hili tatizo kwa njia hiyo.

Kutokuwa na mpango wa kuwa na mwanamke mwingine hata baada ya kuachana nae siwezi kulizungumzia na hata wewe hauko katika nafasi hiyo kwani hujui huwa inakuaje maisha baada ya kutengana yanavyokuwa,mwombe Mungu yasikukute tu maana Mungu ni mwingi wa mifano kwa wanadamu wake.

Pole kwa unayopitia,wenzako tunayapitia pia ingawa hayafanani na ya kwako.
 
MWANAMKE..!! Mie nawaogopa sana viumbe hawa jamani ..nawaogopa sana sana .. Sijui life langu litakuwaje, kungekuwa Na kijiulimwengu free from women I rather go there , stay and live there ..

Mkuu nenda jela, kule huwa kuna dunia ya wanaume peke yao na wanawake peke yao...
 
Kuna wazee wetu ambao wamekaa zaidi ya hiyo miaka kumi unayoisema na wamekuwa wakivumiliana,sasa wewe mwenyewe kumbe unaweza kujua tatizo ni ndugu zake,kuna njia za kupita na kutatua tatizo hilo nadhani kabla ya kuoa ulichumbia kwa kutumia washenga hivyo unaweza maliza hili tatizo kwa njia hiyo.

Kutokuwa na mpango wa kuwa na mwanamke mwingine hata baada ya kuachana nae siwezi kulizungumzia na hata wewe hauko katika nafasi hiyo kwani hujui huwa inakuaje maisha baada ya kutengana yanavyokuwa,mwombe Mungu yasikukute tu maana Mungu ni mwingi wa mifano kwa wanadamu wake.

Pole kwa unayopitia,wenzako tunayapitia pia ingawa hayafanani na ya kwako.

Hapo nimekupata mkuu!
 
Katika muda ambao tumeishi wote sikuwahi kujadili mambo yangu ya ndani na m2 yeyote! Huwa sipendi kutangaza udhaifu wa mwenzangu - nami pia sipendi atangaze udhaifu wangu. Namaanisha hata wazazi (upande wangu) wanajua kuwa tunaishi kwa amani ya hali ya juu kwa kuwa hawakuwahi kusikia kuwa tumekwaruzana; nisijue upande wake kwa kuwa kipindi tukiwa kwenye mtafaruku sm kutoka kwao huwa ni nyingi sana.

Ni muda sasa wa kulijadili na wazazi wa pande zote (au viongozi wa kidini). Hili sio la kulivaa peke yako, na inabidi kufanya haraka sana.

Ninakuhakikishia kuwa ana mengi moyoni ambayo kama akiyasema wewe utashangaa sana na Mungu akiwa kati yenu mtayamaliza na mtaishi vizuri tena, bado hamjafikia pabaya.

Nisamehe kwa kauli yangu ya kwanza kabisa, ila haya yote sikuyafahamu kabla, kuishi kwingi ni kuona mengi Kaka. Mungu akutangulie uiokoe ndoa.
 
inakera kweli, sasa
huyu mwananke ana matatizo, kwanza yawezekana anasema hivo kukutisha
unajua tena wanawake akili zao ndogo saana, pili yawezekana ni mambo
ambayo aliyazoea kuyasema bila kumaanisha, au background ya familia yake
wazazi walikua wanatishana mbele ya watoto mambo kama hayo, ila kama
hana makosa makubwa ya kumwacha, mpende mtimizie ilyo haki yake, nadhani
mtaelewana kwani kupishana kimawazao katika familia ya wawili mbona
kawaida, mwanaume pia unakosea, ila maana na msingi kusaeheana wongo
jombaaaaaa

Una maanisha nini unaposema wanawake akili zao ndogo?
 
ni muda sasa wa kulijadili na wazazi wa pande zote (au viongozi wa kidini). Hili sio la kulivaa peke yako, na inabidi kufanya haraka sana.

Ninakuhakikishia kuwa ana mengi moyoni ambayo kama akiyasema wewe utashangaa sana na mungu akiwa kati yenu mtayamaliza na mtaishi vizuri tena, bado hamjafikia pabaya.

Nisamehe kwa kauli yangu ya kwanza kabisa, ila haya yote sikuyafahamu kabla, kuishi kwingi ni kuona mengi kaka. Mungu akutangulie uiokoe ndoa.

hapo mkuu nimekuelewa; ila sasa umri huu kuanza mazingira ya kushitakiana haipendezi kabisa. Mungu anitangulie; nimejaribu kusoma vitabu vingi vinavyohusu mambo ya ndoa - ushauri wote unaishia kwenye kumuomba mungu! Unaomba hadi unafika katikati unayakumbuka maudhi na kukatisha sara. Duh!
 
Una maanisha nini unaposema wanawake akili zao ndogo?

Anamaanisha kuwa akili za wanawake ni ndogo ukilinganisha na za wanaume au hujaelewa ndg yangu.
Ndo maana kwa serikali ya Jamhuri ya Tannzania kuna wizara ya kushughulikia mambo ya wanawake na watoto.
 
inakera kweli, sasa huyu mwananke ana matatizo, kwanza yawezekana anasema hivo kukutisha unajua tena wanawake akili zao ndogo saana, pili yawezekana ni mambo ambayo aliyazoea kuyasema bila kumaanisha, au background ya familia yake wazazi walikua wanatishana mbele ya watoto mambo kama hayo, ila kama hana makosa makubwa ya kumwacha, mpende mtimizie ilyo haki yake, nadhani mtaelewana kwani kupishana kimawazao katika familia ya wawili mbona kawaida, mwanaume pia unakosea, ila maana na msingi kusaeheana wongo jombaaaaaa

Khaaaaa! Mie sikubali upite bila kupingwa. Tena utuombe radhi. Jamani eeeh, snowhite cacico FP madame X BADILI TABIA gfsonwin MamDENYI Smiles Preta Smile @King'asti Kipipi nyumba kubwa na wadada wengine wote njooni mumsome huyu smallvile anasema wanawake akili zao ndogo saana!
 
Anamaanisha kuwa akili za wanawake ni ndogo ukilinganisha na za wanaume au hujaelewa ndg yangu.
Ndo maana kwa serikali ya Jamhuri ya Tannzania kuna wizara ya kushughulikia mambo ya wanawake na watoto.

Una DHARAU wewe!
 
Hili suala ni gumu sana kama hauto tambua kuwa akili yako na mkeo zipo tofauti. Mwanamke ni mtu ambaye anapenda muda wote akutie kwenye himaya yake ya kutawala ili kila analosema uwe unakubali tu bila kulifanyia uchunguzi. Mwanamke akikuta kila jamba analokuambia wewe, halafu wewe hujibu neno lazima akutafutie sababu kuangalia je unampenda, na akigundua kuwa unampenda ndipo ana anza visa vya kutaka kurudi nyumbani kwao ili akuone wewe utasemaje. Sasa ili aache kusema hivyo na ukitaka kugundua kuwa nimnafiki siku akisema hivyo mwambie achukue vitu vyake aende ataona lazima atakataa kwenda kwao. kitu kinachotakiwa usitake ufananishe akili yako na ya kwake. Yaani ukiona umepata mke ambaye akili zinafanana ni kushukuru Mungu.
 
Wala si mbaya,yeye ametamani ulimwengu usio na wanawake ndio kaelekezwa ulipo,ubaya uko wapi hapo?

MAGEREZA sio ulimwengu; akiamua kuishi bila wanawake anaweza tu! Bahati mbaya mimi tayari nimeishaingia kwenye trap
 
Back
Top Bottom